Watanganyika watakiwa kuondoka Zanzibar!

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
0000001moto.jpg

Moto ukiwaka katikati ya mtaa mjini Zanzibar jana baada ya vurugu za wanaharakati kupinga muungano na kudai Zanzibar ijitawale. Picha na Salma Said


Baada ya kuwapo kwa amani kwa takribani mwaka mmoja tangu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, vurugu na hali ya wasiwasi zimeibuka tena baada ya wanaharakati wa Kiislam kufanya maandamano kutaka uhuru wa visiwa hivyo.

Zanzibar ilijikuta katika hali tete kiusalama tangu mwaka 1995 baadaya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais, ambayo Chama cha Mapinduzi (CCM) kiilibuka kidedea na Chama cha Wananchi (CUF) kupinga, lakini uhasama huo ulizikwa Julai 31 mwaka 2010, baada ya kura ya maoni ya kuunda Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa.

Lakini kuanzia juzi usiku hadi jana jioni mji wa Unguja na viunga vyake ulitikiswa na mabomu ya kutoa machozi ambayo polisi waliyatumia kutawanya mamia ya wanaharakati hao wa Kiislam wakiongozwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI).

Mabomu ya machozi yalipigwa mfululizo juzi usiku na kuendelea kutwa nzima jana, hivyo kuathiri shughuli za biashara, ibada katika makanisa mbalimbali na kusababisha hofu kwa wananchi.

Kwa muda wa saa takriban mbili hivi kati ya saa 3:00 na saa 5:00 asubuhi, helkopta ya polisi ilikuwa ikipasua anga la Zanzibar ambalo lilikuwa limetandwa na moshi uliotokana na mabomu ya machozi pia uchomaji wa matairi ya magari.


Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa aliwaambia waandishi wa habari kuwa wafuasi hao wamefanya uharibifu mkubwa ikiwa pamoja na kuchoma moto makanisa mawili na kwamba, watu saba akiwamo Imamu wa Msikiti wa Bizeredi, Maalim Mussa Juma wanaotuhumiwa na matukio hayo wamekamatwa na jeshi hilo.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Askofu Dickoson Maganga alisema watu wasiojulikana walivamia kanisa lao eneo la Kariakoo Mjini Zanzibar mnamo saa 4.30 usiku na kuvunja ukuta, kuchoma viti vya plasitiki pamoja na gari yake.

Chanzo cha vurugu hizo kinatajwa kuwa ni wanaharakati hao juzi kufanya mkusanyiko na maandamano makubwa ya kushtukiza ambayo yalizistua mamlaka za usalama visiwani humo, lakini baada ya kutawanyika jioni baadhi ya viongozi wa maandamano hayo walitiwa mbaroni.

Baada ya kukamatwa kwao, wafuasi wao walikusanyika makao makuu ya polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Madema, kushinikiza kutolewa kwa viongozi hao wanaoshikiliwa kituoni hapo.

Habari zaidi zinasema kutokana na hali ilivyo, askari polisi walitarajiwa kuongezwa visiwani humo, ili kusaidia kuimarisha hali ya usalama pia kuwadhibiti wahalifu ambao walikuwa wameanza kuelekea nje ya maeneo ya mji.

Tayari kuna taarifa kuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoka Tanzania bara jana mchana walingia Zanzibar kwa ajili ya kuongeza ulizi katika mji wa Unguja.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza hakuna kiongozi yoyote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) aliyetoa kauli kuhusu hali hiyo.

Kauli ya Polisi
Kamishna Mussa alisema jeshi lake litaendelea kuwasaka na kuwatia mikononi wote waliopanga fujo hizo pamoja na viongozi wote wa JUMIKI.

“Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar ndio iliyohusika na kuwachochea vijana kukusanyika na kufanya uharibifu ikiwemo kuchoma moto gari, kupanga mawe barabarani na kufanya hujuma mbalimbali kinyume cha sheria. Tutaendelea kuwasaka kwa gharama zote,” aliapa Kamishna Mussa.

Alifafanua kwamba kwa sasa mikusanyiko yote ya mihadhara ya kidini na vyama vya siasa, lazima ipate kibali cha polisi vyinginevyo jeshi lake litatumia nguvu za ziada kutawanya mikusanyiko hiyo ili kulinda sheria za nchi, amani na utulivu.

Hata hivyo, kamishna huyo wa polisi alijizuia kuhusisha harakati za Uamsho na chama cha siasa wala kutaja majina ya viongozi ambao tayari wanashikiliwa na jeshi lake.

“Mpaka sasa hivi sina majina yao kwa jumla, lakini tumewakamata viongozi wa Uamsho na tunatendelea kuwasaka lakini jina moja tu ndio ninalo ambalo ni Mussa Abdallah Juma,” alisema Kamishna huyo.

