watangazaji kuweni makini mnapotangaza!

watangazaji kuweni makini mnapotangaza!

bigcell

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
219
Reaction score
60
Wakuu kwema? usiku wa kuamkia leo wakati narejea home kutoka kuwapa pole wahanga wa mabomu ya gongo la mboto,niliikuta radio One inatumbuiza miziki laini,meseji za kuwaliwaza wafiwa,wahanga Walionusurika na milipuko ya mabomu ya g.mboto. Ila kitu kimoja ambacho nilishindwa kumuelewa mtangazaji wa kipindi Gadna James a.k.a King G, wakati akitafsiri au kuuelezea asili ya wimbo,nilimnukuu akisema ' kuna wakati fulani miaka ya zamani kulitokea tetemeko kubwa sana duniani,ila sikumbuki ni nchi gani na mwaka gani,ndipo walipojikusanya wanamuziki wengi na kuamua kutunga wimbo wenye urefu wa dk 7 kwa ajili kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi. Namaliza kumnukuu.Wimbo ukaanza ni 'We are the world' ambao ulitungwa na Michael Jackson na Lionel Richie na kuwashirikisha wanamuziki 45.Wimbo ulitungwa jan 1985 na kurekodiwa mach '85, mahususi kwa ajili ya baa la njaa lilotokea afrika kuanzia mwaka 1982-85 barani afrika ktk baadhi ya nchi esp Sudan,Ethiopia na somali.Naomba aelimishe uma wa tz.
 
WATANGAZAJI WETU HATA HISTORIA HAWAJUI? CRAP:coffee::coffee::coffee::coffee::laugh:
 
Hao ni ma-mc na sio watangazaji!

Ni kweli, hawa watangazaji wetu ni ma-MC's wa kwenye minuso na sio radio personality.
Radio personality ughaibuni ni profession tena yenye mshiko wa nguvu ambako imagine mtu kama Howard Stein alisaini na Sirius Satellite Radio, 5-year contract worth about $500 million!!!. Hela yake hakuna cha Beckham, Torres, wala Kobe!!
Naona hapo redio stations zimevamiwa na hao wenye matokeo ya form IV kuishia kupata "D" mbili, kichwani ni pumba tupu.
 
....hizi kali sana!
My friend anaperform radio station mkoa fulani....hana ujuzi na taaluma hiyo but ni MC.
Naona ujanja na sauti ndio CV zao kupresent kwa hizo radio stations etc.
 
Kuna mwingine anaitwa CYPRIAN MUSIBA wa magic fm. siku ya valentine day alitangaza na kusisitiza kuwa mwanzilishi wa siku hiyo St. Valentine (hakujua kama hata ni saint) eti alikuwa hapendi vijana waoe bali alikuwa anapendekeza vijana wa kiume kugonga mademu na kuwaacha i.e. St Valentine alipendekeza vijana wasioe. I WAS SHOCKED. Na huyo Gadna James a.k.a King G ni hao hao kina 'MISIBA'
 
Dah Rais muongo media nayo hivyo hivyo ooohooo Mungu tusaidie
 
Ni kweli kabisa baadhi ya watangazaji hawana general knowledge hasa historia, jiografia na hata Kiswahili, yaani kuna wakati wanachapia lugha mpaka utashangaa, utani, maneno ya ovyo ovyo inakuwa kama studio ni kijiwe fulani hivi. Hawawezi -ku-visiolize wasikilizaji wao ni akina nani. Kwa kweli wamiliki wa vituo vya redio wawe makini wakati wa kuajiri watangazaji.
Hongera TBC, Radio One na RFA kwa kuwa na watangazaji wengi wazuri na wanaojua nini wanachofanya, wako serious na kazi.
 
out of context, out of reality...sijui tunaelekea wapi nchi hii....kwani huo wimbo unagusa vipi kweli reality wa watu wetu waliofiwa, majeruhi, watu waliopoteza property etc...in this context of tragedy of gombo la mboto? Sad sad indeed
 
wakuu kwema? Usiku wa kuamkia leo wakati narejea home kutoka kuwapa pole wahanga wa mabomu ya gongo la mboto,niliikuta radio one inatumbuiza miziki laini,meseji za kuwaliwaza wafiwa,wahanga walionusurika na milipuko ya mabomu ya g.mboto. Ila kitu kimoja ambacho nilishindwa kumuelewa mtangazaji wa kipindi gadna james a.k.a king g, wakati akitafsiri au kuuelezea asili ya wimbo,nilimnukuu akisema ' kuna wakati fulani miaka ya zamani kulitokea tetemeko kubwa sana duniani,ila sikumbuki ni nchi gani na mwaka gani,ndipo walipojikusanya wanamuziki wengi na kuamua kutunga wimbo wenye urefu wa dk 7 kwa ajili kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi. Namaliza kumnukuu.wimbo ukaanza ni 'we are the world' ambao ulitungwa na michael jackson na lionel richie na kuwashirikisha wanamuziki 45.wimbo ulitungwa jan 1985 na kurekodiwa mach '85, mahususi kwa ajili ya baa la njaa lilotokea afrika kuanzia mwaka 1982-85 barani afrika ktk baadhi ya nchi esp sudan,ethiopia na somali.naomba aelimishe uma wa tz.
hatuna watangazaji sikuhizi tuna matapeli wa redione/clouds fm/nk huo upuuzi umeimbwa pia jana cluods bahati akuelezea maana alijua atachemka kijana mmoja alikuwa itv nw clouds.....alinibore alipoesema wakazi wa lugalo inabidi mjiandae jinsi ya kuyakabili mabomu dem'n kijana huna adabu kabisa
 
Huo ni uzembe wa mtangazaji kani siku hizi kila kitu kipo mtandaoni.

hao ni wavivu wa kusoma mitandao. wabadilike.
 
Hili ni tatizo la kitaifa...watu hawana muda wa kusoma na kufatili mambo..yaani alishidwa ku google kidogo tu kwenye simu yake na kupata details za wimbo huo kabla kusema takataka hizo..yeye mwenyewe hajui hata tetemeko lilitokea wapi...yaani uhuni uhuni kama anafanya comedy kwenye kipindi kigumu.
 
Hayo ni matokeo ya kuajiri CHEAP LABOUR! Wamiliki wa vituo hivyo hawajajua madhara ya kuajiri watu wasio proffesionals, wanajishushia hadhi!
 
Msimshambulie sana huyo mtangazaji, amekosea kidogo tu...labda ni kati wa watangazaji vijana amabao hawajacheki historia na kujua kuwa 'we are the world - Haiti remix' iliyotengenezwa na Wyclef Jean kuchangia maafa ta tetemeko la ardhi Haiti ilikuwa ni 'remix' lakini yeye akidhani ndio 'first version'!

Ukweli ni kwamba 'we are the world' uliimbwa tena mwaka jana kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi Haiti!
 
Hawa watu wa ajabu sana....J3 Regina Malekwa wa Clouds akimbwembwesha ujio wa valentine day akasema mpenzi wa Shakespeare anaitwa Romeo Juliet
 
Huu ni ugonjwa unaosumbua redio zetu nyingi. Kuna muda wanachefua wanaweka vi mijadala vya kijingajinga visivyoelimisha zaidi ya umalaya. HEKO -TBC, RFA na R/ONE.
 
Back
Top Bottom