chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,961
Wasomi na wadau mbalimbali wa siasa wameponda hotuba ya Magufuli aliyoitoa Dodoma alipokuwa akikabidhiwa uenyekiti na Jakaya Kikwete
Mojawapo ya wasomi hao ni lecturer wa chuo kikuu cha Ruaha (RUCU) Prof. Gaudence Mpangala akisema kuwa haikuwa sahihi kwa Magufuli kutangaza Dodoma kuwa watumishi wote wa umma lazima wawe chini ya CCM alisema ''Watumishi wa umma hawapaswi kuwa chini ya chama cha siasa hata kama ni chama tawala, Magufuli hakuwa sahihi, CCM inapaswa kutimiza ilani yake lakini sio kwa njia ya kuwaingilia watumishi wa umma''
Naye Profesa Wa UDSM Kitila Mumbo amesema anashangazwa na kitendo cha mwenyekiti huyo wa chama kupiga marufuku mikutano ya siasa wakati ndio inayowapakuonekana na kusikika na wananchi
Naye mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa amesema jukumu la watumishi wa umma wanasimamiwa na bunge kwa upande wa serikali kuu na madiwani kwa upande wa serikali za mitaa, amesema wanatarajia kuwa ataruhusu mikutano ya siasa ambayo ameipiga marufuku
Naye kiongozi wa ACT Zitto Kabwe amesema ameshangazwa sana na kitendo chake cha kuwatishia kuwafukuza wanachama wanaokikosoa chama
Naye mchambuzi wa siasa kutoka CUF Julius Mtatiro amesema japo amefurahishwa na hotuba hiyo kugusia mambo muhimu kama kuondoa rushwa kwenye chama na kuhamishia makao makuu Dodoma japo kuna mengine hayakuzungumziwa kwa kina lakini ameponda kitendo cha Magufuli kusema kuwa wanachama wa CCM ndio watakua ma boss wa watumishi wa umma