Watangazaji na Lugha

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Kwa kawaida mimi sio mpenzi wa kusikiliza radio , ni mara chache sana huwa nasikiliza kwa sababu maalumu , Leo kwa bahati nzuri nilikuwa nasikiliza machache kutoka kituo cha clouds FM .

Mtangazaji Dina Marios , alikuwa anaongelea Tukio la ajali mkoani Manyari huko Babati , Nakumbuka alisema kitu kama hichi “ KUNA AJALI IMETOKEA BABATU , NA WATU NANE WAMEUWAWA WENGINE 3 KUJERUHIWA “

Nikashituka kidogo , nilisikia neno hilo kuuwawa , na bado mtangazaji huyo na mwenzake aliyekuwa nae studio hakuomba radhi na wala msimamizi wa matangazo hayo hakusema chochote kile , inaelekea alipatia sana .

Nikafikiria mfano , kuna ndugu wa marehemu anasikiliza matangazo hayo halafu asikie kwamba Ndugu yake aliuwawa katika ajali hiyo atachukuliaje ? je akiamua kwenda mahakamani kudai ushahidi na maelezo zaidi ya waliotekeleza mauaji hayo atakuwa na makosa yoyote ?

Waandishi na watangazaji wengi Tanzania kwa sasa hawafuati maadili ya utangazaji na uandishi kiasi kwamba hata wengine tunasita kufungulia radio zao , kusoma magazeti yao na hata kujibizana nao katika makala wanazoandika au kusambaza katika magazeti .

Ninauhakika chama cha waandishi wa habari na watangazaji wanajua mambo haya na ni lazima wachukuliwe kwa umakini zaidi ili hapo mbeleni watu wasiongee vitu vya ajabu wakasababisha hata mauaji katika baadhi ya jamii .

Mfano Nchini Somalia , Waandishi wengi wa habari wanaouwawa nikwa sababu ya kukosa maadili ya utangazaji , wanatangaza vitu visivyoeleweka kwa mahakama za kiisilamu na wananchi badala yake wanachochea vita zaidi na wao kuuliwa mitaani .

Sawa na hapa tu , waandishi wanavyoripoti kuhusu mgogoro wa tarime na zile koo , njia zao za utangazaji na ushabiki zinachochea fujo na vurugu zaidi katika jamii hizo husika .

Vyombo vya habari viwe mbele katika kuhakikisha waandishi na watangazaji wao wanafuata maadili ya uandishi pamoja na mila na desturi za mtanzania wanavyotangaza na kuripoti habari zao au matukio au uchambuzi wao .
 
Watangazaji wengi sana wa redio hii ni bogus sana mbona! Yaani wewe unashangaa leo? Wala mimi sishangai sana. Ungekuwa unasema waliotangaza ni RTD ama Radio One ningeshangaa, maana hawa at least wako serious na habari zao, lkn sio clouds FM. Kama huamini hebu jaribu kuomba elimu zao hao watangazaji, unaweza kukuta hakuna hata mmoja mwenye elimu ya uandishi wa habari.
 
Watangazaji wengi siku hizi ni ma-DJ's, sasa DJ na kutangaza habari wapi na wapi. Wanachoniuzi zaidi hata wakikosea huwa hawajui kuomba radhi tena usiombe ukakuta wako wawili studio ndo kwanza watakuwa wanachekacheka tu
 
Mnasahau kuwa kigezo cha kufanya kazi clouds kigezo ni kuwa miss Ilala, Temeke au Kinondoni, na sio elimu ya uandishi wa habari
 
Unajua Tatizo kubwa la ndugu zetu wa Radio na Tv tuseme ni Kwanza lugha yenyewe ya Kiswahili nafikiri inawapita kushoto sasa ninawasiwasi maana huku kwenye ung'eng'e ndio kabisaaa. Pili wengi wao sidhani kama wamekwenda vizuri shule husika kwa maana ya Uandishi wa Habari na Utangazaji. Na tatu tukubali kwamba Kazi za siku hizi hasa za Redio na Tv hapa Bongo watu wanawachukua watoto wa dada zao, shangazi na wajomba na hasa hasa waajari wengi wanapenda kuwachukua wale warembo waliokosa Zawadi wakati wa mashindano ila wanajua kusoma na wanasura nzuri basi hapo ajira Fasta.

Isitoshe hata Ukabila fulani hivi upo ingawa sikatai uwepo kulingana na historia ya kuelimika ya hapo kale lakini sasa unakuta LAFUDHI yaani "Accent" ya kutamkwa kwa Maneno siyo halisia. Jaribu siku moja Kuangalia Taarifa ya Habari au Kipima Joto ITV ukutane na Bwana Mmoja anaitwa Steven Chuwa
 
haya ni matokeo ya kupeana ajira kwa kujuana, kufahamiana toka shuleni na kujua nani alikuwa bishoo wa nguvu enzi zake, ajira za nani anapenda muziki wa aina gani..............its hopeless!! Tatizo ni kwamba vijana wengi wana- subscribe kwa hizi redio mjinga na wanafikiri its a cool thing.

Ingekuwa vema hawa watangazaji wawe wanapitia kazi zao kabla kwenda hewani..........usiombe ukatazama Channel TEN asubuhi wakati wa magazeti..utalia!! Maana inaumiza pale ambapo mtu anatoa tafsiri kosefu ya kichwa cha habari.

