Wataalamu wa kukopa bila kurefund

Wataalamu wa kukopa bila kurefund

waleoleo

Member
Joined
Jun 18, 2012
Posts
53
Reaction score
17
Inakera pale mtu anapokuja na shida anakuomba hela with a promice ntakupa after three days afu anauchuna hasemi kitu after those days anakua anakupiga fix tu. Mbaya zaidi anakuzungusha mpaka unakata tamaa. kulipa deni kunakupunguzia aibu tukikopa tulipe
 
Dawa yake akikukopa tena wewe mgaie bureeeee!
 
Sina ndo maana nimekopa......sasa hela yakulipa ntapata wapi?!!!!!
 
Kama kakupa cku 3 atakua amerejesha ikifika siku ya 3, anza kuhesabu tena mpaka atakapokuja kulipa ndo ujue ndo cku ya 3
 
Kama kakupa cku 3 atakua amerejesha ikifika siku ya 3, anza kuhesabu tena mpaka atakapokuja kulipa ndo ujue ndo cku ya 3, na asipokuja ujue haijafika bado
 
buku kumi tu umeamua kunifungulia UZI!!!Chilax mkuu ....narekebisha INSHU nitakutumia fasta
 
Inakera pale mtu anapokuja na shida anakuomba hela with a promice ntakupa after three days afu anauchuna hasemi kitu after those days anakua anakupiga fix tu. Mbaya zaidi anakuzungusha mpaka unakata tamaa. kulipa deni kunakupunguzia aibu tukikopa tulipe

pole sana.
 
mbaya zaidi jamaa anakumbia njoo saa kumi uchukue ukfika unaambiwa katoka mapema sana leo job!!
 
kuna watu 5 nawadai pesa ndogo tu lakin kulipa matanga na mwisho wa mwezi ulishapita,lakin awalipi wengine wameuchuna,mwingine aliniambia aamesafiri nikaja kumkuta kwenye mkutano wa harusi,wengine awapokei simu,dawa ni kukomaa nao na sikopeshi tena wanaume
 
Mi ishu ya kikopesha nshaachana nayo zamani. Kama nna hela bora mtu nimgaie. Waongo wengi nowadays. Humjui mwenye shida ya kweli au ya uongo
 
Au kukopa sukari lakini kulipa shubiri.....

Halafu sasa ukizidai hela zako unaweza kuonekana mbaya....

Lol, umenikumbusha mbali, kuna mtu namdai mwaka wa tatu huu, na kila siku anazushia jambo! Kwa sasa nimekataa tamaa nimeamua kumuacha na kusamehe deni! Binadamu wengine sijui tumeumbwaje umbwaje?!
 
Hahah kwa wabongo kukopa na kudaiwa ni kama kaugonjwa ka taifa...
Hata kama hamtaki kila Mbongo anadaiwa kitu ka 400k kutoka lile deni la nje la taifa...
 
Back
Top Bottom