Watangaza utalii wageuka watalii scandinavia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watangaza utalii wageuka watalii scandinavia

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Selungo, Jan 25, 2010.

 1. S

  Selungo JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WANA JF!

  Hapa nchini Finland mjini Helsinki yapo maonesho ya kimataifa ya kutangaza utalii. Karibu nchi zote duniani zimeleta wawakilishi wa kutangaza vivutio vyao hapa ikiwa ni pamoja na jirani zetu wa Kenya.
  Cha kushangaza kama kawaida ya Watanzania, jamaa waliotumwa kuiwakilisha nchi yetu katika maonesho haya ya siku saba, walikuwa kwenye banda lao kwa siku moja na nusu tu. Baada ya hapo jamaa wamepanda boti na ninavyo tuma taarifa hii wapo nchini Sweden watumbua kwa raha zao. Cha ajabu Rais wa nchi ya Finland amepita kuangalia na kujionea shughuli katika maonesho haya na alipo fika banda la Tanzania alishangaa kuona analazimika kujiokotea mwenyewe vipeperushi bila kuona wataalam wa utalii Tanzania ili kupata maelezo ya kina kuhusu vivutio vyetu. Vile vile watu wengi hapa wameonyesha nia ya kutembelea Tanzania kwani walikuwa wamejazana kwenye banda na kushangaa kuona halia watu wa kuwapa maelezo.

  Wana jamvi hii imekaa je??????
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mhhhh...........

  hiii nchi kama imelogwa vile........................
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  selungo, hiyo ndio bongo...
  hatuko serious, ni mabingwa wa kuongea
  accountability is lacking
  hiyo wizara ndio usiseme
  halafu tunalipana kama mawaziri wa ulaya kwenda nje ya nchi
  wakati matumizi halisi hayazidi 40% ya advances\hizi zote ni costs za corruption na corrupt society, there is no ownership na nchi yetu wala rasilimali

  wewe umeleta hapa hiyo hoja na watawala wanaona, lakini utashangaa haohao watawala wanawapandisha vyeo hao watangaza utalii wetu waliokwenda finland kutalii

  bongo ni zaidi ya ubongo
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  yaani habari kama hizi mtu unaweza
  pata magonjwa ya ajabu tu mwisho wake..

  hii nchi inakufanya uwe depressed.........
  yaani kila mtu serikalini
  hajui wajibu wake...........
   
 5. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Tuamini kwamba aliyewatuma atahitaji repoti ya kazi watakaporudi, na ni hapo palipo ukweli uongo hujitenga. Kwa sababu maonyesho ya siku saba, wao wanmefanya siku moja na nusu ofcourse huu ni utani ambao kimaadili ya kazi watahitajika kuadhibiwa labda iwe hiyo kazi waliajiriwa na mjomba wao na ni kazi ya kifamilia vinginevyo usalama wao kikazi siuoni.
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Hamsemi Ukweli kuwa Nchi haina Viongozi wazuri, nchi imeoza wakumlaumu nani kama sio Viongozi wanao husika wa Wizara ya Utalii?Nchi imejaa Viongozi wala Rushwa na Mafisadi tutaendelea kweli jamani? kila kiongozi anakuwa Mfisadi Mla Rushwa na mwizi wa Mali ya Umma tutaendelea kweli?chaku shangaza hao wahusika wa hilo banda la Maonyesho wamekwenda nchini sweden kujirusha sasa kule walipotumwa kufanya shughuli za Maonyesho hawapo? Kutakuwa na Maendeleo kweli hapo kwetu Tanzania?Ama kweli MIAFRIKA BWANA NDIVYO ILIVYO
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mkuu hili linatapisha kabisa, ni zaidi ya kichefuchefu... hivi sheria yetu inasemaje hapa? kuna namna ya kuwashitaki kudai haki yetu? maana wamekula pesa yetu?
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  this is where we need to be massive and patriots
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wanatumia posho zao ambayo ni kodi za walala hoi kupigana mikasi na kupiga mitungi mamtoni badala ya kufanya kazi iliyowapeleka. Wabongo hatuko makini
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  mkuu..
  wao na mabosi wao wote wasaniii....
  tuombe mungu wapate waziri kama
  magufuli labda ndo unaweza kwenda
  kupeleka ripoti hii....but otherwise.....
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nadhani bado tuna wajibu na wananchi wenzetu hata kama viongozi wetu ni wabovu, we need to change...
   
 12. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Kama rais JK akienda nje anakwenda kwenye shopping na kubembea pamoja na kupima akili unafikiri wengine watafanya nini kama sio maajabu.
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  Mkuu mwenyewe anabembea sembuse hawa? ila tatizo ni elimu .utakuta hawa jamaa wamesomea mambo mengine kabisa ila wameweka na baba zao kwenye sehemu nyeti sAsa ww unategemea nini?
   
 14. _ BABA _

  _ BABA _ JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninaumia Moyo sana ninaposikia habari kama hizi......anyway ngoja nimalize masomo yangu ya fani ya UTALII then nije toa mchango wangu mdogo kwenye hii sector.......serious we guys have to change to the maximum but kwa mwendo huu maendeleo tutaishia kuyaona kwa wenzetu tu kila siku.
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Jan 25, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Hao ndiyo wabongo haswa.


  Wakirudi Tanzania utashangaa wanapewa promosheni, kwani huenda katika ile posho yao kulikuwa na shea fulani ya bosi; kwa hiyo hawana wasiwasi kabisa.


  Hebu unaweza kutuambia banda la wenzetu waKenya lilikuwa katika hali gani? najua kuwa wako serious sana katika hiyo sekta ya utalii.
   
 16. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #16
  Jan 25, 2010
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tusiwalaum, labda wanataka kufungua banda la kutangaza utalii sweden, inawezekana walisoma mazingira ya finland wakaona hakuna wateja wa kutosha, hivyo bora kufunga na kuhamia huko waliko sasa!
   
 17. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Watumishi wa serikalini wana matatizo hayo sana,wao badala ya kuenda kufanya kazi wanenda kutalii. Hawa jamaa wamelaaniwa.
   
 18. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ........Tena wanaweza kuzamia hawa huko huko mamtoni wasirudi tena bongo, kuna watu walipelekwa Canada kwenye semina, baada ya semina kwisha wakaamua kwenda kuzamia USA. Akili za baadhi ya watanzania muda mwingine mchemsho kweli kweli.
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wakishuka na ndege uwanjani, waongozwe mojakwamoja kwenye karandinga na kusomewa mashitaka ya uhujumu uchumi!
  Wametuaibisha sana washenzi hawa!
   
 20. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45

  Ndugu yangu pole saana kama una ndoto hizo sahau kabisa kwani kama unatarajia kuomba kazi TTB au TANAPA, NI ngomu saana kuipata kwani kuna watu wamejijengea himaya huko na familia zao

  unless una mtu wa..............? malizia
   
Loading...