Wasomi wazidi kuikosoa Serikali

Huyo msomi ni mnafiki kaongea mambo yaleyale bila kuleta solution!!

Solution ni kila mtu afuate sheria.Hakuna aliyejuu ya SHERIA.Na rais ameapa kuilinda SHERIA NA KATIBA ya NCHI basi avilinde na kuvitetea pia
 
We ulienda shule ipi!!!
Msomi akiongea unachofeel kusikia unakenua meno !!!
Msomi huyo huyo akiongea usichotaka kusikia unamshambulia??
Kuwa na tabia ya kueshimu maoni ya mtu yeyote maana hapa ni jukwaaa huru

Nimekupa mpaka mifano ya wasomi waliotolewa njee ya nchi wakaja wakawa Vila.za baada ya kutumikia watu wanaitumikia ccm
Wengine walitoka Un wakaja kuwa mafisadi !!
Wasomi wetu ni sizitaki mbichi hizi ila akionjeshwa mnofu wa ccm anasahau usomi wake wote anaanza kuitumikia ccm

Uwaoni wakikosoa wakiwa ndani ya mfumo!!!
Professor ninayemweshimu hapa Tanzania ni mmoja tu yule wa mbeya!!

I believe we are on the same page but deferent approaches. Malipo yasiyostahili kwa wanataaluma / wasomi ni chanzo kikubwa cha wengi kukimbilia siasa inayotoa malipo mapana ambayo wakati mwingine hayana mashiko katika ustawi wa jamii inayokusudiwa kujengwa.
 
I believe we are on the same page but deferent approaches. Malipo yasiyostahili kwa wanataaluma / wasomi ni chanzo kikubwa cha wengi kukimbilia siasa inayotoa malipo mapana ambayo wakati mwingine hayana mashiko katika ustawi wa jamii inayokusudiwa kujengwa.
Hapo sawa!!!
 
Naomba uelewe bosi Rais haitumii katiba kuwa dicteta ila imempa madaraka makubwa kiasi ambacho maamuzi anayoyafanya unaweza kusema ni dicteta.Wewe unatakiwa ulie na kupigania mabadiliko ya katiba na si kusema Rais dicteta haitasaidia kitu
 
Nitachangia hilo unalosema Tanzania hakuna wasomi. Hilo siyo kweli. Wasomi wapo tena wengi. Ni kwq bahati mbaya siasa ina nguvu kuliko Usomi. Hawahawa unaowaona hawajasoma ni lulu huko Botswana, Zambia na kwingineko duniani. Wahandisi, Madaktari nk ambao ni Watanzania wanaheshimika sana huko duniani. Wanadeliver. Hapa nyumbani ipo shida kubwa sana. Mifano yangu ya Prof Tibaijuka, Mzee Omar Nundu walifanya makubwa huko nje. Lakini sote tunajua kilichowakumbuka Tido Mhando, Prof Tibaijuka, Omar Nundu. Kama Taifa ipo shida mahali. Wasomi tena wabobezi wapo na walijijengea heshima kubwa nje ya nchi.
Kwa kadri ya nilivyoelewa, mada hii imechukuliwa kutoka katika andiko au makala ya Professor Mtanzania aliye US, na hadi uaminiwe huko ujue yuko vizuri, je naye siyo msomi?
Hivyo siyo sahihi kusema Tanzania hakuna wasomi, huo ni uongo. Labda useme Pure Scientists kwa level za Newton, Pascal, nk lakini usomi watu wapo na kama professionalism ingekua ni silaha kamili na maslahi yakawa bora,Wasomi wenye weledi ambao ni Watanzania wapo wengi tu.
Huwezi kusema kuna wasomi wakati utafiti unasema 61%ya waitimu wa elimu ya juu wana uwezo mdogo wa maarifa na ufahamu
 
Mimi kama msomi wa Sheria ninakushauri wewe pia na wa TZ wote kwa ujumla sambamba na kudai kuwa Rais wetu ni dicteta hauna budi kabla hujajidhatiti na kauli hiyo uisome vizuri katiba hususani isome na uielewe ibara ya 36 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977,hakika katiba hii kupitia ibara hiyo inampa Rais madaraka makubwa sana ya kufanya chochote kile na ukizingatia kuwa katiba ndio sheria mama na mamlaka yake ni ya juu(siperior authority over any other law applied in Tanzania).Hivyo tatizo si Rais kwani yeye anatumia madaraka ya kikatiba hivyo tatizo kubwa ambalo linatutesa na litaendelea kututesa mda mrefu ni mamlaka ya kikatiba.Hivyo katiba inahitajia mabadiliko ili kupunguza madaraka hayo huku uwe na kumbukumbu kuwa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa alishangaa sana kuona katiba ilivyo mpa madaraka makubwa yeye kama Rais kiasi ambacho alisema angeweza kuwa Dicteta.
Unaposoma hiyo ibara ya 36 pia soma ibara ya 46A ibara ndogo ya 1na 2 na ya3.
Utaona kuwa rais hayuko juu ya sheria, na kuna hatua ambazo bunge linaweza kumchukulia kama atavunja katiba ya nchi au kwenda kinyume na maadili. Ni kweli ibara ya36 inampa madaraka makubwa lakini sio ya kuvunja katiba.

