Wasomi wazidi kuikosoa Serikali

No wonder maprof wa tanzania wanaendesha tax huko marekani.yani huyu aliyetoa haya maoni nae ni prof kweli?
Heeeeee! Maprof wa kibongo walioko US wanaendesha tax huko? Basi walioko nchini watakuwa wanaendesha Boda Boda!
 
Na Profesa Joseph Mbele

Nimeona nianzishe mjadala wa suala linalovuma wakati huu nchini Tanzania, ambalo ni: Je, Rais Magufuli ni dikteta uchwara?

Tundu Lissu, mwanasheria wa CHADEMA ndiye mwanzilishi wa dhana hii ya kwamba Rais Magufuli ni dikteta uchwara. Kwa kuanzia, ninapenda kuwashutumu polisi na watawala wa CCM kwa namna walivyolishughulikia suala hili.

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, Tundu Lissu ana haki na uhuru wa kuwa na mawazo yake kuhusu suala lolote. Ana haki na uhuru wa kuwa na mtazamo wake juu ya Rais Magufuli. Ana haki na uhuru wa kutoa mawazo yake kama alivyofanya.

Mtu mwingine yeyote naye ana haki na uhuru huo. Kwa hivi, kauli ya Tundu Lissu haikuhitaji hatua zilizochukuliwa na polisi za kwenda kumkamata na kumsafirisha kutoka Singida hadi Dar es Salaam kwa mahojiano makao makuu ya polisi.

Jambo ambalo lingeweza kufanyika, bila taabu yote hii na ufujaji wa hela za walipa kodi, ilikuwa ni kwa serikali kujibu hoja za Tundu Lissu na kuthibitisha kuwa Rais Magufuli si dikteta uchwara. Malumbano ya hoja yangetosha.

Ndio utaratibu unaotakiwa katika jamii iliyostaarabika. Ninaamini kuwa wa-Tanzania wana akili timamu, na wana uwezo wa kuchambua mambo. Wana uwezo wa kusikiliza hoja za pande mbali mbali na kutambua upande upi ni sahihi.

Madai ya polisi na watawala wa Tanzania kwamba kauli ya Tundu Lissu ni uchochezi ni ya kuwadhalilisha wananchi. Ni kusema kwamba wananchi ni wajinga, wasio na uwezo wa kutathmini na kuchambua mambo.

Ni kwanini serikali haikuchukua njia hii ya kujibu hoja kwa hoja? Inamaanisha kwamba katika serikali nzima hakuna mtu mwenye akili ya kuweza kumpinga Tundu Lissu na kuthibitisha kuwa Rais Magufuli si dikteta uchwara?

Inamaanisha kuwa watendaji wote wa serikali hii ya CCM ni watendaji uchwara, au ni watendaji hewa, au ni ******?

Rais Magufuli, kwa mtazamo wangu, amekuwa akivuka mipaka ya katiba kwa baadhi ya kauli zake. Hana mamlaka kikatiba wala kwa mujibu wa sheria za vyama vya siasa, kuweka vizuizi juu ya mikutano na maandamano ya vyama vya siasa. Taratibu zote zimeelezwa katika katiba ya Tanzania na katika sheria ya vyama vya siasa.

Kwa bahati nzuri, katiba ninayo na nimeisoma, na sheria ya vyama vya siasa, ambayo imewekwa kwenye tovuti ya ofisi ya msajili wa vyama, nimeisoma pia: http://www.orpp.go.tz/en/rules/. Kwa kupitia katiba na sheria, ni wazi kuwa Rais Magufuli anakiuka katiba na sheria, na kwa hivyo, kauli ya Tundu Lissu kwamba Rais Magufuli ni dikteta uchwara ni sahihi.

Vyama vya siasa vinawajibika kufanya mikutano na maandamo kwa amani, ili kutangaza sera zao, kutafuta wanachama wapya, na kadhalika. Rais Magufuli, au mtu mwingine yeyote hana wadhifa wa kuwawekea zuio kama alivyofanya. Hana mamlaka ya kusema kwamba watu wafanye siasa katika maeneo yao tu.

Hana mamlaka ya kutangaza, hata kwa kisingizio cha "hapa kazi tu," shughuli zipi za kisiasa zisitishwe hadi mwaka 2020. Huu ni udikteta.

