Watalii kutoka Israel kutua nchini Agosti 2, 2021

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
664
1,000
Na Joseph ngilisho Arusha, Watalii zaidi ya 150 kutoka nchini Israel wanatarajia kutua nchini Tanzania kesho jumatatu kwa ajili ya shughuli za Utalii ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ,Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi na Mawasiliano kutoka Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete alisema Agosti 2,watalii 150 wataingia nchini .

Aidha aisema watalii wengine 200 wanaotarajiwa kufika nchini Tanzania agosti 9 mwaka huu kutembelea vivutuio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini na pia watatembelea hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)

Alisema jumla ya watalii wapatao 550 watawasili nchini kwa nyakati tofauti tofauti na kutembelea hifadhi za Taifa zilizoko Kaskazini mwa Tanzania

Alisema kundi la kwanza linawasili leo (kesho) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) watakuwa watalii 150

Alisema ujio wa watalii hao unatokana na juhudi kubwa za utangazaji utalii katika dojo hilo linalokuwa kwa kasi pamoja na juhudi za makusudi zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya sita katika suala la kukabiliana na Uviko 19

Alisema kwa mujibu wa miongozo mbalimbali iliyotolewa na inayoendelea kutolewa na Shirika la Afya Duniania (WHO) ikiwemo utolewaji wa chanjo

"Watalii wanatoka Israeli moja kwa moja na ndege yao hadi Kia na watafika alfajiri ya leo,hii ni jitihada kubwa ya kutangaza utalii kati Tanzania na nchi ya Israeli"

Alisisitiza kuwa kuwepo kwa ubalozi wa Tanzania nchini Israeli kumechangia kiasi kikubwa ongezeko la watalii hao ambapo mwaka jana 2020Tanzania ilipokea zaidi ya watalii 1000 kutoka nchini Israeli waliofika kutembelea vivutuio mbalimbali na idadi inatarajia kuongezeka mwaka 2021
 
richie ze best

JF-Expert Member
Nov 4, 2013
297
500
Toka mwaka jana mwezi watisa mpaka mwezi watatu, Zanzibar ilipokea watalii wengi kuliko miaka miaka mitatu nyuma kabla ya corona, na wengine waliamia kabisa tokana na kuaminika Tz hakuna corona, mahotel, apartment na vi hotel mshenzi vilijaza, ila baada ya JPM kufa na kauli za mama kuhusu kuwepo na corona imeshusha idadi kubwa ya watalii, ikiwa wapolish, warusi na waukraine wamekata mguu kuja Zanzibar.

Kwa sasa utalii Zanzibar ni tia maji tia maji.

Nashangazwa kuingia wageni 500+ tunashangilia, wakati Zanzibar tulikua tunapokea wageni 900+ kila siku.
Tumeamua kucheza mziki wa kimagharibi, tukubaliane na khali.
 
Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
1,967
2,000
1×100=100
100×1=100

Ila katika biashara hazifanani kuna 100 moja ambayo ni bora kuliko nyingine.
 
Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
6,017
2,000
Toka mwaka jana mwezi watisa mpaka mwezi watatu, Zanzibar ilipokea watalii wengi kuliko miaka miaka mitatu nyuma kabla ya corona, na wengine waliamia kabisa tokana na kuaminika Tz hakuna corona, mahotel, apartment na vi hotel mshenzi vilijaza, ila baada ya JPM kufa na kauli za mama kuhusu kuwepo na corona imeshusha idadi kubwa ya watalii, ikiwa wapolish, warusi na waukraine wamekata mguu kuja Zanzibar.

Kwa sasa utalii Zanzibar ni tia maji tia maji.
Nashangazwa kuingia wageni 500+ tunashangilia, wakati Zanzibar tulikua tunapokea wageni 900+ kila siku.
Tumeamua kucheza mziki wa kimagharibi, tukubaliane na khali.
Walikuwa ni wataliii au usalama wa taifa la Israel walikuja kwa mishe maalumu
 
MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
2,792
2,000
Inakuwaje nchi kama Moroco inaingiza watalii Milion 10 plus kwa mwaka? Sisi tunachezea milion 2 na ila tambo za kutosha,

Juhudi zinahitajika sana
 
MC RAS PAROKO

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
584
1,000
Toka mwaka jana mwezi watisa mpaka mwezi watatu, Zanzibar ilipokea watalii wengi kuliko miaka miaka mitatu nyuma kabla ya corona, na wengine waliamia kabisa tokana na kuaminika Tz hakuna corona, mahotel, apartment na vi hotel mshenzi vilijaza, ila baada ya JPM kufa na kauli za mama kuhusu kuwepo na corona imeshusha idadi kubwa ya watalii, ikiwa wapolish, warusi na waukraine wamekata mguu kuja Zanzibar.
Acha kupotosha mkuu.. Warusi waliokua wakimiminika ZNZ walikuja sababu bei zilikua chini mno na hapakua na jam, duniani kote kulikua na makatazo ya kusafiri ila kwao Russia walishadungwa dawa na walikuja kwa bei robo na ilivyo kawaida. Znz iliyokua inajaza wataliano enzi za JK sio zanzibar ya warusi wenye pesa za kuvizia. Mfano mwepesi Keny walikua wanatoa takwim za waathirika wa covid kila siku na kuchukua tahadhari zote lkn bado walipokea wagen wengi zaidi ya Tz (wakati ya hayat JPM)

Kufunga macho sio njia salama kukwepa ngumi ya uso. anachokifanya SSH faida yake itaonekana leo na hata kesho..
 
Acha upuuzi, unajua hakuna wakati usafiri ulikua wa tabu na wa gharama kuliko kipindi ninachozungumzia, na sababu kubwa kulikua hakuna ndege za moja kwa moja baada ya kuwazuia ndege za kenya ama umesahau? Kabla ya kubwabwaja hebu jaribu hata ku google.
 
richie ze best

JF-Expert Member
Nov 4, 2013
297
500
Huu ni upuuzi na ujuha kusema takwimu zilitoka msimu wa JK wakati corona ilikuwako msimu wa magufuli, shame elim ya kata
 
MC RAS PAROKO

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
584
1,000
Ndege bei ikiwa juu na hotel inakua juu? watu wamelala kwa robo bei msimu huu wa covid na bado offa zipo nyingi hadi wa leo ila kwa kuwa unaamini unachosikia endelea kuamini.
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
56,221
2,000
Na sisi tuhakikishe hawaingii kama hawajachanjwa au kuwa na uthibitisho hawana mdudu...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom