Watanganyika watakiwa kuondoka Zanzibar!

Watanganyika watakiwa kuondoka Zanzibar!

Leo hii baadhi ya watanganyika wenzetu wa Jf na visogo vyao utadhani ncha za isosceles triangle ati wanajifanya ma-Malcom X kutetea machotara walioandikwa kwenye mabango ya UVCCM ilhali wao wenyewe wakichangamana na hao machotara wanakuwa treated kama mbwa tu.

Tuache unafiki suala la ubaguzi visiwani siyo la kisiasa ni la kihistoria na kijamii zaidi.
 
Je hii haiwezi kuwa nbinu ya kupenyeza majeshi kwa kisingizio cha kulinda amani halafu haohao wataonekana kwenye sanduku la kura
 
Wacheni propaganda za ujinga na uhuni katika jamii. Hii ni thread ya 2012 kabla ya UKAWA. Ukweli ni kuwa kura zilizozidi za Maalim Seif na kumpa ushindi mkubwa pamoja na ongezeko la idadi ya viti vya ubunge, uwakilishi na udiwani kwa CUF Zanzibar ni kutokana na kura za Watanganyika wakaazi wa Zanzibar. CUF na Wazanzibar wanatambua hilo. Watanganyika wengi ukiwauliza watakwambia wanajihisi wako salama Zanzibar kuliko wakiwa Dar es salaam. Na hili linathibitishwa kwa kuwepo Wamasai wengi huko hata kabla ya Lowasa kutoka CCM na kujiunga CHADEMA.

Zanzibar ni ya wote & all are welcome!
 
Leo hii baadhi ya watanganyika wenzetu wa Jf na visogo vyao utadhani ncha za isosceles triangle ati wanajifanya ma-Malcom X kutetea machotara walioandikwa kwenye mabango ya UVCCM ilhali wao wenyewe wakichangamana na hao machotara wanakuwa treated kama mbwa tu.

Tuache unafiki suala la ubaguzi visiwani siyo la kisiasa ni la kihistoria na kijamii zaidi.
Kuna baadhi ya watu wanazivaa siasa za Zanzibar bila kufahamu historia ya Zanzibar!

Kuna baadhi wanadhani tatizo ni CCM au CUF!

Ubaguzi unaotokea Zanzibar haukuanzishwa na CCM au CUF bali ni matunda ya historia.
 
Wacheni propaganda za ujinga na uhuni katika jamii. Hii ni thread ya 2012 kabla ya UKAWA. Ukweli ni kuwa kura zilizozidi za Maalim Seif na kumpa ushindi mkubwa pamoja na ongezeko la idadi ya viti vya ubunge, uwakilishi na udiwani kwa CUF Zanzibar ni kutokana na kura za Watanganyika wakaazi wa Zanzibar. CUF na Wazanzibar wanatambua hilo. Watanganyika wengi ukiwauliza watakwambia wanajihisi wako salama Zanzibar kuliko wakiwa Dar es salaam. Na hili linathibitishwa kwa kuwepo Wamasai wengi huko hata kabla ya Lowasa kutoka CCM na kujiunga CHADEMA.

Zanzibar ni ya wote & all are welcome!
Mkuu, umesoea Chuo gani cha uongo?
 
Wacheni propaganda za ujinga na uhuni katika jamii. Hii ni thread ya 2012 kabla ya UKAWA. Ukweli ni kuwa kura zilizozidi za Maalim Seif na kumpa ushindi mkubwa pamoja na ongezeko la idadi ya viti vya ubunge, uwakilishi na udiwani kwa CUF Zanzibar ni kutokana na kura za Watanganyika wakaazi wa Zanzibar. CUF na Wazanzibar wanatambua hilo. Watanganyika wengi ukiwauliza watakwambia wanajihisi wako salama Zanzibar kuliko wakiwa Dar es salaam. Na hili linathibitishwa kwa kuwepo Wamasai wengi huko hata kabla ya Lowasa kutoka CCM na kujiunga CHADEMA.

Zanzibar ni ya wote & all are welcome!
Wewe ulizijuaje kama ni kura za Watanganyika wakaazi wa Zanzibar?

