Watanganyika na Wazanzibar, muda wa kupata Katiba Mpya na Tume Huru ni sasa

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,947
3,820
Mwaka huu na ujao 2022 katiba ni lazima ipatikane CCM wakitaka wasitake na kama hawataki wakae pembeni maana saa mbaya! Umma umeanza kuiva na uvumilivu juu ya genge la CCM lililojipenyeza kwenye vyombo vya dola sasa upo wazi na wanaofaidika na hayo si wengine ni wale walio juu ya mstari viongozi wa CCM waalio wengi, mwanachama wa kawaida wa CCM hana chake anatumiwa au yupo kama ganda tu kuhifadhi kilichomo ndani kwa ufupi wanatumika kirahisi sana.

Sasa Zanzibar hakuna mategemeo ya uchumi wa buluu wala kijani, muamko ni kudai tume mpya ya uchaguzi wanasema kwa hali na mali ni jitihadi juu ya nchi yao baada ya kumezwa na genge la waliojivalisha UCCM, tuseme kwao ni kama kisa cha mbweha aliejivalisha ngozi ya kondoo ndivyo CCM inavyoonekana.

Kinachohitajika ni umoja na mshikamano tu na ndipo Tanzania itakapokombolewa kwa mara nyingine badala ya uhuru, Kuna genge limeiteka Tanzania nalo ni CCM wachache wanachama wa kawaida wa CCM hawana chao,maana tunawaona mashule,kipato ni kile kile cha kuuza mboga na kubangaiza hapa na pale,Tanzania ni nchi Tajiri sana sana kuliko nchi nyingine ,inasemwa huko nje kama si ya kwanza ni ya pili kiujumla ,inakuwaje wachache tu ndio wanatudanganya na kujifanya wao ndio kila kitu,ni wezi na ni majambazi hawana budi kuondolewa kistaarabu.

Wala sioni sababu ya watu hawa kuungwa mkono kwa eti vyombo vingine vinafaidika na serikali yao ni uwongo, hakuna wanaofaidika ila manyigu wachache sana maana wengine wakistaafu na kuvua zana tunapishana nao sokoni wamevaa ndara na wengine wamebahatika kuwa na baiskeli. Hata malipo yao kuyapata ni mbinde.

Zanzibar upepo umeanza kuvuma tena sio wakitoto ile GNU karibu inapigwa teke kwani genge la CCM liliwekwa kwenye vipimo na kwa bahati mbaya wameshindwa kuviona wakavikwaa wanguwangu.

WaTanganyika wenzangu ngoma ikipigwa Zanzibar huchezwa maziwa Makuu. Katiba mpya na tume huru ndio nyimbo hakuna cha gaidi wala teroristi, Genge la CCM linataka kuipindisha agenda ila kwa kumkamata Mbowe wamezidi kuchochea kuni.

Wanachama kibao na wengi sana wa CCM waliokuwa wamebaki na kadi za CCM wanazirudisha na kuzichana zimezagaa njiani kwani wamechoka kutumiwa wanaofaidika na CCM walio kwenye mnyororo wa uongozi tu, wanachama kadi wanabaki na kadi na hawafaidiki hata na huduma za kawaida.

Shime wimbo popote ulipo ni KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi.
 
Kumkamata Mbowe ni kutaka kupindisha chombo kilichoanza kukamata direction kwa ufupi hakuna kurudi nyuma tena ni madai ya KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi ndio yawe yanapewa kipau mbele.

Hilo la Mbowe na Ugaidi ni lao CCM wamejitwisha waachiwe waende nalo na wakati likifuatiliwa kwa ukaribu na viongozi wa Chadema wasiache kasi waliyoianzisha kupigwa na chini na kudorora. Kama CCM hawataki KAtiba mpya na Tume huru Samia Suluhu abwage manyanga.
 
I shot the Sherrif but I swear it was on self defense.
 
Uongozi si lelemama, wananchi wanalia wanasononeka maana ndani ya bunge la Tanzania hakuna mbunge hata mmoja aliepigiwa kura za wananchi zilizohisabiwa na kumfanya ashinde KIHALALI, ni mizengwe na sasa tunawaona kila mmoja anashughulika na mlo wake tu siku ipite achukue mshahara wa bure.

Bunge halina nguvu wala meno lipo lipo tu, labda kunikama mimi mwananchi wa kawaida kisa nimesema bunge ni dhaifu na kujilabu lakini kiukweli lipo lipo tu, mwisho wa mwezi ufike nitiliwe changu watajiju.
 
Nyinyi tafuteni katiba ya chadema siokatiba ya wananchi. Katiba ya wananchi italetwa na wananchi wenyewee, sio hizofujo zenu
 
Kikundi kidogo cha wa CCM ambao hawataki katiba mpya ili walinde maslai yao. Katiba Mpya ni ss na haiepukiki
 
Nyinyi tafuteni katiba ya chadema siokatiba ya wananchi. Katiba ya wananchi italetwa na wananchi wenyewee, sio hizofujo zenu
Hivi unadhani kama tungekuwa na kambi kuu ya upinzani bungeni hii sheria ya tozo ya miamala ingepita?

Katiba iliyopitwa na wakati ndiyo sababu kubwa.

FUNGUA AKILI
 
Hivi unadhani kama tungekuwa na kambi kuu ya upinzani bungeni hii sheria ya tozo ya miamala ingepita?

Katiba iliyopitwa na wakati ndiyo sababu kubwa.

FUNGUA AKILI
Lipa kodi kwa maendeleo ya taifa. Katiba itatafutwa na watanzania wasio na mlengo wa chama chochote.
 
Back
Top Bottom