Sijaona mahali katiba pamoja na kasoro zake inaweza kumpa raisi uwezo wa kuwa dikteta. Labda tunatumia hili neno dikteta vibaya ndio maana Lisu hataki kusema dikteta akaishia hapo, anasema 'dikteta uchwara'.
 
Kuna watu wanataka unapoandika maelezo lazma uandike neno solution wapate kuona kuna suluhisho la mada husika limetolewa.Solution- read between the lines.
 
Nimekupata DANNY JULLY lakini hoja zangu hazijasema kuwa rais yupo juu ya sheria ila amepewa madaraka makubwa kiasi ambacho anauwezo wa kufanya maamuzi yoyote kwa mwamvuli wa katiba kuhusu jambo lolote na mtu wa kawaida(ordinary person)anaweza kusema kuwa anafanya maamuzi ya kidikteta.

Pili,ibara ulioitaja inahusu kumtoa madarakani Rais(impeachment of president) kabla ya kumshtaki.Hivyo hoja yako hiyo haiendani na kiin cha hoja yangu ya madaraka makubwa ya Rais,pia kumbuka hiyo ibara ya 46A inatumika pale tu ambapo unatak kumshtaki Rais kwa kosa la jinai au la kiraia,hivyo mimi kusema Rais anamadaraka makubwa kupitia ibara ya 36 sijamaanisha kuwa huwezi kumshtaki Rais kupitia ibara ya 46A.
 
Kwanza mm nakataa Tanzania hakuna wasomi bali kuna watu waliospend muda wao madarasani na kutunukiwa vyeti kwani changamoto zinazotukabili toka enzi ya uhuru nchi ilipokuwa na ma doctor wazawa 5 na injinia 1 ni zile zile mpka leo interview zinafanyika uwanja wa taifa kwa jinsi degree, masters na phd zilivyo nying nchi hii lakini changamoto ni zile zile za toka enzi za uhuru

Pia tunakiwa kujua maana halisi ya dictator kwa vigezo vya udictator magufuli hana ila kinachomfanaya aonekane dictator ni kutaka watanzania waishi kwa kufata mfumo wa sheria hcho tu. Katiba aijakubali maandamano tu ndo maana kukawa na taasisi zinazotoa vibali vya kufanya maandamano kazi hyo walipewa jeshi la police kwani wao ndo wanahusika na ulinzi wa raia na mali zao sasa kama police wameona viashilia vya uvunjifu wa amani katiba inawaruhusu kupiga marufuku maandamano ayo. Leo huwezi kusema maandamano yatakuwa ya amani wakati unatumia maneno ya lazima,hatukubali,aiwezekani,unaanzisha operation zenye majina ya ajabu sehemu yeyote unaposikia kuna operation hujue hapo amani hakuna aiitaji phd kujua ilo hata hospital operation ndio tiba ya mwisho kwa mgonjwa je leo chadema wameshindwa kutumia njia yeyote mpaka watangaze operation ????

Chama kinachojinasibu kuwa na hazina kubwa ya wasomi leo wameshindwa kutumia njia nyingine zaidi ya kutangaza maandamano dunia nzima hata marekani maandamano huwa yanadhibitiwa na police kwani impact ya maandamano ni kusababisha ulemavu ,usumbufu kwa watu huwezi kufungua biashara wakati maandamano yakiwapo shuguli nyingi za kiuchumi lazima zisimame pia chadema inatakiwa kujua ICC wanakwenda c watawala peke yao mpaka wapinzani wanakwenda pia. mfano kenya kenyatta na ruto walikuwa watawala?? kwa nn asiende kibaki???? ICC wanaangalia source ya vurugu zimesababishwa na nani

Zipo njia nyingi za kufanya harakati zao coz mm naamini hawafanyi siasa bali wanafanya harakati tu kama wameshindwa bungeni sehemu pekee wanayoweza kuishinda serikali na ikakubali ni mahakamani pale ndipo wanaweza kupata haki zao zote tena hao waliokataa wasifanye siasa ndio watakuwa wanawalinda katk mikutano yao si wanawanasheria wazuri basi wakapambane mahakamani kama wanaona katiba imevunjwa coz sheria zinatungwa bungeni zinatafasiliwa mahakamani kuliko kuwaletea vijana wa maskini ulemavu kwa kupigwa mabomu na maji ya kuwasha
Una interests fulani chama tawala hongera kwa kuwa mtumwa wa fikra za chama.Changamoto za nchi hii ni zilezile sababu ya watu kama wewe wasioweza kutoka kwenye comfort zone zao kwa kuogopa kukinzana na watawala wasijepoteza walicho nacho ingawa ukweli halisi wanaujua.
 