Naomba unielimishe kwa sababu anayefahamu aina ya kura moja ni mpiga kura mwenyewe.
 
Wewe ulizijuaje kama ni kura za Watanganyika wakaazi wa Zanzibar?

Naomba unielimishe kwa sababu anayefahamu aina ya kura moja ni mpiga kura mwenyewe.

Kuna somo linaitwa statistics dude! Kama ulivyojuwa kama Wapemba wanapigia CUF. UKAWA imewaondoa hofu Watanganyika wakaazi na kuingia imani na CUF kwa kugunduwa kwamba hichi chama lengo lao kubwa ni kushika madaraka kutoka kwa CCM na sio chuki dhidi ya Watanzania wenzao. Na ndio maana CCM wakawa wanahangaika kuwanyang'anya vipande vya kupigia kura baadhi yao kwa vile propaganda yao dhidi ya CUF ilifanya kazi mpaka tu Lowasa alipojiunga na Chadema. Mimi personaly niliwahi kuwahoji Wamasai wengi tu na walinihakikishia kuwa watapigia kura CUF lakini walikuwa na hofu ya visasi kutoka kwa CCM dhidi yao. Wewe ulifikiria hizo kura za ziada zimetoka wapi. Kama hujui wapiga kura wako ni kina nani hiyo mikakati yako ya kampeni in future elections utaifanya vipi. It's all about statistics and that's what statisticians are paid for!
 
Yale yale ya South Africa.
Tumewaweka Mazimbu, morogoro hadi wakapata uhuru.
Tumekwenda kufanya kazi kwao, matokeo yake ni kuuawa kinyama.
Ndio litakalofuata huko Zanzibar.
The way the cookie crumbles in Zanznibar.

Wapemba nao wafunge maduka yao Dar es salaam?
Pazuri sana hapo!
Na hapa ndo wazenji wanapokosea kuchanganya dini na siasa.
waliowapora ushindi ni serikali iweje wachome makanisa?
Lakini niliwahi kusema humu kuwa ule waraka ulioenda kwa papa
ulikuwa na lengo la kutaka kuondoa lawama endapo haya tunayoyaona yataanza.

Sitamani serikali itumie nguvu,maana mataifa yote
yaliyotumia nguvu tunaona yanalia kila siku,
kushindana na mtu asiyethamini uhai wake
ina gharama kubwa kuliko maelewano.

Kama kweli CUF ilishinda Zanzibar wakabidhiwe
nchi yao,wakishindwa kuiongoza wananchi watawatoa kwa kura
kama walivyokichoka chama tawala wanataka kukitoa kwa kura
lakini watawala hawataki.

wIto wangu kwa wazanzibar,wasiunganishe siasa na dini.
maana hakuna uthibitisho wa wazi kawmba kwamba wafuasi
wa ccm ni wakristo.Endapo wataendelea kuchoma makanisa
basi itakuwa wazi kwamba wao shida yao si serikali bali ni kufuta ukristo
Zanzibar kitu ambacho kitazaa uhasama mkubwa.
 
Mkuu, umesoea Chuo gani cha uongo?

Hilo jina lako linaonesha kama wewe ni muhuni fulani tu, kwa hiyo kuni accuse mimi kuwa nimesomea uwongo, sioni ajabu. If you cant respect yourself with a dignified user name, I don't entirely expect you to respect others!
 
Yale yale ya South Africa.
Tumewaweka Mazimbu, morogoro hadi wakapata uhuru.
Tumekwenda kufanya kazi kwao, matokeo yake ni kuuawa kinyama.
Ndio litakalofuata huko Zanzibar.
The way the cookie crumbles in Zanznibar.

Wapemba nao wafunge maduka yao Dar es salaam?
Pazuri sana hapo!
Hii yote ni michezo ya kuigiza,Wazanzibar kama Wazanxibar hawana tatizo na mtu yeyote - hawawezi kuwasakama wabara wanao fanya kazi au biashara huko Zanzibar wakati wakijua wazi wazi kwamba kuna Waunguja na Pemba lukuki huku bara, mtu mwenye akili timamu hawezi kuhanzisha upuuzi huo ambao unaweza kuwa cost Wazanzibari dearly.

