Makosa 5 tunayoyafanya wakati wa kuchaji simu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,882
155,860
Tumeona simu nyingi zinakufa betri (battery) kwa mda mfupi toka simu inunuliwe, hii inatokana na makosa ambayo tunafanya wakati wa kuchaji simu zetu.

Makosa gani na nini kifanyike?

Mara nyingi watumiaji hawajali namna bora ya kuchaji vifaa vyao hii ni kutokana na kutopata maelekezo mazuri kutoka kwa watengenezaji wa simu au wauzaji wa simu.

kuna vitu vya msingi vya kuzingatia pindi unapochaji simu yako....

Hii ni kuifanya simu ikae na chaji (charge) kwa mda mrefu na kutunza betri (battery) ya simu iweze kudumu zaidi.

Malalamiko ya simu kupoteza uwezo wa kukaa na chaji ni mengi, lakini watumiaji pia tunachangia kwa sehemu kubwa kwa kukosa elimu ya namna bora ya kuchaji simu

JINSI YA KUCHAJI SIMU YAKO VIZURI

1. TUMIA CHAJA RASMI (USE OFFICIAL CHARGER)

Kutumia chaja ambayo siyo rasmi au siyo maalumu kwa kifaa husika ni moja ya kosa ambalo hufanywa na watumiaji wengi,wengi huwa tunaangalia kama chaja inaingiliana na simu husika

kila simu huja na chaja yake kwenye box la simu ingali ikiwa mpya, tofauti na hapo inakupasa ununue chaja ya kifaa husika kutoka kwa wauzaji rasmi au duka la kuuza vifaa hivyo, sababu kila simu ina aina yake tofauti ya kupokea umeme.

2. USISUBIRI MPAKA SIMU IISHE CHAJI NDIPO UICHAJI

Inashauriwa kuchaji simu yako pindi ikifikia 20% ya uwezo wa betri na mara nyingi simu hutuma ujumbe au kuonyesha alama kwenye betri kuashiria betri inahitaji kuchajiwa. (20% ni bora zaidi)

Ukiona hizo dalili/alama unaweza kuichaji simu yako. wataalamu wanasema simu hupeleka chaji kwa haraka kuanzia 20% – 80% baada ya hapo inakuwa inapeleka taratibu mpaka kufikia 100% ambapo huacha kupeleka chaji.

3. ONDOA CHAJA KWENYE SOKETI PINDI SIMU INAPOJAA.

Simu za kisasa zina uwezo wa kuacha kupeleka chaji (cease charging) pindi simu ikifikisha 100% lakini hiyo haileti uhalali kuwa chaja itaacha kufanya kazi.

Tunashauriwa kuiondoa simu kwenye chaji pindi tu inapojaa.

4. USIWEKE SIMU SEHEMU YENYE JOTO WAKATI WA KUCHAJI.

Halijoto (Temperature) ni kitu cha muhimu sana katika kuboresha maisha ya betri ya simu,na hii huenda ni sababu kubwa ambayo hufanya betri za simu kuharibika

halijoto (Temperature) ikiwa kubwa hasa wakati wa kuchaji simu husababisha betri kuharibika/kufa mapema kuliko simu ambayo imewekwa kwenye halijoto la chini.

Tuangalie mazingira ambayo tunachajia simu zetu, kusiwe na joto kali sana.

5. USITUMIE SIMU WAKATI WA KUCHAJI.

Hili ni kosa kubwa ambalo wengi tunalifanya bila kujua, simu haiwezi kufanya kazi mara mbili kwa usahihi,simu iingeze chaji na kutumia chaji kwa wakati mmoja. hii inaua cells kwenye betri maana betri hutumia nguvu isivyo kawaida

Kingine inaharibu mzunguko wa kuchaji simu (charging cycles), kama simu ilitakiwa ijae ndani ya dakika 30 basi itatumia dakika 50 au zaidi na hii hufanya betri kupata joto na hupelekea kuharibu kabisa betri ya simu.

USHAURI

Epuka simu yako kuishiwa chaji kabisa yaani 0% ya betri, na kulaza simu yako kwenye chaji mara kwa mara.

Joto husababisha kuharibu betri, jitahidi kuweka simu sehemu isiyo na joto kali, pia usifunike simu wakati wa kuchaji.

Usitumie simu wakati wa kuchaji, hasa hasa usitumie kwa kazi nzito kama kucheza games, kuangalia video mtandaoni (streaming).

Tumia Battery Saving Features kama kupunguza screen brightness, kuzuia Apps background etc, pia update simu yako mara kwa mara

MASWALI YANAYOULIZWA SANA.

1: Je, ni Kweli Kwamba Hupaswi Kuchaji Simu yako hadi 100%?

Hiki ni kitu ambacho wengi tunafanya, tunapenda simu zijae mpaka 100%, kulingana na bwana Asidor Buchmann , CEO wa Cadex Electronics na mwanzilishi wa Battery university alisema...

Siyo vizuri kuchaji simu mpaka 100%, Betri za Lithium zinazopatikana kwenye smartphones hazipendi kuchajiwa mpaka 100% hasa wakati wa joto husababisha betri pia kupata joto na simu kupata joto, hii inaua ufanisi wa Betri.

2: Je, naweza kuiweka simu chaji usiku kucha?

Kitu kingine ambacho tunafanya ni kuweka simu chaji wakati tunaenda kulala usiku na kuitoa asubuhi hii haishauriwi,inashauriwa kuchaji simu kuanzia 20% - 80%

Ukilaza simu kwenye chaji inachaji mpaka 100% inastop...

Simu ikipungua mpaka 99% inajichaji tena mpaka 100% kufanya hivyo mara kwa mara si vizuri kwa afya ya betri.

3. Je, Ni Salama Kuchaji Simu mara nyingi kwa siku?

Ndiyo, simu nyingi zina Lithium-ion batteries ambazo hupenda kuchajiwa kwa internal fupi fupi.

4. Je, "Fast chargers" Huharibu Betri?

Hapana, kama ukinunua simu yenye uwezo wa Fast charging, basi inauwezo wa kupokea chaji haraka kwa kutumia Faster charger, Na haiwezi kuharibika. Lakini tu kwa simu zenye uwezo huo, si kila simu inauwezo kwa Fast charging.

5. Vipi kuhusu Wireless Charging?

Simu nyingi za kisasa zinakuja na Wireless charging, Wireless charging haiharibu betri ya simu yako japo inatengeneza joto kwa kiasi kuliko chaja za kawaida, ukiona joto limezidi basi betri au simu ina matatizo.
 
Imejini simu itajaa kwa masaa 3, unaweza kuacha kuwasiloana kwa muda wa masaa 3?
Labda uwe na simu zaidi ya moja
 
Back
Top Bottom