Mimi ni raia ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Ninachotaka ni kuona nchi inaendeshwa kwa mujibu wa katiba na sheria zilizopo. Ninataka utawala wa sheria, unaozingatia haki za binadamu.
Mleta mada mwenyewe utata mtupu
 
Halafu huko Marekani vyama vya siasa vinafanya maandamano na mikutano ya hadhara kuikashifu serikali baada ya uchaguzi? Mbele amefilisika sana.
Kaangalie tena mkutano wa democrat, Chama kinachoongoza serikali, kwenye mkutano wamemzomea mgombea wao na hata rais Obama mwenyewe. Huko paache palivyo hakuna hotuba za "mimi" kule ni "sisi" sio democrat wala Republican sisi wamarekani.
 
Kaangalie tena mkutano wa democrat, Chama kinachoongoza serikali, kwenye mkutano wamemzomea mgombea wao na hata rais Obama mwenyewe. Huko paache palivyo hakuna hotuba za "mimi" kule ni "sisi" sio democrat wala Republican sisi wamarekani.
Hayo ndio maandamano?
 
Kisarufi neneo uchwara linapaswa kuambatana na neno linaloashiria positivity kwa sababu lenyewe ni negative. Mfano mwanasiasa uchwara, msomi uchwara, tajiri uchwara na wala si mjinga uchwara au dikteta uchwara masikini uchwara n.k. labda ingefaa kusema mwanademokrasia uchwara. ikiwa maneno mawili yanaashiria negativity maana yake itakuwa positive. mfano tukisema; it is not uncommon to see coconut trees along the coast. maana yake ni kwamba ni kawaida kuiona minazi ukanda wa pwani.
Sasa ukienda kiundani sana unaweza kuhitimisha kuwa dikteta uchwara inaashiria kitu tofauti sana na kile wengi wanachokitolea povu hadi kumsaka Lisu kama wanamsaka Idd Ami!
 
CHADEMA wanavaa magwanda ikiwa na maana ya vazi la kijeshi. wanaitana makamanda neno litumikalo jeshini kuashiria viongozi wa mapambano.
kauli zao ni za kutisha adui aogope. majina wanayowapa maadui zao si mazuri yanafanan na yale ya wanajeshi wanayowapa maadui zao. mfano nduli Amini, Joka kuu nk.
Hii ni mbinu tu katika medani ya siasa. Labda tuiite gun boat diplomacy
Kama tukiwa na uvumilivu wa kisiasa tunaweza kutafakari haya na kukabiliana na hii hali kidiplomasia and more intelligently kuliko kupaniki na kujiandaa kurusha ngumi. bora mabondia wanatishana kabla ya pambano lakini pambano likiisha wanakumbatiana. Hili la kwetu halitakuwa hivyo! so tuwe makini pande zote mbili.
 
Mimi kama msomi wa Sheria ninakushauri wewe pia na wa TZ wote kwa ujumla sambamba na kudai kuwa Rais wetu ni dicteta hauna budi kabla hujajidhatiti na kauli hiyo uisome vizuri katiba hususani isome na uielewe ibara ya 36 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977,hakika katiba hii kupitia ibara hiyo inampa Rais madaraka makubwa sana ya kufanya chochote kile na ukizingatia kuwa katiba ndio sheria mama na mamlaka yake ni ya juu(siperior authority over any other law applied in Tanzania).Hivyo tatizo si Rais kwani yeye anatumia madaraka ya kikatiba hivyo tatizo kubwa ambalo linatutesa na litaendelea kututesa mda mrefu ni mamlaka ya kikatiba.Hivyo katiba inahitajia mabadiliko ili kupunguza madaraka hayo huku uwe na kumbukumbu kuwa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa alishangaa sana kuona katiba ilivyo mpa madaraka makubwa yeye kama Rais kiasi ambacho alisema angeweza kuwa Dicteta.
Mkuu, mbona ibara ya 36 inazungumzia juu ya mamlaka ya kuanzisha na kuwateua watu kushika nafasi za madaraka....Sijaona popote katika ibara hiyo palipompa mamlaka makubwa ya kufanya chochote anachotaka nje ya kuanzisha, kuteua watu kushika nafasi za madaraka. Labda utupe ibara nyingine inayompa mamlaka hayo makubwa ya kufanya chochote akitakacho including kuzuia vyama vya siasa na wanasiasa kutofanya kazi za siasa mpaka 2020. Au panapompa mamlaka ya kutoa tangazo la kuruhusu kufanyika kwa mikutano ya siasa ambayo itafanywa na madiwani na wabunge kwenye maeneo yao waliyochaguliwa. Ninashauku sana ya kutoka kujua hii mamlaka Rais anaitoa wapi...Tafadhari nisaidie ndugu yangu msomi wa sheria Kassim Rashid
 
