watangazaji kuweni makini mnapotangaza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

watangazaji kuweni makini mnapotangaza!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bigcell, Feb 18, 2011.

 1. bigcell

  bigcell JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Wakuu kwema? usiku wa kuamkia leo wakati narejea home kutoka kuwapa pole wahanga wa mabomu ya gongo la mboto,niliikuta radio inatumbuiza miziki laini,meseji za kuwaliwaza wafiwa,wahanga Walionusurika na milipuko ya mabomu ya g.mboto. Ila kitu kimoja ambacho nilishindwa kumuelewa mtangazaji wa kipindi Gadna James a.k.a King G, wakati akitafsiri au kuuelezea asili ya wimbo,nilimnukuu akisema ' kuna wakati fulani miaka ya zamani kulitokea tetemeko kubwa sana duniani,ila sikumbuki ni nchi gani na mwaka gani,ndipo walipojikusanya wanamuziki wengi na kuamua kutunga wimbo wenye urefu wa dk 7 kwa ajili kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi. Namaliza kumnukuu.Wimbo ukaanza ni 'We are the world' ambao ulitungwa na Michael Jackson na Lionel Richie na kuwashirikisha wanamuziki 45.Wimbo ulitungwa jan 1985 na kurekodiwa mach '85, mahususi kwa ajili ya baa la njaa lilotokea afrika kuanzia mwaka 1982-85 barani afrika ktk baadhi ya nchi esp Sudan,Ethiopia na somali.Naomba aelimishe uma wa tz.
   
 2. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hapo unena kuuu.Basi wangepika nyimbo za maomborezo kuliko kujipigia tu nyimbo.Thank
   
 3. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hao ndio watangazaji wenu wa kibongo bongo, pumba tupu, eti mtangazaji huna uhakika na ujumbe unaotaka kuwapa wananchi na bado unawadanganya."kuna wakati fulani miaka ya zamani kulitokea tetemeko kubwa sana duniani,ila sikumbuki ni nchi gani na mwaka gani"
  haya bwana, kazi kwenu
   
 4. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  :laugh:

  Huyo mtangazaji ameakisi tabia yetu halisi waTanzania, kuleta usanii kwenye kila jambo hata kama unapotosha...

  :laugh:
   
 5. s

  shosti JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  :laugh::laugh::laugh::coffee:
   
 6. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hapo sijui nani kajichanganya wewe , yeye au wote . KUna We r the World mbili, moja uliyo iongelea na nyingine ilikua a remake kwa ajili ya kuchangia maafa ya tetemeko la Ardhi la Haiti , sasa sijui huyu mtangazaji alipo sema "zamani" alikua na maana ya zamani ipi na labda alikua ana maana ya Haiti ila akakosa nyimbo hiyo mpya akapiga ile ya zamani au labda alielezea sema wewe hukujua kama kuna "We r the world " mpya iliyo fanyika karibuni.
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  We're the world ya kwanza iliwashirikisha akina Lionel Richie, Michael J, Harry Belafonte n.k. na ilikuwa mahususi kwa ajili ya Janga la njaa kule Ethiopia na jirani.
  Kama Gardner anasema anakumbuka miaka 1985 ni wazi alimaanisha hii ya kwanza. Kama amemtaja Michael ni wazi alimaanisha hii ya kwanza.
  We're the world ya pili ilikuwa mwaka jana baada ya tetemeko, na hii ilikuwa Remake ikiwa na Lionel Richie na vijana wengine. Micheal Jackson hakuwepo then.
  Kwa jinsi ya maelezo yalivyo ni dhahiri G amejichanganya, (We're the world, Njaa, Michael Jackson,Tetemeko, Remake we're the world) haviwezi kutengeneza paragraph moja kamili bila kutofautisha.
   
 8. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hivi Clouds hawana website ambayo unaweza kutoa feedback??
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Sio Clouds, redio one.
   
 10. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Unashangaa?!!! Mi niliwahi kumsikia mtangazaji akifafanua kuwa Jasusi ni liJangili au Jambazi lililoshindikana kwenye jamii (Radio capita FM)
   
Loading...