Na Profesa Joseph Mbele

Nimeona nianzishe mjadala wa suala linalovuma wakati huu nchini Tanzania, ambalo ni: Je, Rais Magufuli ni dikteta uchwara?

Tundu Lissu, mwanasheria wa CHADEMA ndiye mwanzilishi wa dhana hii ya kwamba Rais Magufuli ni dikteta uchwara. Kwa kuanzia, ninapenda kuwashutumu polisi na watawala wa CCM kwa namna walivyolishughulikia suala hili.

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, Tundu Lissu ana haki na uhuru wa kuwa na mawazo yake kuhusu suala lolote. Ana haki na uhuru wa kuwa na mtazamo wake juu ya Rais Magufuli. Ana haki na uhuru wa kutoa mawazo yake kama alivyofanya.

Mtu mwingine yeyote naye ana haki na uhuru huo. Kwa hivi, kauli ya Tundu Lissu haikuhitaji hatua zilizochukuliwa na polisi za kwenda kumkamata na kumsafirisha kutoka Singida hadi Dar es Salaam kwa mahojiano makao makuu ya polisi.

Jambo ambalo lingeweza kufanyika, bila taabu yote hii na ufujaji wa hela za walipa kodi, ilikuwa ni kwa serikali kujibu hoja za Tundu Lissu na kuthibitisha kuwa Rais Magufuli si dikteta uchwara. Malumbano ya hoja yangetosha.

Ndio utaratibu unaotakiwa katika jamii iliyostaarabika. Ninaamini kuwa wa-Tanzania wana akili timamu, na wana uwezo wa kuchambua mambo. Wana uwezo wa kusikiliza hoja za pande mbali mbali na kutambua upande upi ni sahihi.

Madai ya polisi na watawala wa Tanzania kwamba kauli ya Tundu Lissu ni uchochezi ni ya kuwadhalilisha wananchi. Ni kusema kwamba wananchi ni wajinga, wasio na uwezo wa kutathmini na kuchambua mambo.

Ni kwanini serikali haikuchukua njia hii ya kujibu hoja kwa hoja? Inamaanisha kwamba katika serikali nzima hakuna mtu mwenye akili ya kuweza kumpinga Tundu Lissu na kuthibitisha kuwa Rais Magufuli si dikteta uchwara?

Inamaanisha kuwa watendaji wote wa serikali hii ya CCM ni watendaji uchwara, au ni watendaji hewa, au ni ******?

Rais Magufuli, kwa mtazamo wangu, amekuwa akivuka mipaka ya katiba kwa baadhi ya kauli zake. Hana mamlaka kikatiba wala kwa mujibu wa sheria za vyama vya siasa, kuweka vizuizi juu ya mikutano na maandamano ya vyama vya siasa. Taratibu zote zimeelezwa katika katiba ya Tanzania na katika sheria ya vyama vya siasa.

Kwa bahati nzuri, katiba ninayo na nimeisoma, na sheria ya vyama vya siasa, ambayo imewekwa kwenye tovuti ya ofisi ya msajili wa vyama, nimeisoma pia: http://www.orpp.go.tz/en/rules/. Kwa kupitia katiba na sheria, ni wazi kuwa Rais Magufuli anakiuka katiba na sheria, na kwa hivyo, kauli ya Tundu Lissu kwamba Rais Magufuli ni dikteta uchwara ni sahihi.

Vyama vya siasa vinawajibika kufanya mikutano na maandamo kwa amani, ili kutangaza sera zao, kutafuta wanachama wapya, na kadhalika. Rais Magufuli, au mtu mwingine yeyote hana wadhifa wa kuwawekea zuio kama alivyofanya. Hana mamlaka ya kusema kwamba watu wafanye siasa katika maeneo yao tu.

Hana mamlaka ya kutangaza, hata kwa kisingizio cha "hapa kazi tu," shughuli zipi za kisiasa zisitishwe hadi mwaka 2020. Huu ni udikteta.

Mimi ni raia ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Ninachotaka ni kuona nchi inaendeshwa kwa mujibu wa katiba na sheria zilizopo. Ninataka utawala wa sheria, unaozingatia haki za binadamu.

