Wasomi waponda hotuba ya Magufuli Dodoma

Wasomi waponda hotuba ya Magufuli Dodoma

Serikali ina mihimili mikuu mitatu, ambayo ni bunge, mahakama na utawala. Naomba nigusie mhimili wa tatu ambao ni utawala.

Utawala juu kabisa yupo rais, chini yake yuko wazili Na kabinet yote ya mawazili. Tukumbuke kila mwajiliwa yupo Chini ya
Wizala husika, mfano mwalimu yupo wizala ya elimu....
Kwa maana hiyo, ikiwa wazili husika anatokana na chama tawala sina shaka hata mtumishi atatokana na chama husika. Ingawa nchi yetu democrasia yake imetukuka, mwajiliwa atajijua chama Chake ila kiuhalisia anatakiwa kuwa na chama tawala ili akitumikie chama na kutekeleza ilani ya chama hicho. Kwa Lugha nyingine, mtumishi asiyeendana na ilani ya chama Huyo anakwamisha juhudi za serikali ndo maana huitwa jipu na kutumbuliwa.

Maana yangu ni kwamba rais hajakosea kusema mtumishi ni mwana ccm
 
Hahahaha hiyo list ya wasomi sasa hadi Msigwa yupo...!

Hivi Zitto ni mzima kweli wa akili? Ni wapi Mh Rais alisema atawafukuza wanao kikosoa chama?Nadhani sasa Zitto ana karibia kuchanganyikiwa..
hahaha Zito bado ana mawenge ya kufukuzwa chadema. alisahau alivyokosoa chadema tu alifukuzwa akakimbilia mahakamani. akawa mbunge wa mahakama. leo yooote kayasahau. kwa sababu angekuwa anayakumbuka asinge mshangaa Magufuli
 
Kwa kawaida Chama kinakuwa na sera na serikali inatafsiri hizo sera katika sheria na taratibu ambazo hutekelezwa na watumishi.
Chama hakifanyi kazi siku kwa siku na watumishi. Mfano sera ya elimu bure itatafsiriwa katika sheria na kanuni na kutekelezwa kiserikali na si kichama. Kwa hiyo itakuwa ajabu, mfano, kiongozi wa chama kwenda kwenye ofisi ya serikali na kuagiza jambo lolote. Kwa mantiki hiyo viongozi wa chama sio immediate bosses wa watumishi wa umma. Tusidanganyane bure ama sivo tunaweza kuleta vurugu bure!
 
Mkuu kama huyo ni professor basi tuna safari ndefu!!

hivi msomi gani asiyejua kuwa hii ni selikari iliyochini ya CCM??

Mfano mimi ni Mkurugenzi NHC,ina maana boss wangu ni kinana?Inamaana Kinana anaweza kuja ofisini kwangu na kuanza kunichimba mkwara juu ya utendaji wangu?Nonsense
 
Mkuu kama huyo ni professor basi tuna safari ndefu!!

hivi msomi gani asiyejua kuwa hii ni selikari iliyochini ya CCM??
Kama ni hivyo si angechagua makada wa ccm kwenye ngazi zote za utumishi wa umma
 
Naomba kuuliza ni nani anayeoongoza serikali? watumishi wa serikali wanafanya kazi ili kutimiza Ilani ya chama gani? watumishi waliopo katika wizara waziri ni wa chama gani na mwanachama wa chama gani?
Ccm,kwahiyo?
 
Hahahaha hiyo list ya wasomi sasa hadi Msigwa yupo...!

Hivi Zitto ni mzima kweli wa akili? Ni wapi Mh Rais alisema atawafukuza wanao kikosoa chama?Nadhani sasa Zitto ana karibia kuchanganyikiwa..
Kwani wewe hukusikia aliposema angekuwa yeye ndio JK halafu nusu ya wanachama wakaimba kuwa wanaimani na mtu Fulani basi robo au nusu wangepotea!Jifikirishe kabla ya kujibu
 
Wasomi na wadau mbalimbali wa siasa wameponda hotuba ya Magufuli aliyoitoa Dodoma alipokuwa akikabidhiwa uenyekiti na Jakaya Kikwete

Mojawapo ya wasomi hao ni lecturer wa chuo kikuu cha Ruaha (RUCU) Prof. Gaudence Mpangala akisema kuwa haikuwa sahihi kwa Magufuli kutangaza Dodoma kuwa watumishi wote wa umma lazima wawe chini ya CCM alisema ''Watumishi wa umma hawapaswi kuwa chini ya chama cha siasa hata kama ni chama tawala, Magufuli hakuwa sahihi, CCM inapaswa kutimiza ilani yake lakini sio kwa njia ya kuwaingilia watumishi wa umma''
Naye Profesa Wa UDSM Kitila Mumbo amesema anashangazwa na kitendo cha mwenyekiti huyo wa chama kupiga marufuku mikutano ya siasa wakati ndio inayowapakuonekana na kusikika na wananchi

