Waswahili wanaousifia uwanja wa Amani Zanzibar kwa jina la Guantanamo bay ni maamuma wa historia na haziwatoshi

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
57,243
Reaction score
90,301
Guantanamo bay ambacho ni kituo cha jeshi la Marekani katika ardhi ya Cuba pwani kilijipatia umaarafu sana baada ya vita vya ugaidi kuanzia mwaka 2001.

Hapo Guantanamo bay ndipo walipokuwa wanashikiliwa kama mahabusu watu waliokamatwa na vyombo vya US kutoka nchi nyingine wakituhumiwa kama magaidi hatari zaidi. Hao watu ambao wengine walikuwa magaidi kweli na wengine walikamatwa kwa bahati mbaya au kimakosa tu waliteswa mateso ya kila aina yaliyopelekea hadi vifo wakati mwingine.

Guantanamo bay ilitumika kama kituo cha kuwashikilia kwa sababu wengi wao walikuwa hawawezi kushitakiwa katika mahakama za Marekani. Unapoona Mswahili anachukulia Guantanamo bay kama jina la sifa unajua tu hazimtoshi, ni akili ndogo.
 
Tulosoma shule za boarding mabweni mengi tu yalipewa majina ya Guantanamo
 
Ule uwanja bado ila basi tu capacity yake ni ndogo hauna hata hadhi dijui kwanini wanapeleka mashindano huko, zanzibar wajenge uwanja mkubwa km mkapa stadium
 
Mkuu, naamini umeona idada ya mashabiki wanaoingia kwa Mkapa. Bora zanzibar kwenye mechi za yanga wanaingia wengi
 
Guantanamo bay ambacho ni kituo cha jeshi la Marekani katika ardhi ya Cuba pwani kilijipatia umaarafu sana baada ya vita vya ugaidi kuanzia mwaka 2001.

Hapo Guantanamo bay ndipo walipokuwa wanashikiliwa kama mahabusu watu waliokamatwa na vyombo vya US kutoka nchi nyingine wakituhumiwa kama magaidi hatari zaidi. Hao watu ambao wengine walikuwa magaidi kweli na wengine walikamatwa kwa bahati mbaya au kimakosa tu waliteswa mateso ya kila aina yaliyopelekea hadi vifo wakati mwingine.

Guantanamo bay ilitumika kama kituo cha kuwashikilia kwa sababu wengi wao walikuwa hawawezi kushitakiwa katika mahakama za Marekani. Unapoona Mswahili anachukulia Guantanamo bay kama jina la sifa unajua tu hazimtoshi, ni akili ndogo.
Wewe inakuuma nini !

Watu wanajua historia kuliko hata wewe.
 
Guantanamo, sobibor , gaza , darfur ,

wanasema shida isikie kwa wengine tu
 
Back
Top Bottom