Kama ndo hivyo mambo yanaenda basi kazi tunayo....Ndugu yangu pole saana kama una ndoto hizo sahau kabisa kwani kama unatarajia kuomba kazi TTB au TANAPA, NI ngomu saana kuipata kwani kuna watu wamejijengea himaya huko na familia zao
unless una mtu wa..............? malizia
WANA JF!
Hapa nchini Finland mjini Helsinki yapo maonesho ya kimataifa ya kutangaza utalii. Karibu nchi zote duniani zimeleta wawakilishi wa kutangaza vivutio vyao hapa ikiwa ni pamoja na jirani zetu wa Kenya.
Cha kushangaza kama kawaida ya Watanzania, jamaa waliotumwa kuiwakilisha nchi yetu katika maonesho haya ya siku saba, walikuwa kwenye banda lao kwa siku moja na nusu tu. Baada ya hapo jamaa wamepanda boti na ninavyo tuma taarifa hii wapo nchini Sweden watumbua kwa raha zao. Cha ajabu Rais wa nchi ya Finland amepita kuangalia na kujionea shughuli katika maonesho haya na alipo fika banda la Tanzania alishangaa kuona analazimika kujiokotea mwenyewe vipeperushi bila kuona wataalam wa utalii Tanzania ili kupata maelezo ya kina kuhusu vivutio vyetu. Vile vile watu wengi hapa wameonyesha nia ya kutembelea Tanzania kwani walikuwa wamejazana kwenye banda na kushangaa kuona halia watu wa kuwapa maelezo.
Wana jamvi hii imekaa je??????
Kaka unatakiwa kuwa mzalendo angalau katika kiwango cha mawazo, zile ni kodi zetu ambazo zinatakiwa zitumike kwa mujibu wa taratibu na kanuni za kazi kama walivyoelekezwa wakati wanaondoka kwa safari hiyo. Kama kila mtu atakuwa anapiga akipata nafasi wanao tutawaachia nini nchi hii?Hahahaaa!! MBONA RAIS NA YEYE ALI STAREHE KWENYE BEMBEA ??? Hayo ma meli yanayozunguka usiku mzima yana starehe kabisa kabisa..!! Hata ingekuwa mimi nadhani ningetupilia mbali vipeperushi uchwara na kuingia Casino za kwenye Boat kula raha ndani ya BIRKA CRUISER. Usinikumbushe huko Scandinavia mkuu..! Fedha zenyewe ziletwazo na watalii wakina Zakia wamezibandua vya kutosha. Tanzania ni nchi ya UKIPATA NAFASI PIGA..!!!
Kaka unatakiwa kuwa mzalendo angalau katika kiwango cha mawazo, zile ni kodi zetu ambazo zinatakiwa zitumike kwa mujibu wa taratibu na kanuni za kazi kama walivyoelekezwa wakati wanaondoka kwa safari hiyo. Kama kila mtu atakuwa anapiga akipata nafasi wanao tutawaachia nini nchi hii?
Kama ndo hivyo mambo yanaenda basi kazi tunayo....
WANA JF!
Hapa nchini Finland mjini Helsinki yapo maonesho ya kimataifa ya kutangaza utalii. Karibu nchi zote duniani zimeleta wawakilishi wa kutangaza vivutio vyao hapa ikiwa ni pamoja na jirani zetu wa Kenya.
Cha kushangaza kama kawaida ya Watanzania, jamaa waliotumwa kuiwakilisha nchi yetu katika maonesho haya ya siku saba, walikuwa kwenye banda lao kwa siku moja na nusu tu. Baada ya hapo jamaa wamepanda boti na ninavyo tuma taarifa hii wapo nchini Sweden watumbua kwa raha zao. Cha ajabu Rais wa nchi ya Finland amepita kuangalia na kujionea shughuli katika maonesho haya na alipo fika banda la Tanzania alishangaa kuona analazimika kujiokotea mwenyewe vipeperushi bila kuona wataalam wa utalii Tanzania ili kupata maelezo ya kina kuhusu vivutio vyetu. Vile vile watu wengi hapa wameonyesha nia ya kutembelea Tanzania kwani walikuwa wamejazana kwenye banda na kushangaa kuona halia watu wa kuwapa maelezo.
Wana jamvi hii imekaa je??????
Kama ni kweli hebu mpelekee sms Mheshimiwa Rais. Ataifanyia kazi. Hana masihara mheshimiwa. Believe you me.
Mkuu nimeogopeshwa sana na hizi habari, sasa haka kaujuzi kangu nikipata napenda sana nije kukatumia hapo nyumbani kwa faida ya jamii nzima.........pls naomba ushauri wako nini cha kufanya ili kuepuka yote hayo....kuna mambo mengine yanatendeka yanatia kichefuchefu kabisa, hali ndo hivyo kwa taarifa yako ukibahataika ukaingia utaundiwa visa mpaka ukimbie mwenyewe
Hao ndiyo wabongo haswa.
Wakirudi Tanzania utashangaa wanapewa promosheni, kwani huenda katika ile posho yao kulikuwa na shea fulani ya bosi; kwa hiyo hawana wasiwasi kabisa.
Hebu unaweza kutuambia banda la wenzetu waKenya lilikuwa katika hali gani? najua kuwa wako serious sana katika hiyo sekta ya utalii.
[/COLOR]
HESHIMA MBELE NA MASLAHI YA WATANZANIA MBELE.
Mkuu Kichuguu!
Habari ya banda la wenzetu Kenya ilikuwa ni balaa. Jamaa walikuja wakiwa wamekamilika na kwamba wanaujuwa wajibu na kazi iliyowapeleka Finland. Banda lilikuwa linawakilisha kila kivutio kilichopo nchini Kenya. licha ya vivutio vya Kenya, pia walikuwa na poster kubwa " A LAND WITH SO MUCH TO OFFER" DISCOVER THE MAGIC OF AFRICA "VIEW KILIMANJARO THROUGH KENYA". Na mambo mengi mno kiasi kwamba nilijisikia kufa. Niliona kila kilichokuwa kizuri ndani ya lile banda kilikuwa ni cha kwetu.
Kilichotaka kiniua ni pale nilipoona jamaa wamekuja na wataalam wa kuuza safari. Watu walikuwa wananunua "FULL TOUR PACKAGES", tayari kwa kusafiri kwenda Kenya kipindi cha summer. Mfano walikuwa wame-organize na AURINKO MATKAT ambao hawa ni travel operator ili kuuza full packages.
Nilishindwa kuamini kile nilikuwa nakiona wenzetu wanakifanya sisi ndio kwanza tumekimbilia boat na kuacha kabisa kile kilichotupeleka.
Je, huko TTB na kwingineko hakuna wataalam wa utalii na masoko jamaniiiiiiiie??????????? Hivi aliyetuloga amekwisha kufa nini? Inauma mno.
Wana JF tusaidiane katika hili jamani!!! Nadhani si wakati mwafaka wa kufumbia macho mambo kama haya.
Nawasilisha.