Watangazaji wa TV wajifunze uvaaji wa nguo

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,886
Kitu ambacho huwa kinanikera ni uvaaji wa nguo wa baadhi ya watangazaji kwenye TV.

Kuna baadhi ya watangazaji wanatia kinyaa uvaaji wa nguo zao. Leo nilikuwa naangalia taarifa ya habari TBC yaani yuletangazaji wa kike alikiwa amevaa hovyo kweli. Makeup hazijakaa fresh kabisa.

Hivi huwa hakuna washauri mpaka mtu anatokea kwenye public?

Kwa kweli watangazaji jitahidini kuvaa nguo vizuri. Kwani ku match guo mbona simple tu?

Yangu hayo tu.
 
ungeweka na picha kwa sababu maelezo hayajitoshelezi kwa ambaye hajaangalia taarifa ya habbari
 
ungeweka na picha kwa sababu maelezo hayajitoshelezi kwa ambaye hajaangalia taarifa ya habbari
Sijaongelea taarifa ya leo nimetoa mfano tu kuhusu leo. Ila wapo wengi sana kwenye TV za bongo.
 
Nawakubal wale wa Citizen tv ya Kenya, ingawa huwa siangalii kila siku ila kwa hizo mara chache, nadhan wanavaa vizur na kuvutia ..!!

TBC ni hovyo kila idara, Studio, Picha, Habari, watangazaji n.k.

Hatuwasemi kwa nia mbaya, bali ili mjirekebishe, mnatutia aibu sana ..!!
 
We ni mnafiki
Ndugu kwenye ukweli huwa tunasema. Tukiangalia TV za nchi zingine ni tofauti mno. Huu sio unafiki ni ukweli. Wanatakiwa wabadilike.

Hasemi hivi kwa kuwatukana ni kuwaeleza vitu gani sisi watazamaji vinatuboa. Na mwisho wa siku kufanikisha.
 
Labda unawazungumzia wale wenye nywele za asili na hata usoni unaona yuko natural tu?
Hapana ndugu. Ninaongelea jinsi ya uvaaji wa nguo na sehemu husika.
Jinsi ya ku match nguo, uwekaji wa makeup. Unakuta mtu kavaa viatu vyekundu, suruali ya njano shati la zambarau tai yeusi na koti jeupe. Huu uvaaji gani sasa. N:B huu ni mfano tu kuonesha kukerwa na uvaaji wa baadhi ya watangazaji.
 
Mnunulie hzo unazotaka avae
Kila mtu anatakiwa kuipenda kazi yake. Huenda labda hawajui. Kupangilia nguo sio kwamba ni utajiri ni utaratibu tu. Ninasema hivyo kwasababu tukiangalia watangazaji wa nchi zingine nguo wanavaa fresh tu.

Kunasiku moja nilishangaa sana kuna mtangazaji mmoja wa clouds TV. Sijui anaitwa kipanya yaani alikuwa amevaa kama anaenda kulima. Miguuni kavaa yeboyebo na jinsi alivyokuwa mamevaa kuanzia juu mpaka chini hovyo kabisa.
Siku ile alikuwa anamuhoji mama Salima Kikwete.
 
Tatizo siyo watangazaji kwa sababu wao wanakuja na nguo zao za nyumbani, bali ni mfumo wa vituo
 
Tatizo siyo watangazaji bali ni sera au mfumo wa kituo husika cha utangazaji katika baadhi ya mashirika ya utangazaji mfano Supersport wao wana sare kabisa zinazovaliwa na mtangazaji awapo kazini au studio. Sasa televisheni zetu mtangazaji anakuja na nguo yake ya nyumbani na hivyo huwezi kumchagulia cha kuvaa. Yaani huyo uliyemuona ujuwe ndo katokelezea japo wewe unamkandia. Utandawazi baba.
 
Back
Top Bottom