Kasekenya awataka TEMESA kuwa wabunifu

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amewataka watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kuangalia namna bora ya kuja na ubunifu katika maeneo yao ya kazi ili kuboresha utendaji kazi wao wa kila siku.

Naibu Waziri ameyasema hayo leo Tarehe 18 Machi, 2024 wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa Wakala huo ambapo amefanya pia Ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa
Baraza la Wafanyakazi.

Mkutano huo wa Baraza la Wafanyakazi umefanyika katika Ofisi za TEMESA Makao Makuu mjini Dodoma na kuhudhuriwa na baadhi ya watumishi waliowawakilisha Watumishi wenzao kutoka Mikoa na vituo pamoja na Mameneja wa Mikoa.

Naibu Waziri Kasekenya amesema wakala unatakiwa kujiendesha kibiashara ili kuongeza pato la Serikali na kuwagiza watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuzingatia ushindani wa kibiashara.

”Kuweni wabunifu wa vyanzo vipya vya mapato, wabunifu katika matumizi ya mifumo ya
TEHEMA na mbinu mbalimbali za kibiashara, ni vyema tukakumbushana kwamba Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi imeweka malengo
mbalimbali na utekelezaji wa Ilani hiyo unategemea watumishi wa umma”. Amesema
Kasekenya.

Kasekenya ameongeza kuwa TEMESA inatengeneza magari ya Serikali ili kuwawezesha watumishi wengine wa Umma kufikia malengo mbali mbali ili kutekeleza majukumu yao
hivyo amewataka wakala kukumbuka dhamana waliyopewa na kuwaasa kusoma na kuelewa na kutekeleza Ilani ya Chama.

Aidha kasekenya amewataka watumishi kuzingatia maadili katika utendeji kazi na kutoa rai kwa watumishi wanaofanya biashara na TEMESA kwa kificho au wazi kwa kupitia kampuni binafsi na kupelekea mgongano wa kimaslahi waache tabia hiyo kwakuwa hawataiwezesha TEMESA kufikia malengo yake waliyojiwekea.

IMG-20240318-WA0415(1).jpg
IMG-20240318-WA0414(1).jpg
IMG-20240318-WA0413(1).jpg
 
Back
Top Bottom