Binafsi natoa pendekezo kwa Dk.Magufuli ahunde kimya kimya timu ya watu wachache wenye maadili ya hali ya juu wafanye upepelezi wa kina ili wabaini ni akina nani wapo behind dalili hizi mbaya zinazo palilia uvunjivu wa amani nchini - upelelezi uhanzie kwa baadhi ya Viongozi wenzako huko Zanzibar -instinct zangu zinanieleza hawakwambii kila kitu, haya mambo ya sijui Uhamusho nk hayawezi kushamiri bila ya baraka za baadhi ya Viongozi wenzako ambao hampo pamoja kimkakati au kifikira wanakupa lip services tu lakini deep down hampo pamoja wanapenda sana Zanzibar ijitenge na Bara and they mean it, wanawatumia proxy group kuwasemea na kuanzisha vurugu zisizo kuwa na kichwa wala miguu.

Dk.Magufuli fuata nyayo za Baba wa Taifa ambaye alikuwa anawachukulia hatua kali sana wale wote walio kuwa wanafanya mbinu za chini chini za kutaka kuvunja muungano huku wakiwa ni wanachama ahi wa chama tawala, Kambarage alikuwa hawaonei aibu hata kidogo hata ukiwa ni rafiki wake vipi anakuweka ndani/kizuhizini - looking back now naona kumbe Baba wa Taifa alikuwa sahihi kabisa, sasa Dk.Magufuli anapaswa kumu-emulate Kambarage bila ya kufanya hivyo hawa watu watakuchanganya uwezi kujua umuamini nani umuhache nani, hawasemi openly lakini nakuhakikishia linapo kuja suala la muungano karibu wote lao moja bila ya kujali itikadi zao za vyama, mipasho ya Kizota ndio ilipaswa kuwafumbua macho wa Bara kuhusu kinacho jiri Visiwani, nayasema haya kwa nia njema tukiyafumbia macho Taifa letu litakuja kudhalilika kweli kutokana na masuala ya Zanzibar.
 
Kuna somo linaitwa statistics dude! Kama ulivyojuwa kama Wapemba wanapigia CUF. UKAWA imewaondoa hofu Watanganyika wakaazi na kuingia imani na CUF kwa kugunduwa kwamba hichi chama lengo lao kubwa ni kushika madaraka kutoka kwa CCM na sio chuki dhidi ya Watanzania wenzao. Na ndio maana CCM wakawa wanahangaika kuwanyang'anya vipande vya kupigia kura baadhi yao kwa vile propaganda yao dhidi ya CUF ilifanya kazi mpaka tu Lowasa alipojiunga na Chadema. Mimi personaly niliwahi kuwahoji Wamasai wengi tu na walinihakikishia kuwa watapigia kura CUF lakini walikuwa na hofu ya visasi kutoka kwa CCM dhidi yao. Wewe ulifikiria hizo kura za ziada zimetoka wapi. Kama hujui wapiga kura wako ni kina nani hiyo mikakati yako ya kampeni in future elections utaifanya vipi. It's all about statistics and that's what statisticians are paid for!
Ulichokiandika hapa ni fikra na hisia zako ambazo hazibebwi na chembe yoyote ya scientific evidence!
 
0000001moto.jpg

Moto ukiwaka katikati ya mtaa mjini Zanzibar jana baada ya vurugu za wanaharakati kupinga muungano na kudai Zanzibar ijitawale. Picha na Salma Said


Baada ya kuwapo kwa amani kwa takribani mwaka mmoja tangu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, vurugu na hali ya wasiwasi zimeibuka tena baada ya wanaharakati wa Kiislam kufanya maandamano kutaka uhuru wa visiwa hivyo.

Zanzibar ilijikuta katika hali tete kiusalama tangu mwaka 1995 baadaya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais, ambayo Chama cha Mapinduzi (CCM) kiilibuka kidedea na Chama cha Wananchi (CUF) kupinga, lakini uhasama huo ulizikwa Julai 31 mwaka 2010, baada ya kura ya maoni ya kuunda Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa.

