Wasukuma na utamaduni wa kutakasa mapacha

Wanyantuzu sio Wasukuma, ni waamiaji tu na walicopy lugha ya Kisukuma ambayo wanaiongea kwa lafudhi tofauti na kisukuma asilia, pamoja na kukopi lugha pia walikopi baadhi ya mila na zingine waliziacha

Weka vyanzo...
 
We kweli kituko! Kama uko Dar nenda pale UDSM Library waambie wakupe dissertation ya Buluda Itandala. Inaelezea vizuri sana mchanganuo wa Wasukuma (wakiwemo Wanyantuzu), asili yao n.k. Tafuta pia maandiko ya Batibo kuhusu uhusiano wa lahaja ya Kinyantuzu na lugha jirani. Jisomee kwanza kabla ya kupanda jukwaani vinginevyo utaendelea kuonekana kituko.
 
Aisee, asante kwa kunifahamisha kuwa Wanyantuzu kuwa nao ni Wasukuma
 
Kwetu Ng'wabuki kata ya Bumera
 
Sijawahi kusikia Wanyambiti, wanyankanga, wanyageita, bali wote huwà wanaitwa Wasukuma tu, nashindwa kuelewa ikawaje hawa wa Ntuzu kuitwa Wanyantuzu?
 
Nenda makumbusho ya Bujora, utafahamu hata mengine ambayo huyajui! Siyo kuandika vitu vya kusadikika ambavyo huna ushahidi navyo.

Ntaenda kaka hapo Bujora, lakini hakuna Msukuma wa maeneo mengine anaekubali kuwa mnyantuzu kuwa ni Msukuma, bali huwa wanawaita Wanyantuzu tu kwa nini?
 
USA baby...
Huwezi kufiti kila sehemu kihivyo, utachekesha!
 
Ntuzu ni tabaka kama ilivyo kwa Nkamba na Nseya. Lakini Ntuzu ndiyo tabaka iliyokuwa imara katika kutunza tamaduni za kisukuma hadi leo. Nenda Bujora utajifunza mengi..
Daaaah mkuu umenikumbusha home kabsa,mimi ni mseya pale ikulu ya chief makwaya kidaha pale Ukenyenge negezi.sisi maeneo yetu ukizaa mapacha unachezwa ngoma inayoitwa bhukango,aiseee yaani nyama kwa wingi.
 
Naona BBC wanashida na watu wa huko maana walianza na mauji ya vikongwe, wakaja ndoa za utotoni na sasa hivi wamekuja na hii ya watoto mapacha!
haujuwi kuna reporter wao yuko huko anakusanya habari kwani wangejuaje yote hayo
 
Wanyantuzu sio Wasukuma, ni waamiaji tu na walicopy lugha ya Kisukuma ambayo wanaiongea kwa lafudhi tofauti na kisukuma asilia, pamoja na kukopi lugha pia walikopi baadhi ya mila na zingine waliziacha
waliami akutoka wapi mkuu maana naona unawafahamu sana
 
sio kija ni shija
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…