Hali bado tete
Wakati jeshi la polisi litoa onyo hilo, hali ya usalama ilionekana kuwa bado tete huku maeneo kadhaa ya Mji wa Zanzibar hasa Darajani na Michenzani ambako muda wote ni sehemu zenye harakati nyingi za biashara, jana zilikuwa zimebakia bila pilikapilika kutokana na askari waliojihami kufanya doria katika mitaa yote na kulipua mabomu kila penye kikundi cha watu waliokusanyika wakinywa kahawa.

Mitaa hiyo ilikuwa imechafuliwa kwa mawe, matofali na magogo yaliowekwa barabarani ili kuziba njia kwa ajili kuzuia magari yasipite huku mipira ya magari ikiwashwa moto na vijana hao.

Kwa upande wake Askofu Maganga akizungumzia uvamizi kisha uhalifu uliofanywa kanisani kwake alisema:

“Nasikitika sana kwa tukio hili ambalo tayari tumeiarifu polisi ambao jana (juzi), usiku walifika hapa wakishirikiana na kikosi cha kuzima moto na kufanikiwa kuuzima moto huo ambao kwa habati nzuri haujaathiri paa la kanisa letu,” alishukuru kiongozi huyo.

Alisema kundi la watu ambalo lilikuwa likitoa maneno ya kashfa na kutishia maisha ya waumini waliokuwa wakifanya ibada usiku huo, lilikatisha ibada hiyo pamoja na kusababisha uharibifu wa mali ya kanisa hilo yenye thamani ya zaidi ya Sh 100 millioni.

Kauli ya JUMIKI
Kutokana na hali hiyo, jumuiya hiyo jana ilitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari ikikanusha kuhusika na kuchochea watu kuchoma kanisa wala kuharibu mali za watu.

Hata hivyo, Katibu wa Jumuiya hiyo, Abdallah Said alisema katika taarifa hiyo kwamba jeshi la polisi linapaswa kubeba lawama kwa yote yaliotokea kutokana na kuvunja sheria na kuwakamata viongozi bila ya utaratibu wa busara.

“Uislamu ni dini ya amani na inahimiza ushirikiano na utulivu na hatuwezi kuwatuma watu kwenda kuvunja makanisa na kuharibu mali, kwa sababu ndani ya imani zetu tunajua hilo ni kosa na jambo ambalo halifai katika maamrisho ya dini yetu,” alisema Sheikh Abdallah.

Taarifa hiyo ilisema pia kwamba jumuiya hiyo imekuwa wazi katika kudai maslahi ya Zanzibar na sio vinginevyo na kuahidi kufanya hivyo kwa njia za amani, na iwapo watakuwa wamekosea basi wapo tayari kufikishwa katika vyombo vya sheria.

“Ni lazima polisi wajue kwamba tupo tayari kufanya kazi kwa misingi ya kisheria na hata kwa kujisalimisha tupo tayari, lakini ukamataji bila kufuata busara na sheria haukubaliki. Tunachokitaka ni kura ya maoni haraka na hilo tutaendelea kulidai,” alisisitiza katibu huyo wa JUMIKI.

Wakati viongozi wa Uamsho wakiendelea kutafutwa na jeshi la polisi, nyumba ya kiongozi aliyeongoza maandamano juzi Sheikh Farid Hadi Ahmed inadaiwa kuvunjwa milango usiku wa manane alipokuwa akiswakwa jeshi hilo.

Hata hivyo, taarifa hizo hazikuthibitishwa iwapo ni polisi waliofanya kitendo hicho au la, wanafamilia wanasema waligongewa milango na kutakiwa wafungue baada ya kutofungua walisikia kishindo kikubwa cha kusukumwa milango katika eneo la Mbuyuni Mjini Unguja.

Vijana katika mitaa ya Zanzibar jana walionekana wakiwa na hamasa kubwa wakidai kuendelea kuungana na viongozi wao kudai haki ya Zanzibar, pamoja na kutaka Zanzibar huru kutoka ndani ya mikono ya Muungano.

“Sisi tunachokitaka Zanzibar yetu watupige mabomu, watuue, watukamate lakini tunataka Zanzibar yetu na hatusikii lolote,” walisikika baadhi ya vijana.

Hada jana jioni vurugu katika badhi ya maeneo hususan Kwelekwe na njia ya Baa ya Amani zilikuwa zikiendelea na gari moja lilichomwa moto karibu na ofisi ya CCM.

Matukio kabla
Zanzibar imekuwa ikitawaliwa na matukio ya ghasia ambayo licha ya mihadhara hiyo ya Kiislam ilikuwa ni uhasama wa kisiasa kati ya vyama vikuu vya CUF na CCM, hatua ambayo iliwahi kusababisha mauaji ya Januari 27, mwaka 2001.