Lakini kuanzia juzi usiku hadi jana jioni mji wa Unguja na viunga vyake ulitikiswa na mabomu ya kutoa machozi ambayo polisi waliyatumia kutawanya mamia ya wanaharakati hao wa Kiislam wakiongozwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI).

Mabomu ya machozi yalipigwa mfululizo juzi usiku na kuendelea kutwa nzima jana, hivyo kuathiri shughuli za biashara, ibada katika makanisa mbalimbali na kusababisha hofu kwa wananchi.

Kwa muda wa saa takriban mbili hivi kati ya saa 3:00 na saa 5:00 asubuhi, helkopta ya polisi ilikuwa ikipasua anga la Zanzibar ambalo lilikuwa limetandwa na moshi uliotokana na mabomu ya machozi pia uchomaji wa matairi ya magari.


Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa aliwaambia waandishi wa habari kuwa wafuasi hao wamefanya uharibifu mkubwa ikiwa pamoja na kuchoma moto makanisa mawili na kwamba, watu saba akiwamo Imamu wa Msikiti wa Bizeredi, Maalim Mussa Juma wanaotuhumiwa na matukio hayo wamekamatwa na jeshi hilo.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Askofu Dickoson Maganga alisema watu wasiojulikana walivamia kanisa lao eneo la Kariakoo Mjini Zanzibar mnamo saa 4.30 usiku na kuvunja ukuta, kuchoma viti vya plasitiki pamoja na gari yake.

Chanzo cha vurugu hizo kinatajwa kuwa ni wanaharakati hao juzi kufanya mkusanyiko na maandamano makubwa ya kushtukiza ambayo yalizistua mamlaka za usalama visiwani humo, lakini baada ya kutawanyika jioni baadhi ya viongozi wa maandamano hayo walitiwa mbaroni.

Baada ya kukamatwa kwao, wafuasi wao walikusanyika makao makuu ya polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Madema, kushinikiza kutolewa kwa viongozi hao wanaoshikiliwa kituoni hapo.

Habari zaidi zinasema kutokana na hali ilivyo, askari polisi walitarajiwa kuongezwa visiwani humo, ili kusaidia kuimarisha hali ya usalama pia kuwadhibiti wahalifu ambao walikuwa wameanza kuelekea nje ya maeneo ya mji.

Tayari kuna taarifa kuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoka Tanzania bara jana mchana walingia Zanzibar kwa ajili ya kuongeza ulizi katika mji wa Unguja.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza hakuna kiongozi yoyote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) aliyetoa kauli kuhusu hali hiyo.

Kauli ya Polisi
Kamishna Mussa alisema jeshi lake litaendelea kuwasaka na kuwatia mikononi wote waliopanga fujo hizo pamoja na viongozi wote wa JUMIKI.

“Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar ndio iliyohusika na kuwachochea vijana kukusanyika na kufanya uharibifu ikiwemo kuchoma moto gari, kupanga mawe barabarani na kufanya hujuma mbalimbali kinyume cha sheria. Tutaendelea kuwasaka kwa gharama zote,” aliapa Kamishna Mussa.

Alifafanua kwamba kwa sasa mikusanyiko yote ya mihadhara ya kidini na vyama vya siasa, lazima ipate kibali cha polisi vyinginevyo jeshi lake litatumia nguvu za ziada kutawanya mikusanyiko hiyo ili kulinda sheria za nchi, amani na utulivu.

Hata hivyo, kamishna huyo wa polisi alijizuia kuhusisha harakati za Uamsho na chama cha siasa wala kutaja majina ya viongozi ambao tayari wanashikiliwa na jeshi lake.

“Mpaka sasa hivi sina majina yao kwa jumla, lakini tumewakamata viongozi wa Uamsho na tunatendelea kuwasaka lakini jina moja tu ndio ninalo ambalo ni Mussa Abdallah Juma,” alisema Kamishna huyo.

Hali bado tete
Wakati jeshi la polisi litoa onyo hilo, hali ya usalama ilionekana kuwa bado tete huku maeneo kadhaa ya Mji wa Zanzibar hasa Darajani na Michenzani ambako muda wote ni sehemu zenye harakati nyingi za biashara, jana zilikuwa zimebakia bila pilikapilika kutokana na askari waliojihami kufanya doria katika mitaa yote na kulipua mabomu kila penye kikundi cha watu waliokusanyika wakinywa kahawa.

