Je, ni solar yenye ukubwa gani itanikidhi kwa haya mahitaji?

Alejandroz

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
327
376
Siku njema wana jf

Nataka nihamie kwenye nyumba isiyo naumeme na kwasasa hali yangu kifedha si njema sana, Nahitaji mfumo wa solar utakaoniwezesha kuwasha taa 4, kuchaji simu na kuangalia tv yangu ya inchi 32 walau kwa masaa machache huku nikijipanga kusogeza umeme.

Nimepita kwenye maduka kadhaa ya bidhaa za solar kila muuzaji ananiambia lake

Wengine wanasema Solar pannel ya watt 20 na betri ya N18 itanifaa

Wengine wanasema Solar pannel ya watti 30 na betri ya N26 itanifaa

Hivyo naomba unishauri kwa hii bajeti yangu ndogo naweza pata solar yenye nguvu kiasi gani ili angalau niweze kuangalia hata taarifa ya habari.
 
kama TV ingekua ni ya Solar, basi ingekua poa
hata battery na panel za size ndogo zingefaa

Inverter (zenyewe kama zenyewe) zinakula umeme unakuta nguvu yote ya battery inaishia huko
 
Siku njema wana jf

Nataka nihamie kwenye nyumba isiyo naumeme na kwasasa hali yangu kifedha si njema sana, Nahitaji mfumo wa solar utakaoniwezesha kuwasha taa 4...
Mkuu kama nyumba yako haiko mbali na nguzo, nakushauri fanya wiring hata sebuleni tu kisha uvute umeme ufurahie maisha huko kulikobaki utamalizia taratibu kadri mfuko wako utakavyo kuruhusu.

Hii ni kwasababu gharama utakayotumia kuweka huo mfumo wa umeme wa jua kulingana na mahitaji yako itakuwa iko sawa tu au inakaribiana kwa karibu na gharama za kuingiza umeme nyumbani kwako.

Pia hizi solar za siku hizi ni pasua kichwa unaweza ukaiweka vizuri tu halafu ndani ya miezi sita ukaanza kuona mapicha picha

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom