nafahamu wengi hamtapenda lakini ndivyo dunia ilivyo ukimwaga ugali watu wanamwaga mboga lakini katika viongozi wa sasa wa vyama vyote vikuu hakuna aliyekuwa msafi tofauti ni kwamba kundi fulani liko jikoni la kundi lingine liko sebuleni waliko jikoni wananafasi kubwa ya kula msosi wanavyotaka lakini ikitokea nafasi ya kundi lililoko sebuleni kuingia jikoni tatizo litakuwa lile lile kwani nao si wasafi ebu soma hii stori ya katibu mkuu wa magwanda akiwa na umri wa miaka sitini na tisa akini bado ana mchumba:....
Kashfa ya katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema),Dk Willibrod Slaa imewekwa hadharani kwamba kiongozi huyo alifukuzwa upadri baada ya kutafuna mamilioni ya fedha zilizochangwa kwa ajili ya ujio wa hapa nchini wa Kiongozi wa Kanisa katoliki nchi duniani papa katika miaka ya tisini
Tuhuma hizo zimemwagwa na Waziri Steven Wassira katika mikutano ya kampeni za ccm kumnadi mgombea wa chama hicho sioi Solomon sumari katika Jimbo la Arumeru mashariuki
tuhuma hizo zinakuja wakati vyama hivyo viwili vikubwa nchini vikirusiana vijembe na makombora mazito mazito
kashfa hiyo imetolewa katika vijiji vya kata Kikwe katika Jimbo hilo la Arumeru Mshariki Mkoani Arusha.
Wassira alisema kwamba Dk Slaa ambaye pia aliwahi kuwa katibu mkuu wa baraza la maaskofu nchini(TEC) kabla ya kukumbwa na kashfa hizo za kutafuna mamilioni hayo ya fedha zilizochangwa na waumini wa katoliki kutoka vigango na parokia mbalimbali nchini ili kufaniisha ujio wa Papa miaka ya tisini kitendo kilichopelekea kufukuzwa kazi ya upadri.
amesisitizas kwamba kiongozi huyo hana kifua cha kupambana na ufisadi kwa kuwa hata yeye alitafuna fedha za kanisa.
Aliwataka wakazi wa kata ya Kikwe kumuuliza Dk Slaa chanzo cha kufukuzwa upadri pindi atakapotia mguu ndani ya kata yao na kuwataka wakazi hao kutosikiliza sera za kiongozi huyo kwa kuwa si msafi wa kujipambanua kwamba anapambana na ufisadi nchini.
Alimtuhumu Dk Slaa Pia katika hatua nyingine anatuhumiwa kumfukuza kazi mhasibu wa chama hicho ngazi ya taifa kwa kosa la kukataa kutekeleza maagizo yake amlipe shilingi milioni 10 mchumba wake,Josephine Mushumbushi kitendo kinachotia mashaka ya uadilifu wa kiongozi huyo.
Hata hivyo,alishangaa kitendo cha Dk Slaa kuishi maisha ya uchumba wakati akiwa na umri wa miaka zaidi ya 60 na kudai kitendo hicho kinashangaza umma wa watanzania pamoja na wafuasi wa vyama vya siasa nchini.
Wakati huo huo,Wassira ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM alisema kwamba mgombea ubunge wa Chadema,Joshua Nassari hafai kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kuwa ni kijana mkorofi na mara kwa mara baba yake mzazi amekuwa akimsihi kuachana na ukorofi tangu wakati akiwa chuo kikuu cha Dar es salaam.
Alisema kwamba baba wa mgombea huyo ambaye ni kiongozi wa dini amekuwa akimsihi kuachana na ukorofi ikiwa ni pamoja na kuoa ili aweze kutulia lakini cha ajabu Nassari amekuwa akionekana na bibi wa kizungu mwenye umri wa zaidi ya miaka 60 akizunguka naye mitaani.
Wassira amewataka wananchi wote waliojiandikisha kuhakikisha wanatunza shada zao ili kuepuka kuporwa na wafuasi wa chadema
Amesema tayari chama cha chadema kimeanza mchezo mchafu kwa kusambaza waraka pamoja na vijana kwa ajili ya kununua shahada
Natoa changamoto:
1. Ukiwa unaanza kujenga hoja kwa uwoga huu, basi ni hoja ambayo inalenga kuvutia upande mmoja wa hoja au kuonyesha kuwa wewe mtoaji wa hoja unalenga wasomaji/wasikilizaji wakuelewe hivyo ambavyo wewe unataka iwe hivyo.....tazama ulivyoanza"
nafahamu wengi hamtapenda lakini ndivyo dunia ilivyo ukimwaga ugali watu wanamwaga mboga"Kwanini unadhani mwanzo huu ni mzuri kuujengea hoja..nahisi ni siasa!!
2. Tatizo langu ni busara ya Mzee WASSIRA, siku sio nyingi zilizopita alisikika akisema kuwa Mh. JOSEPHAT KIBOKO NYERERE hana busara kwa kusema maneno au lugha chafu dhidi ya MKAPA..sasa haya maneno yake yasiyo hata na ushahidi wa kuthibitisha hayo anayosema yanatoka wapi.....???
Anasema hivi "
a.
Kashfa ya katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema),Dk Willibrod Slaa imewekwa hadharani kwamba kiongozi huyo alifukuzwa upadri baada ya kutafuna mamilioni ya fedha zilizochangwa kwa ajili ya ujio wa hapa nchini wa Kiongozi wa Kanisa katoliki nchi duniani papa katika miaka ya tisini" Atuambie taarifa hii imewekwa hadharani wapi, na akina nani wameweka...otherwise huo ni uwongo and he's trying to buy political votes kutoka kwa wasioweza kujua ukweli au undani wa mambo haya.
b.
kabla ya kukumbwa na kashfa hizo za kutafuna mamilioni hayo ya fedha zilizochangwa na waumini wa katoliki kutoka vigango na parokia mbalimbali nchini ili kufaniisha ujio wa Papa miaka ya tisini kitendo kilichopelekea kufukuzwa kazi ya upadri. Kwa namna ninavyojua SIASA za Tanzania jambo hili kama lingekuwa limefanyika sina hakika mpaka leo hii habari hii ingekuwa ni bora kutumika leo mwaka 2012 na SIO mwaka 2010 wakati wa UCHAGUZI..maana siasa inakuwa na timing zake ili adui yako apate kukuua politically ni lazima atafute muda muafaka wa kufanya political assassination and NOT anything else.
c. HII hoja nayo haiuziki/ kununulika save for those who dont trouble themslves. Ninaamini ktka kila ofisi kuna utaratibu wa kufanya malipo na retirements. Sasa ili sisi wasomaji tuweze kuamini ni bora wanaotoa hoja hizi waje na data kamilifu, mfano: Mhasibu aliyefukuzwa ni fulani (kwa jina), habari imethibitishwa na... (jina, cheo ktk ofisi iliyotuhumiwa,), tarehe ya tukio, kwa sasa mhasibu ni fulani (labda)...., na madai ya aliyefukuzwa yalikuwa ni......VINGINEVYO HUO NI UWONGO NA UPUUZI...AND IT RATHER INTENDS TO EMBRACE POLITICAL IGNORANCE
"
Alimtuhumu Dk Slaa Pia katika hatua nyingine anatuhumiwa kumfukuza kazi mhasibu wa chama hicho ngazi ya taifa kwa kosa la kukataa kutekeleza maagizo yake amlipe shilingi milioni 10 mchumba wake,Josephine Mushumbushi kitendo kinachotia mashaka ya uadilifu wa kiongozi huyo.
d. Hata hivyo,alishangaa kitendo cha Dk Slaa kuishi maisha ya uchumba wakati akiwa na umri wa miaka zaidi ya 60 na kudai kitendo hicho kinashangaza umma wa watanzania pamoja na wafuasi wa vyama vya siasa nchini. PERSonal attacks??? MZEE hana ufahamu, i cant buy hizi propaganda.
e. Joshua Nassari hafai kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kuwa ni kijana mkorofi na mara kwa mara baba yake mzazi amekuwa akimsihi kuachana na ukorofi tangu wakati akiwa chuo kikuu cha Dar es salaam. YAANI wassira....KWANINI UNASEMA MAMBO HAYA YA UWONGO lakini unajua unaowafanyia hivyo hawawezi kukuhoji, pia yaani BABA NASSARI akueleze wewe ukorofi wa mtoto wake wakati huu wa uchaguzi na sio vinginevyo??
HAYA KILA HERI KWA WANA ARUMERU MASHARIKI, ila uwongo, ujuha, rushwa na uovu mwingine hautavijenga TANZANIA na siasa ni sehemu muhimu katika MAISHA yetu tukikosea katika kuchagua viongozi BORA tutaendelea kujadili ever bila CHANGES.