Mitaa hiyo ilikuwa imechafuliwa kwa mawe, matofali na magogo yaliowekwa barabarani ili kuziba njia kwa ajili kuzuia magari yasipite huku mipira ya magari ikiwashwa moto na vijana hao.

Kwa upande wake Askofu Maganga akizungumzia uvamizi kisha uhalifu uliofanywa kanisani kwake alisema:

“Nasikitika sana kwa tukio hili ambalo tayari tumeiarifu polisi ambao jana (juzi), usiku walifika hapa wakishirikiana na kikosi cha kuzima moto na kufanikiwa kuuzima moto huo ambao kwa habati nzuri haujaathiri paa la kanisa letu,” alishukuru kiongozi huyo.

Alisema kundi la watu ambalo lilikuwa likitoa maneno ya kashfa na kutishia maisha ya waumini waliokuwa wakifanya ibada usiku huo, lilikatisha ibada hiyo pamoja na kusababisha uharibifu wa mali ya kanisa hilo yenye thamani ya zaidi ya Sh 100 millioni.

Kauli ya JUMIKI
Kutokana na hali hiyo, jumuiya hiyo jana ilitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari ikikanusha kuhusika na kuchochea watu kuchoma kanisa wala kuharibu mali za watu.

Hata hivyo, Katibu wa Jumuiya hiyo, Abdallah Said alisema katika taarifa hiyo kwamba jeshi la polisi linapaswa kubeba lawama kwa yote yaliotokea kutokana na kuvunja sheria na kuwakamata viongozi bila ya utaratibu wa busara.

“Uislamu ni dini ya amani na inahimiza ushirikiano na utulivu na hatuwezi kuwatuma watu kwenda kuvunja makanisa na kuharibu mali, kwa sababu ndani ya imani zetu tunajua hilo ni kosa na jambo ambalo halifai katika maamrisho ya dini yetu,” alisema Sheikh Abdallah.

Taarifa hiyo ilisema pia kwamba jumuiya hiyo imekuwa wazi katika kudai maslahi ya Zanzibar na sio vinginevyo na kuahidi kufanya hivyo kwa njia za amani, na iwapo watakuwa wamekosea basi wapo tayari kufikishwa katika vyombo vya sheria.

“Ni lazima polisi wajue kwamba tupo tayari kufanya kazi kwa misingi ya kisheria na hata kwa kujisalimisha tupo tayari, lakini ukamataji bila kufuata busara na sheria haukubaliki. Tunachokitaka ni kura ya maoni haraka na hilo tutaendelea kulidai,” alisisitiza katibu huyo wa JUMIKI.

Wakati viongozi wa Uamsho wakiendelea kutafutwa na jeshi la polisi, nyumba ya kiongozi aliyeongoza maandamano juzi Sheikh Farid Hadi Ahmed inadaiwa kuvunjwa milango usiku wa manane alipokuwa akiswakwa jeshi hilo.

Hata hivyo, taarifa hizo hazikuthibitishwa iwapo ni polisi waliofanya kitendo hicho au la, wanafamilia wanasema waligongewa milango na kutakiwa wafungue baada ya kutofungua walisikia kishindo kikubwa cha kusukumwa milango katika eneo la Mbuyuni Mjini Unguja.

Vijana katika mitaa ya Zanzibar jana walionekana wakiwa na hamasa kubwa wakidai kuendelea kuungana na viongozi wao kudai haki ya Zanzibar, pamoja na kutaka Zanzibar huru kutoka ndani ya mikono ya Muungano.

“Sisi tunachokitaka Zanzibar yetu watupige mabomu, watuue, watukamate lakini tunataka Zanzibar yetu na hatusikii lolote,” walisikika baadhi ya vijana.

Hada jana jioni vurugu katika badhi ya maeneo hususan Kwelekwe na njia ya Baa ya Amani zilikuwa zikiendelea na gari moja lilichomwa moto karibu na ofisi ya CCM.