Anyway hainishitui maana inaelekea watu wamekuwa complacent na matukio yanayowazunguka. Hata Rais wetu kashikilia "dummy check" iliyoandikwa kwa maneno laki 2 na kwa tarakimu laki 3, tunaelekea wapi!!!
 
watangazaji wengi hasa hao wa Clouds fm ni hopeless kabisa .yaani kazi yao ni kuopngea mambo ya watu kwa ujumla wamefanya hii redfio kama kijiwe chao cha kuongelea mambo ya watu wengine hasa hcho kipindi cha leo tena hakina maadili kabisa
 
Kwa mtazamo wangu, tunaodhani kuwa tunajua lugha ya Kiwahili ni wengi sana. Lakini, kinyume chake ni kuwa wengi wetu hatuijui lugha hii kwa ufasaha. Hata sisi tulioandika humu ukumbini hatuijui lugha hii kwa kiasi tunachokifiria. Mtu akikaa chini kutuchambua, hatachukua muda mrefu kuyaona makosa yetu.

Kitu kibaya zaidi ni kwamba ama hatujui kama hatujui au hatutaki kukubali kuwa hatujui. Kwa hiyo, ni lazima tujue na tukubali kuwa wanao kiharibu au wasiojua Kiswahili fasaha si Watangazaji na Waandishi peke yao bali ni sisi sote.

Tukifikia hatua hii, itakuwa ni mwanzo mzuri sana wa kuibadilisha lugha hii na kuiweka katika mizania ya kuheshimika, kupendwa, kuimarishwa na kuendelezwa katika misingi bora.

Katika kila lugha kuna ile lugha inayokubalika kama lugha ya mitaani. Lakini, tunapoichukua ile lugha ya mitaani na kuiingiza katika shule. redioni, magazetini, kwenye televisheni, mahakamani, bungeni na sehemu stahiki, huo ndio unakuwa mwanzo wa kuiporomosha lugha hiyo katika ujumla wake.

Kwa mfano: hatusemi "kitu hichi" bali tunasema "kitu hiki." Na katika wingi wake, tunasema "vitu hivi." Utagundua mara moja kuwa Ndugu Shy naye tayari kishafanya makosa katika makala yake hii inayokosoa Watangazaji wa Radio Clouds.

Badala ya kuwa walimu, tungekubali kuwa wanafunzi wazuri, tukajifunza kwa bidii lugha yetu hii adhimu. Huu ni urithi wetu wa kujivunia na ni urithi wa vizazi vyetu vinavyokuja.

Tuna mtindo pia ambao mimi binafsi nautumia kama wengi wengine. Mtindo ambao nauita "mtindo mbaya." Huu ni ule mtindo wa kuchanganya lugha, tunao uita Swanglish. Huu mtindo unaudhi sana. Hata pale ambapo lipo neno rahisi na la kawaida, mtu atapenyeza hapo neno la Kiingereza. Hata kama yule anayezungumza naye hatajua maana ya lile neno. Hali ambayo inaufanya ujumbe usifike unakokusudiwa.

Mara nyingi, dhamira hapo ni kuashiria usomi. Yaani, kwetu sisi usomi ni kujua Kiingereza. La haula, laiti tungejua, duniani kuna wasomi wengi mno ambao hawajui Kiingereza.

Imefika wakati, tuwajibike kuijivunia lugha yetu hii ya Kiswahili.
 
Tukiwa kwenye somo la lugha, maandishi fasaha ni kuuawa, siyo kuuwawa.
 
Nakumbuka alisema kitu kama hichi " KUNA AJALI IMETOKEA BABATU , NA WATU NANE WAMEUWAWA WENGINE 3 KUJERUHIWA "

Nikashituka kidogo , nilisikia neno hilo kuuwawa , na bado mtangazaji huyo na mwenzake aliyekuwa nae studio hakuomba radhi na wala msimamizi wa matangazo hayo hakusema chochote kile , inaelekea alipatia sana .

Ukiniuliza mtangazaji amekosea wapi?
Nitakuambia amekosea kutamka BABATI na KUUAWA, sentensi iliyobaki kwangu mimi ni sahihi. Lakini hii kuuawa naweza kuikubali kutokana na lugha ya mtaani anayoitumia 'Mtango' kwa maneno kama kuuwawa, baadawe n.k kiasi kwamba naona imekubalika.

Kwa ujumla kiswahili kwa sasa kiko mahututi, msimamizi wa matangazo na yeye inawezekana aliona sawa. Mradi ujumbe muhimu ulifika kwa wasikilizaji.
 
Watangazaji wengi sana wa redio hii ni bogus sana mbona! Yaani wewe unashangaa leo? Wala mimi sishangai sana. Ungekuwa unasema waliotangaza ni RTD ama Radio One ningeshangaa, maana hawa at least wako serious na habari zao, lkn sio clouds FM. Kama huamini hebu jaribu kuomba elimu zao hao watangazaji, unaweza kukuta hakuna hata mmoja mwenye elimu ya uandishi wa habari.

Ni kweli maana kufanya mizaa katika kutangaza ndio zao. Kumekuwa na makosa mbali mbali katika kukitumia Kiswahili na wakati huo huo jamii inategemea hao ndiyo role-model wetu wa kufundisha Kiswahili kwa njia ya radio.
 
Anyway hainishitui maana inaelekea watu wamekuwa complacent na matukio yanayowazunguka. Hata Rais wetu kashikilia "dummy check" iliyoandikwa kwa maneno laki 2 na kwa tarakimu laki 3, tunaelekea wapi!!!
Bi mkubwa bwana.. teh teh kwi kwi, Muungwana sidhani kama kuna chuo maarufu kitakachompa honoraria causa.

Nasikia alipewa Mareaknani na kina tapeli Andrew Young
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom