Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Na Joseph ngilisho Arusha, Watalii zaidi ya 150 kutoka nchini Israel wanatarajia kutua nchini Tanzania kesho jumatatu kwa ajili ya shughuli za Utalii ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ,Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi na Mawasiliano kutoka Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete alisema Agosti 2,watalii 150 wataingia nchini .
Aidha aisema watalii wengine 200 wanaotarajiwa kufika nchini Tanzania agosti 9 mwaka huu kutembelea vivutuio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini na pia watatembelea hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)
Alisema jumla ya watalii wapatao 550 watawasili nchini kwa nyakati tofauti tofauti na kutembelea hifadhi za Taifa zilizoko Kaskazini mwa Tanzania
Alisema kundi la kwanza linawasili leo (kesho) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) watakuwa watalii 150
Alisema ujio wa watalii hao unatokana na juhudi kubwa za utangazaji utalii katika dojo hilo linalokuwa kwa kasi pamoja na juhudi za makusudi zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya sita katika suala la kukabiliana na Uviko 19
Alisema kwa mujibu wa miongozo mbalimbali iliyotolewa na inayoendelea kutolewa na Shirika la Afya Duniania (WHO) ikiwemo utolewaji wa chanjo
"Watalii wanatoka Israeli moja kwa moja na ndege yao hadi Kia na watafika alfajiri ya leo,hii ni jitihada kubwa ya kutangaza utalii kati Tanzania na nchi ya Israeli"
Alisisitiza kuwa kuwepo kwa ubalozi wa Tanzania nchini Israeli kumechangia kiasi kikubwa ongezeko la watalii hao ambapo mwaka jana 2020Tanzania ilipokea zaidi ya watalii 1000 kutoka nchini Israeli waliofika kutembelea vivutuio mbalimbali na idadi inatarajia kuongezeka mwaka 2021