Lakini, uhasama huo wa kisiasa ambao ni wa kihistoria ulizikwa baada ya kura hiyo ya maoni na uchaguzi mkuu wa 2010 hatua ambayo imemfanya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa SMZ huku baadhi ya mawaziri pia wakitoka katika chama hicho.

Hata hivyo, wanaharakati hao wa Kiislam wameanza upya kuilipua Zanzibar wakishinikiza visiwa hivyo viwe taifa huru kwa kujitenga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zitto ataka tume ya uchunguzi
Katika hatua nyingine Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amemtaka Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aunde kikosi kazi maalum kwa ajili ya kudhibiti vurugu hizo na kuanza mazungumzo na pande zote kwa kuwa, "Hiki sio kitendo cha kudharau kabisa."

Alifafanua kwamba waliochoma nyumba za ibada wasakwe na kufikishwa mbele ya sheria mara moja na kuongeza, "Tusiruhusu hata kidogo wapuuzi wachache kutuingiza katika vurugu za kidini ili kufikia malengo yao ya kisiasa."

CHANZO: Gazeti la Mwananchi

Katika gazeti la Tanzania Daima

Kadhalika, kuna madai kuwa wafuasi wengine wa kundi hilo, walijigawa na kuanza kuzifuatilia nyumba wanamoishi wafanyabiashara na wafanyakazi wanaotoka Tanzania Bara na kuzishambuli kwa mawe, huku wakitoa maneno ya vitisho.

Mmoja wa wafanyakazi hao kutoka Bara, anayefanya kazi katika hoteli moja ya kitalii (jina linahifadhiwa), alikiri nyumba yao kushambuliwa vikali, na jana alilazimika kuhamia kwa rafiki zake ambao ni wenyeji wa visiwani hapa.


My concern: Tunakoelekea sijui ngoja nione movie itaishia wapi
 
Warudi tu Tanganyika maana inakoelekea sasa itakuwa ni kuviziwa mtu unapotezewa uhai.
 
Yale yale ya South Africa.
Tumewaweka Mazimbu, morogoro hadi wakapata uhuru.
Tumekwenda kufanya kazi kwao, matokeo yake ni kuuawa kinyama.
Ndio litakalofuata huko Zanzibar.
The way the cookie crumbles in Zanznibar.

Wapemba nao wafunge maduka yao Dar es salaam?
Pazuri sana hapo!
 
Umeme kwenda zanzibar kituo chake kiko wapi naona ukimya wetu wanatuona mafala
 
Mwananchi

Mara baada ya kuchoma Makanisa mawili hapo jana kikundi cha uamsho kimepitisha na kusambaza karatasi milangoni mwa wakazi wanaodhaniwa kuwa ni wa kutoka bara na kutakiwa waondoke visiwani humo.

My cincern

Tunakoelekea sijui ngoja nione movie itaishia wapi

Wapuuzi sana hawa jamaa.
Wanafadhiliwa na ndugu zao toka bara.
Ngoja nasi tuwatimue huku.
Walio wa shetani utawaona tu na aya zao za kishetani.
 
Ndg zangu wakati wa kuwalea hawa Zanzibar ambao hawajui asili yao umekwisha cha muhimu nasi tuonyeshe hawa waliopo huku warudi kwao Pemba na Unguja, hakuna haja tena ya kuwaurumia maana wamelikoroga wenyewe na walinywe, tuanze kwa kuwakatia umeme!!!!!!!!!!!!!!!!
 
sipendi wanzanibari wanavyodeka. nadhani imefika mahali tuwatupe kama ganda la muwa. karibia kila kitu wanapata toka bara halafu ng'weee, ngw'eee, ng'weee. stupid
 
Haya ni madhara ya kuruhusu siasa kufanyika hata kwenye masuala ya kisheria. Hivi ingekuwaje kama Muungano huu ungelikuwa wa wazi na wa nchi ya Tanganyika na Zanzibar na hatimaye kuzaa kitu kinachoitwa Tanzania???

Hapa kwetu Muungano wa Zanzibar na nchi hewa "Inadhaniwa kuwa ni Tanganyika"....Kama Wazanzibar watawafukuza au kuua Watanganyika au Wakristo kuwa ndiyo target yao, basi ujue wamepotea sana. Na adhabu yao watakuja kujutia milele.
 
..Wapemba na Waunguja walioko Tanganyika wasihukumiwe kwa makosa ya ndugu zao walioko Zanzibar.

..Watanganyika walioko Zanzibar waondoke huko kama wanaona maisha yao yako hatarini na serikali ya zanzibar haiwezi kuwalinda.
 
Kisingizio chao cha Elimu duni wanataka kusingizia Muungano. Naomba kabla haujavunjika polisi wawape bano la nguvu tena kwa kosa la kuchoma makanisa mpaka wadebwede
 
Kwa jinsi ninavyozifahamu security establishment za nchi hii, hawa jamaa wanaweza wakapotea muda si mrefu,
 
Back
Top Bottom