Naye mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa amesema jukumu la watumishi wa umma wanasimamiwa na bunge kwa upande wa serikali kuu na madiwani kwa upande wa serikali za mitaa, amesema wanatarajia kuwa ataruhusu mikutano ya siasa ambayo ameipiga marufuku

Naye kiongozi wa ACT Zitto Kabwe amesema ameshangazwa sana na kitendo chake cha kuwatishia kuwafukuza wanachama wanaokikosoa chama

Naye mchambuzi wa siasa kutoka CUF Julius Mtatiro amesema japo amefurahishwa na hotuba hiyo kugusia mambo muhimu kama kuondoa rushwa kwenye chama na kuhamishia makao makuu Dodoma japo kuna mengine hayakuzungumziwa kwa kina lakini ameponda kitendo cha Magufuli kusema kuwa wanachama wa CCM ndio watakua ma boss wa watumishi wa umma
Huyo msomi kasomea wapi? Hajui serikali iliyoko madarakani ni ya CCM? Na hajui ilani inayotekelezwa ni ya CCM? Na hajui watekelezaji wa hiyo ilani ya CCM ni watumishi wa umma?
 
Vipi ile kauli ya Ng'ombe kuvunjika mkia hakuna hata msomi alieikosoa??
 
Wasomi na wadau mbalimbali wa siasa wameponda hotuba ya Magufuli aliyoitoa Dodoma alipokuwa akikabidhiwa uenyekiti na Jakaya Kikwete

Mojawapo ya wasomi hao ni lecturer wa chuo kikuu cha Ruaha (RUCU) Prof. Gaudence Mpangala akisema kuwa haikuwa sahihi kwa Magufuli kutangaza Dodoma kuwa watumishi wote wa umma lazima wawe chini ya CCM alisema ''Watumishi wa umma hawapaswi kuwa chini ya chama cha siasa hata kama ni chama tawala, Magufuli hakuwa sahihi, CCM inapaswa kutimiza ilani yake lakini sio kwa njia ya kuwaingilia watumishi wa umma''
Naye Profesa Wa UDSM Kitila Mumbo amesema anashangazwa na kitendo cha mwenyekiti huyo wa chama kupiga marufuku mikutano ya siasa wakati ndio inayowapakuonekana na kusikika na wananchi

Naye mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa amesema jukumu la watumishi wa umma wanasimamiwa na bunge kwa upande wa serikali kuu na madiwani kwa upande wa serikali za mitaa, amesema wanatarajia kuwa ataruhusu mikutano ya siasa ambayo ameipiga marufuku

Naye kiongozi wa ACT Zitto Kabwe amesema ameshangazwa sana na kitendo chake cha kuwatishia kuwafukuza wanachama wanaokikosoa chama

Naye mchambuzi wa siasa kutoka CUF Julius Mtatiro amesema japo amefurahishwa na hotuba hiyo kugusia mambo muhimu kama kuondoa rushwa kwenye chama na kuhamishia makao makuu Dodoma japo kuna mengine hayakuzungumziwa kwa kina lakini ameponda kitendo cha Magufuli kusema kuwa wanachama wa CCM ndio watakua ma boss wa watumishi wa umma

Mabosi wakubwa na wa kudumu nchini ni wananchi ambao wanakipa chama mamlaka ya kuunda serikali kwa ajili ya kuhakikisha maisha yanakuwa bora, halafu chama tawala ndio boss wa muda wa serikali - kwa mkataba wa miaka mitano mitano tu. Hivyo JPM alikuwa sahihi.
 
Prof. Ndalichako inabidi apitie na cv za wahadhiri kama wanazo sifa stahiki.
 
Hotoba yake JPM nzuri wala hajasema watumishi lazima wawe CCM hao wasomi hawajamuelewa wanafanya analysis uku wakiwa na lengo la kukosoa wala sio kubonyeza isitoshe wasomi hao ni wapinzani unategemea nini situ wapinzani ni wapinzani uchwara.

Kuhusu kuwatishia wanaomkosoa JPM Kwamba atawafukuza MH Zito ujamuelewa JPM kama umemuelewa unawadanganya wananchi,JPM alisema wasaliti ni wale wanaokua mchana CCM na usiku UKAWA akimanisha wanakwamisha chama kisisonge mbele kama wewe walivokutuumu CDM kwamba unawasaliti kuna majimbo uliwauzia CCM JPM hao wanamna hiyo amesema atawatumbua
Hivi kusifu kunajenga???
Ni bora kukosoa udhaifu ili kuimarisha jambo.. Tatizo wabongo tunapenda sifa
 
Back
Top Bottom