Mtangazaji gani ulimjengea picha tofauti na jinsi alivyo, kuanzia kimuonekano, umri na uvaaji pindi ulipomsikiliza kwa mara ya kwanza radioni

Mlundilwa Jr

JF-Expert Member
Dec 11, 2019
2,889
4,295
Vipi mambo wakubwa, wana JF, vijana kwa wazeee

Ebhana leo nimekaa nimetafakari jinsi hii technolojia ilivyokua na kusababisha mambo mengi kuwa mubashara, sijui kama nitakuwa nimeeleweka na Mada yangu.

Anyway me Kuna watangazaji wengi sana niliokuwa nawafuatilia miaka hiyo ya nyuma wakati huo hakuna hii mitandao ya kijamii na hata sasa ninapomsikiliza mtangazaji yeyote ktk Radio ikiwa sijawahi kumuona huwa namtengezea picha kuwa huyu mtu yupo hivi kuanzia muonekano umri na hata uvaaji wake

Wa kwanza

1. Fredrick Bundala
Huyu jamaa kipindi hicho namfuatilia kupitia RFA ktk kipindi chake Cha sintosahau jinsi alivyokuwa anakifungua kipindi na alivyokuwa anajitambulisha basi nilikuwa namvutia picha kuwa huyu jamaa kavaa suti kali na ni mtu mmoja ambaye ana muonekano kama mkurugenzi Fulani hivi yaani nilijua jamaa ni miongoni mwa wasomi wa level Fulani, kiukweli jamaa alinivutia Sana jinsi alivyokuwa anajitambulisha pindi anapofunga kipindi na hata alipokuwa anakifungua kipindi

2. Esielo Mafuru
Huyu jamaa kwa mara ya kwanza namsikia nilijua ni mtu Fulani ambae age imekwenda Sana na hii nikutokana na sauti yake.

Nakumbuka nilianza kumsikia ktk kipindi Cha habari na muziki pale Tbc taifa, Kumbe ni dogo tuu pia kuna siku nilikuwa na ndg yangu tunasikiliza kipindi wakati huo Esielo Mafuru alikuwa anatangaza nikamuuliza hivi huyu mtangazaji anayetangaza unahisi ana miaka mingapi? Yule ndg yangu akaniambia kama 70 hivi nilicheka Sana.

3. Millard Ayo
Huyu jamaa kwa mara ya kwanza namsikiliza kupitia Amplifaya. Nilidhani ni jamaa Fulani kaenda hewani halafu anapenda kuvaa mashati ya mikono mirefu na suruali.

Kumbe jamaa jamaa nikafupi na bishoo kishenzi yaani mitupio yake ni tshrt na bukta huku kapelo kageuza.

4.Fredwaa
RIP, kwakweli jinsi nilivyomjengea taswira na nikaja kumuona Leaders club kipindi Fulani kumbe ndivyo alivyo
Kwani kipindi ana host rfa ktk kipindi chake Cha sindano Tano za moto nilijuwa tuu huyu jamaa atakuwa mbavu halafu anamwili mkubwa ndivyo alivyokuwa kimtindo nilimuotea.

5.Miriamu Migomba
Huyu mwanadada nilimjengea taswira Fulani hivi, kuwa ni msichana mwembamba na anapenda kuvaa vitopu na hiyo ni kutokana na sauti yake kuwa nyororo na nyembamba

Nimekuja kumuona kwenye Tv Kumbe ni bonge la mama na nguo zake ni madera.

Wapo wengi ila acha niishie hapo
Note; wakati nawasikiliza hao presenters nilikuwa nipo mbwinde huko ambako ukinunua maji ya kandolo mfuko unaambiwa urudishe au ukinunua ubuyu vimbegu unaambiwa urudishe.
 
isack gamba

mbase wake na alvyo havipishani


misanya bingi huyu najuaga ni white mwenye kipara cha mkapa alafu bonge anavaa miwani ya mkapa yaani bosi bosi flani hivi

ila mpk anakufa sijamwona live wala hata kwa tv
 
Back
Top Bottom