Kwanza mm nakataa Tanzania hakuna wasomi bali kuna watu waliospend muda wao madarasani na kutunukiwa vyeti kwani changamoto zinazotukabili toka enzi ya uhuru nchi ilipokuwa na ma doctor wazawa 5 na injinia 1 ni zile zile mpka leo interview zinafanyika uwanja wa taifa kwa jinsi degree, masters na phd zilivyo nying nchi hii lakini changamoto ni zile zile za toka enzi za uhuru

Pia tunakiwa kujua maana halisi ya dictator kwa vigezo vya udictator magufuli hana ila kinachomfanaya aonekane dictator ni kutaka watanzania waishi kwa kufata mfumo wa sheria hcho tu. Katiba aijakubali maandamano tu ndo maana kukawa na taasisi zinazotoa vibali vya kufanya maandamano kazi hyo walipewa jeshi la police kwani wao ndo wanahusika na ulinzi wa raia na mali zao sasa kama police wameona viashilia vya uvunjifu wa amani katiba inawaruhusu kupiga marufuku maandamano ayo. Leo huwezi kusema maandamano yatakuwa ya amani wakati unatumia maneno ya lazima,hatukubali,aiwezekani,unaanzisha operation zenye majina ya ajabu sehemu yeyote unaposikia kuna operation hujue hapo amani hakuna aiitaji phd kujua ilo hata hospital operation ndio tiba ya mwisho kwa mgonjwa je leo chadema wameshindwa kutumia njia yeyote mpaka watangaze operation ????

Chama kinachojinasibu kuwa na hazina kubwa ya wasomi leo wameshindwa kutumia njia nyingine zaidi ya kutangaza maandamano dunia nzima hata marekani maandamano huwa yanadhibitiwa na police kwani impact ya maandamano ni kusababisha ulemavu ,usumbufu kwa watu huwezi kufungua biashara wakati maandamano yakiwapo shuguli nyingi za kiuchumi lazima zisimame pia chadema inatakiwa kujua ICC wanakwenda c watawala peke yao mpaka wapinzani wanakwenda pia. mfano kenya kenyatta na ruto walikuwa watawala?? kwa nn asiende kibaki???? ICC wanaangalia source ya vurugu zimesababishwa na nani

Zipo njia nyingi za kufanya harakati zao coz mm naamini hawafanyi siasa bali wanafanya harakati tu kama wameshindwa bungeni sehemu pekee wanayoweza kuishinda serikali na ikakubali ni mahakamani pale ndipo wanaweza kupata haki zao zote tena hao waliokataa wasifanye siasa ndio watakuwa wanawalinda katk mikutano yao si wanawanasheria wazuri basi wakapambane mahakamani kama wanaona katiba imevunjwa coz sheria zinatungwa bungeni zinatafasiliwa mahakamani kuliko kuwaletea vijana wa maskini ulemavu kwa kupigwa mabomu na maji ya kuwasha
umeisoma sheria ya vyama vya siasa au unazungumzia nini, polisi hawana mamlaka ya kuzuia bali kutoa ulinzi. au ndy walewale mlio spend muda wenu madarasani
 
Huyo msomi ni mnafiki kaongea mambo yaleyale bila kuleta solution!!
Mkuu huyo Msomi Prof katoa njia ya kuleta solution, kw kuiomba Govt ijibu hoja ya Mh Lissu.
Ili ss Watanzania tupate kuzichambua hoja zao...
Mkuu punguza hasira tuijenge Nchi yetu tupate kufika, wenzetu wanazidi kutuacha mbali....
 
Back
Top Bottom