Dikteta wa ukweli ni Umma-" Dictatorship of the mass" ukiteta wa mtu mmoja mmoja ni uchwara tu
 
Nimekupata DANNY JULLY lakini hoja zangu hazijasema kuwa rais yupo juu ya sheria ila amepewa madaraka makubwa kiasi ambacho anauwezo wa kufanya maamuzi yoyote kwa mwamvuli wa katiba kuhusu jambo lolote na mtu wa kawaida(ordinary person)anaweza kusema kuwa anafanya maamuzi ya kidikteta.

Pili,ibara ulioitaja inahusu kumtoa madarakani Rais(impeachment of president) kabla ya kumshtaki.Hivyo hoja yako hiyo haiendani na kiin cha hoja yangu ya madaraka makubwa ya Rais,pia kumbuka hiyo ibara ya 46A inatumika pale tu ambapo unatak kumshtaki Rais kwa kosa la jinai au la kiraia,hivyo mimi kusema Rais anamadaraka makubwa kupitia ibara ya 36 sijamaanisha kuwa huwezi kumshtaki Rais kupitia ibara ya 46A.
Sawa nimekuelewa mkuu.
 
Ndugu zangu mnaosema Rais ni dikteta na ambao mnasema Rais siyo dikteta je mnajua sifa na tabia ya mtu ambaye ni dikteta? Na je sifa na tabia hizo rais anayo? Majibu ya maswali haya yatahalalisha au kubatilisha udikteta wa rais kazi kwenu wasomi wa nchi hii
 
Unaweza kukuta hao polisi wanajishauri wenyewe na wala hawatumwi na mtu kwenda kumkamata TL: najiongeza tu kuw hao RPC na Mkuu wao wanajipa kazi ya kushinda mitandao kusikiliza JPM amesemwaje leo na wana act ingali yeye hana wazo wala hajawatuma! Polisi waache kujipendekeza! Wafanye kazi yao!! Kulind amani sio kulinda ukawa wasifanye maandamano!! Waache kujikomba!!!
 
Sikia kwanza Mimi nikwambie sijawai mchagua Magufuli !!

Lakini wasomi wetu wamekuwa wanafiki hasa wakiwa uje ya mfumo lakini wakiitwa waingie ndani ya serikali wanakuwa Mbogo Uo sio unafiki??

Wasomi wangapi walikuwa nje walipoludi wakawa mafisadi??

Wangapi waliludi wakaikumbatia ccm na mfumo wake wa kifisadi??

Fatilia posti zangu unajua kwamba Mimi ni MTU huru asiyeyumbishwa na upande wowote wa siasa za Tanzania kazi yangu ni kuusema ukweli japo unauma!!!
haa haa hapo kwenye wasomi nimemkumbuka Dr RYOBA wa TBC....
 
Mnaosema kavunja katiba nendeni mkafungue kesi ya kikatiba. Yaani lichama likubwa kama CHADEMA mnashindwa na mtu mmoja kama Mtikila ambaye alikuwa haleti siasa uchwara. Yeye alikuwa anaenda kufungua kesi za kikatiba ili kuprove point yake.

Mengine alishasema Mkapa kuhusu Upumbavu na Ulofa. Naona ndo kinachoendelea hapa.
Mfano ni kama huyo juu aliyesema "Majaji wanateuliwa na Mwenyekiti wa CCM."

Huyo ni mtu anayeandika kwa hisia badala ya tafakuri. Ni mtu ambaye hajui ni kesi ngapi CHADEMA imeshinda kwenye mahakama hizo hizo ambazo zinateuliwa na "Mwenyekiti wa CCM."

Na pia ni mtu ambaye hajui kuwa "Mwenyekiti wa CCM" wa sasa hivi ndiye Rais wa Tanzania pia.
Kesi za Mtikila mpaka leo hazijatekelezwa na zingine serikali ilizikatia rufaa licha ya marehemu kuwabwaga mara kadha. Ukweli ni kuwa watawala wa ki Africa walikubali mfumo wa vyama vingi shingo upande. Wewe Tz tangu tuingiie mfumo wa vyama vingi lakini tumeshindwa kutunga sheria zinazoendana na vyama vingi vya siasa. Badala yake zinatumika sheria za mfumo wa chama kimoja tena chama dola.

Maghufuli ni Rais mzuri ila anaonekana mwenye hasira na kutokupenda kukosolewa, nchi haiendeshwi hivyo.

Nashauri ategemee sana upendo wa wananchi wake asitegemee sana vyombo vya dola vitamharibia zaidi
 
Back
Top Bottom