KAULI YA LEO
Neno 'SWAHILI' kimatamshi linaweza kutokana na 'ZIWA HILI' au likatafsiriwa 'SAWAHILI' kutokana na neno la Kiarabu 'SAHIL' linalomaanisha 'PWANI' likirejelea 'lugha', 'tamaduni' na 'watu' wanaoishi 'kando kando ya bahari' au 'Pwani'.
'Wamijikenda' na 'wandigo' waliwaita 'Wajomba' (Wadzomba) au 'watoto wa shangazi' waliokuwa wakizungumza 'Kidzomba' au 'Kijomba' na waliotangamana na Waarabu wakajua kuandika; na ndipo walijiandika 'Waswahili' au 'Wapwani' badala ya 'Wajomba' na lugha yao ya 'Kidzomba' au 'Kijomba' wakaiandika kuwa 'Kiswahili'!
(©) Dkt John Karithi