Matukio kabla
Zanzibar imekuwa ikitawaliwa na matukio ya ghasia ambayo licha ya mihadhara hiyo ya Kiislam ilikuwa ni uhasama wa kisiasa kati ya vyama vikuu vya CUF na CCM, hatua ambayo iliwahi kusababisha mauaji ya Januari 27, mwaka 2001.

Lakini, uhasama huo wa kisiasa ambao ni wa kihistoria ulizikwa baada ya kura hiyo ya maoni na uchaguzi mkuu wa 2010 hatua ambayo imemfanya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa SMZ huku baadhi ya mawaziri pia wakitoka katika chama hicho.

Hata hivyo, wanaharakati hao wa Kiislam wameanza upya kuilipua Zanzibar wakishinikiza visiwa hivyo viwe taifa huru kwa kujitenga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zitto ataka tume ya uchunguzi
Katika hatua nyingine Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amemtaka Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aunde kikosi kazi maalum kwa ajili ya kudhibiti vurugu hizo na kuanza mazungumzo na pande zote kwa kuwa, "Hiki sio kitendo cha kudharau kabisa."

Alifafanua kwamba waliochoma nyumba za ibada wasakwe na kufikishwa mbele ya sheria mara moja na kuongeza, "Tusiruhusu hata kidogo wapuuzi wachache kutuingiza katika vurugu za kidini ili kufikia malengo yao ya kisiasa."

CHANZO: Gazeti la Mwananchi

Katika gazeti la Tanzania Daima

Kadhalika, kuna madai kuwa wafuasi wengine wa kundi hilo, walijigawa na kuanza kuzifuatilia nyumba wanamoishi wafanyabiashara na wafanyakazi wanaotoka Tanzania Bara na kuzishambuli kwa mawe, huku wakitoa maneno ya vitisho.

Mmoja wa wafanyakazi hao kutoka Bara, anayefanya kazi katika hoteli moja ya kitalii (jina linahifadhiwa), alikiri nyumba yao kushambuliwa vikali, na jana alilazimika kuhamia kwa rafiki zake ambao ni wenyeji wa visiwani hapa.


My concern: Tunakoelekea sijui ngoja nione movie itaishia wapi
Mkuu hivi kama uliwahi kutazama movie yabkihindi hapo huna haja ya kushangaa
 
Sioni hasara yoyote kama Muungano ukivunjika, hawa jama wz wanainyonya Tanganyika. Tunawabembeleza wa nini hawa? Binafsi sioni faida yoyote ya kuwabeba hawa jamaa, ni wa shari na wabaguzi wa dini kwa kutumia mwamvuri wa uisilam!!!!
Kati ya hao jamaa na ccm hivi waliotoa tamko la wahzbu na waafrika ni kina nani vile?
 
Najua baadhi watapinga lakini ukweli ni kwamba Zanzibar kuna itikadi za kidini pia. BAADHI ya waislam wanawachukia wakristo kwa imani kwamba ndio wanaoharibu utamaduni wa Wazanzibari na wakati mwingine ndio wanaoifanya CCM iendelee kutawala Zanzibar
 
"Wanaharakati wa kiislamu" duh hawa jamaa nawaogopa sana! Zenji wapewe chao tuu. Alshabab watatua hapa time si nyingi.
 
Ulichokiandika hapa ni fikra na hisia zako ambazo hazibebwi na chembe yoyote ya scientific evidence!

Sasa toa ukweli wako ulobebwa na scientific evidence kwamba Wazanzibari wanawachukia Watanganyika, Wanawapiga Wakristo ni magaidi na hujuma zote munazowatupia. Lakini haya yote hayatuzuwii sisi Watanganyika kwenda Zanzibar kutafuta maisha mapya. Hicho ndicho cha ajabu. Ugaidi wa Zanzibar ni bora kuliko usalama wa Dar es salaaam. Ninae rafiki yangu mmoja ni mshika fedha wa kanisa hapa Dar lakini watoto wake wote anawasomesha Zanzibar. Nilipomuuliza kwa nini anafanya hivyo, jawabu lake aliniambia kuwa Zanzibar kuna maadili mazuri
 
Back
Top Bottom