Wasomi wazidi kuikosoa Serikali

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Na Profesa Joseph Mbele

Nimeona nianzishe mjadala wa suala linalovuma wakati huu nchini Tanzania, ambalo ni: Je, Rais Magufuli ni dikteta uchwara?

Tundu Lissu, mwanasheria wa CHADEMA ndiye mwanzilishi wa dhana hii ya kwamba Rais Magufuli ni dikteta uchwara. Kwa kuanzia, ninapenda kuwashutumu polisi na watawala wa CCM kwa namna walivyolishughulikia suala hili.

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, Tundu Lissu ana haki na uhuru wa kuwa na mawazo yake kuhusu suala lolote. Ana haki na uhuru wa kuwa na mtazamo wake juu ya Rais Magufuli. Ana haki na uhuru wa kutoa mawazo yake kama alivyofanya.

Mtu mwingine yeyote naye ana haki na uhuru huo. Kwa hivi, kauli ya Tundu Lissu haikuhitaji hatua zilizochukuliwa na polisi za kwenda kumkamata na kumsafirisha kutoka Singida hadi Dar es Salaam kwa mahojiano makao makuu ya polisi.

Jambo ambalo lingeweza kufanyika, bila taabu yote hii na ufujaji wa hela za walipa kodi, ilikuwa ni kwa serikali kujibu hoja za Tundu Lissu na kuthibitisha kuwa Rais Magufuli si dikteta uchwara. Malumbano ya hoja yangetosha.

Ndio utaratibu unaotakiwa katika jamii iliyostaarabika. Ninaamini kuwa wa-Tanzania wana akili timamu, na wana uwezo wa kuchambua mambo. Wana uwezo wa kusikiliza hoja za pande mbali mbali na kutambua upande upi ni sahihi.

Madai ya polisi na watawala wa Tanzania kwamba kauli ya Tundu Lissu ni uchochezi ni ya kuwadhalilisha wananchi. Ni kusema kwamba wananchi ni wajinga, wasio na uwezo wa kutathmini na kuchambua mambo.

Ni kwanini serikali haikuchukua njia hii ya kujibu hoja kwa hoja? Inamaanisha kwamba katika serikali nzima hakuna mtu mwenye akili ya kuweza kumpinga Tundu Lissu na kuthibitisha kuwa Rais Magufuli si dikteta uchwara?

Inamaanisha kuwa watendaji wote wa serikali hii ya CCM ni watendaji uchwara, au ni watendaji hewa, au ni vilaza?

Rais Magufuli, kwa mtazamo wangu, amekuwa akivuka mipaka ya katiba kwa baadhi ya kauli zake. Hana mamlaka kikatiba wala kwa mujibu wa sheria za vyama vya siasa, kuweka vizuizi juu ya mikutano na maandamano ya vyama vya siasa. Taratibu zote zimeelezwa katika katiba ya Tanzania na katika sheria ya vyama vya siasa.

Kwa bahati nzuri, katiba ninayo na nimeisoma, na sheria ya vyama vya siasa, ambayo imewekwa kwenye tovuti ya ofisi ya msajili wa vyama, nimeisoma pia: http://www.orpp.go.tz/en/rules/. Kwa kupitia katiba na sheria, ni wazi kuwa Rais Magufuli anakiuka katiba na sheria, na kwa hivyo, kauli ya Tundu Lissu kwamba Rais Magufuli ni dikteta uchwara ni sahihi.

Vyama vya siasa vinawajibika kufanya mikutano na maandamo kwa amani, ili kutangaza sera zao, kutafuta wanachama wapya, na kadhalika. Rais Magufuli, au mtu mwingine yeyote hana wadhifa wa kuwawekea zuio kama alivyofanya. Hana mamlaka ya kusema kwamba watu wafanye siasa katika maeneo yao tu.

Hana mamlaka ya kutangaza, hata kwa kisingizio cha "hapa kazi tu," shughuli zipi za kisiasa zisitishwe hadi mwaka 2020. Huu ni udikteta.

Mimi ni raia ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Ninachotaka ni kuona nchi inaendeshwa kwa mujibu wa katiba na sheria zilizopo. Ninataka utawala wa sheria, unaozingatia haki za binadamu.
 
Unafiki hauko hivyo ........... tafuta maana halisi ya neno unafiki ndiyo utajua nani ni mnafiki na yupi si mnafiki!!
Alitakiwa aje na solution nini kifanyike tutoke hapa tulipo twende mbele!!!

