Wasomi wa Tanzania wametoa mchango gani kwenye Taifa letu mpaka sasa?

Diamond Platnumz kijana wa juzi tu kutoka Tandale mpaka sasa ameshatengeneza Ajira zaidi ya 50.Lakini wanaojiita Wasomi wa Tanzania kazi wanayoweza kila siku ni Kulaumu Serikali,CCM,Nchi ,Wanasiasa.Wamekuwa wazee wa Lawama,Lawama.Wanalaumu kula kitu isipokuwa Uzuzu wao wenyewe na a Ukosefu wa Ubunifu.Huwezi kumsikiliza msomi wa Tanzania ukapata jibu LA tatizo lolote.Nchi yoyote itajivunia kuwa na Diamond Platnumz mmoja kuliko kuwa na Kina Jenerari Ulimwengu 90000000
00000000.
 
Haiwezekani uchumi unayumba hawana la kutufanya kama wasomi, hawajui njia zipi za kutatua hili tatizo,

Yangu ni hayo,
 
Nimekuwa nikijiuliza sana kwa nini wasomi wetu hudanganywa na ccm, maana ukifatilia kwa undani utagundua wazi ndani ya chama cha ccm kuna propaganda nyingi kuliko uhalisia na uongo mwingi kuliko ukweli, pia utagundua kuna nadharia nyingi kuliko vitendo na mbwembwe nyingi kuliko utaalamu.

Ngoja nitoe mifano michache, leo chama hicho kinaimba wimbo kuwa nchi hii inakwenda kuwa nchi ya viwanda na tayari wameshatoa taarifa ya nchi kuwa na viwanda zaidi ya 2000 kuna uwezekano upi kwa nchi hii kuwa ya viwanda bila kuwepo kwa miundombinu madhubuti ya nishati ya umeme? hivyo viwanda zaidi ya 2000 vingeshindwaje kuajiri zaidi ya vijana wetu 100000 wanaozunguka ofisi zote kutafuta ajira?

Kwa nini wasomi walioko ccm wanashindwa kutoa ushauri wao wa kitaaluma kiasi cha kuwaachia wakina Kibajaji wawe ndio washauri wao? huku USA mtaalamu ndie mwenye sauti na mtoa dira ya maendeleo ya nchi wala siyo hao wana siasa walioishia darasa la saba bila cheti
 
Mkuu
Naungana nawe kabisa, ila nadhani ungesema wasomi wengi hudanganywa na wanasiasa (vyama vya siasa) na siyo CCM tu.
Tumeona jinsi wasomi wanavyo kimbilia kwenye siasa badala ya kubakia kwenye utaalamu wao. Wakifika huko wanageuka wana propaganda badala ya kuwa wataalamu. Yote hiyo ni kutafuta maisha ya mazuri bila kuyatabikia.
 
Nianze na salaam kwa wanajamvi,

Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na fadhili kwa kuniwezesha nami kuwa mmoja kati ya wasomi katika nchi yetu. Natumaini ni mkono wake ulioniongoza kwani mimi pekee nisingeweza hata kidogo.

Nchi yoyote imbayo inapiga maendeleo inategemea vitu vitatu.

Mosi ni wasomi ambao kwa kulingana na ufahamu wao wanatakiwa kuwa watu wa kufanyia kazi yale walichojifunza kwa jasho na damu na kuyaweka ili yawe msingi wa maendeleo ya nchi kulingana na tabia nchi yetu.

Pili ni watu ambao kwa kawaida watatunga sera kwa kufasiri yale ambayo wasomi wameyanyumburisha (principles).

Na mwisho ni tabaka la watenda kazi, hawa ni wale ambao wanayabadilisha mawazo ya wasomi kuwa vitendo.

Kwa mtazamo wangu hizi ndio nguzu muhimu katika ustawi wa jamii husika
Cha kuchekesha na kuogofya ni kwamba watu ambao wanatakiwa kuwa wafikiliaji wakuu katika kuunda zana (principles and laws) wanapogeuka kuwa vibaraka wa kundi la pili na kusababisha hilo kundi ndio liwe na kazi ya kufanya yale ya kundi la kwanza.

Hii inateletelea kundi la tatu kukosa miongozo thabiti hivyo kupelekea kuwa na udumavu wa maendeleo.

Kwa nchi yetu ilipofikia sasa ni kuwa wasomi wamekuwa na utapiamlo katika kufanya kazi yao, hii ni aibu kwa wasomi kugeuka kuwa chawa wa utawala
Siku zote msomi anatakiwa kuwa chombo cha maendeleo na si chombo cha kudumaza hayo maendeleo.

Wasomi tunatakiwa tuisimamie kweli hata kama itapelekea kukosa na utawala
Matatizo ya nchi yetu ni mengi na yanazidi kuwa mengi pale ambapo kundi ambalo lilitakiwa kuyatafutia ufumbuzi lianpogeuka kuwa sehemu ya matatizo hayo.

Asanteni
 
Watu wanaamini kusoma sana ni kuongeza maarifa na kuwa na upeo mkubwa wa kuelewa mambo.

Hata hivyo, kuna watu/mtu mwenye PhD ambae anakatisha watu tamaa kabisa na anaifanya PhD ionekane wala haina maana maana mtu/watu hao wanaonekana kukosa kabisa maarifa hata kwa mambo madogo na matokeo yake tunaona wanavyovurunda kila kukicha.

Ni wazi unaweza ukawa na bachelor degree ya GPA 2.2 lakini ukawa bora katika kufanya maamuzi na kutumia maarifa ulionayo kuliko mtu mwenye PhD.

Nafikiri wakati umefika tuanze kufanya research kwa ngazi ndogo kabisa ya familia tuone kati ya wasomi wenye PhD na wale wenye elimu ndogo ni kwa kiasi gani wanamudu kuendesha familia zao kwa mafanikio.
 
Watu wanaamini kusoma sana ni kuongeza maarifa na kuwa na upeo mkubwa wa kuelewa mambo.

Hata hivyo kuna watu/mtu mwenye PhD ambae anakatisha watu tamaa kabisa na anaifanya PhD ionekane wala haina maana maana mtu huyo ameonekana kukosa maarifa kabisa hata kwa mambo madogo.

Ni wazi unaweza ukawa na bachelor degree ya GPA 2.2 lakini ukawa bora katika kufanya maamuzi na kutumia maarifa ulionayo kuliko mtu mwenye PhD.

Nafikiri wakati umefika tuanze kufanya research kwa ngazi ndogo kabisa ya familia tuone kati ya wasomi wenye PhD na wale wenye elimu ndogo ni kwa kiasi gani wanamudu kuendesha familia zao kwa mafanikio.
Kaka PhD zingine ni za maganda ya korosho na zimeandikwa kisukuma hivyo hazina msaada wowote katika jamii. Mbona kuna watu wan PhD za Kiswahili na wameandika hata vitabu tunavisoma, hivyo usilaumu PhD zote!
 
Ndio maana wapo wengi tu wenye shahada halisi za udaktari (Scholarly Doctorates) hata hawazitumii kwenye majina Yao kwa sababu ya shida hiyo.
 
wamekufundisha wewe ukajua kusoma na kuandika ndo maana uko JF unapiga zumari kama vuvuzela
 
Back
Top Bottom