Tena yupo marekani
 
Mimi kama msomi wa Sheria ninakushauri wewe pia na wa TZ wote kwa ujumla sambamba na kudai kuwa Rais wetu ni dicteta hauna budi kabla hujajidhatiti na kauli hiyo uisome vizuri katiba hususani isome na uielewe ibara ya 36 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977,hakika katiba hii kupitia ibara hiyo inampa Rais madaraka makubwa sana ya kufanya chochote kile na ukizingatia kuwa katiba ndio sheria mama na mamlaka yake ni ya juu(siperior authority over any other law applied in Tanzania).Hivyo tatizo si Rais kwani yeye anatumia madaraka ya kikatiba hivyo tatizo kubwa ambalo linatutesa na litaendelea kututesa mda mrefu ni mamlaka ya kikatiba.Hivyo katiba inahitajia mabadiliko ili kupunguza madaraka hayo huku uwe na kumbukumbu kuwa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa alishangaa sana kuona katiba ilivyo mpa madaraka makubwa yeye kama Rais kiasi ambacho alisema angeweza kuwa Dicteta.
 
Kwanza mm nakataa Tanzania hakuna wasomi bali kuna watu waliospend muda wao madarasani na kutunukiwa vyeti kwani changamoto zinazotukabili toka enzi ya uhuru nchi ilipokuwa na ma doctor wazawa 5 na injinia 1 ni zile zile mpka leo interview zinafanyika uwanja wa taifa kwa jinsi degree, masters na phd zilivyo nying nchi hii lakini changamoto ni zile zile za toka enzi za uhuru

Pia tunakiwa kujua maana halisi ya dictator kwa vigezo vya udictator magufuli hana ila kinachomfanaya aonekane dictator ni kutaka watanzania waishi kwa kufata mfumo wa sheria hcho tu. Katiba aijakubali maandamano tu ndo maana kukawa na taasisi zinazotoa vibali vya kufanya maandamano kazi hyo walipewa jeshi la police kwani wao ndo wanahusika na ulinzi wa raia na mali zao sasa kama police wameona viashilia vya uvunjifu wa amani katiba inawaruhusu kupiga marufuku maandamano ayo. Leo huwezi kusema maandamano yatakuwa ya amani wakati unatumia maneno ya lazima,hatukubali,aiwezekani,unaanzisha operation zenye majina ya ajabu sehemu yeyote unaposikia kuna operation hujue hapo amani hakuna aiitaji phd kujua ilo hata hospital operation ndio tiba ya mwisho kwa mgonjwa je leo chadema wameshindwa kutumia njia yeyote mpaka watangaze operation ????

Chama kinachojinasibu kuwa na hazina kubwa ya wasomi leo wameshindwa kutumia njia nyingine zaidi ya kutangaza maandamano dunia nzima hata marekani maandamano huwa yanadhibitiwa na police kwani impact ya maandamano ni kusababisha ulemavu ,usumbufu kwa watu huwezi kufungua biashara wakati maandamano yakiwapo shuguli nyingi za kiuchumi lazima zisimame pia chadema inatakiwa kujua ICC wanakwenda c watawala peke yao mpaka wapinzani wanakwenda pia. mfano kenya kenyatta na ruto walikuwa watawala?? kwa nn asiende kibaki???? ICC wanaangalia source ya vurugu zimesababishwa na nani

Zipo njia nyingi za kufanya harakati zao coz mm naamini hawafanyi siasa bali wanafanya harakati tu kama wameshindwa bungeni sehemu pekee wanayoweza kuishinda serikali na ikakubali ni mahakamani pale ndipo wanaweza kupata haki zao zote tena hao waliokataa wasifanye siasa ndio watakuwa wanawalinda katk mikutano yao si wanawanasheria wazuri basi wakapambane mahakamani kama wanaona katiba imevunjwa coz sheria zinatungwa bungeni zinatafasiliwa mahakamani kuliko kuwaletea vijana wa maskini ulemavu kwa kupigwa mabomu na maji ya kuwasha
 
Technically akili yako haina akili, hujitambui, katika maswala kama haya yanapojadiliwa na watu wenye akili zenye akili kwa maana ya GRAY MATTER, wewe jaribu kufungua kichwa kabla ya kufungua DOMO, Bs
Wewe ndiye ujanielewa unaniatack
 
Technically akili yako haina akili, hujitambui, katika maswala kama haya yanapojadiliwa na watu wenye akili zenye akili kwa maana ya GRAY MATTER, wewe jaribu kufungua kichwa kabla ya kufungua DOMO, Bs
Umeelewa kwanini nimesema unafiki??
Na kama umeelewa umeelewaje??
Ukijibu hayo maswali nitarudi Mimi uwa sipendi ubishi usio na maana uwe chadema uwe ccm nakwambia ukweli tu
 
Back
Top Bottom