Maramla
JF-Expert Member
- Jan 8, 2014
- 581
- 642
Wasomi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamesema mageuzi aliyoyaanza Rais Samia Suluhu Hassan katika eneo la HakiJinai yanapaswa kuwa endelevu.
Mhadhiri wa Sheria Chuoni hapo Dkt. Saudin Jacob anasema uchambuzi na maboresho mbalimbali katika mfumo wa haki jinai ni mwafaka kwa sasa na hata wasomi waliandikia hayo kwa muda lakini sasa yanakwenda kupata utashi wa kisiasa.
Wanafunzi wa fani za sheria na ustawi wa jamii waliochangia mdahalo huo chini ya TBC uliohusisha pia baadhi ya wajumbe wa Tume ya Rais ya Haki Jinai walioongozwa na Makamu Maenyekiti Balozi Ombeni Sefue, wamezitaka taasisi zilizoguswa kuanza mageuzi hayo mara moja badala ya kusubiri.
Mmoja wa wajumbe wa Tume hiyo, Dkt. Laurean Ndumbaro naye amesema mambo waliyoyaibua yanakwenda kuboresha maisha ya wananchi na kuwaongezea uwezo wa kuendesha shughuli zao za kiuchumi bila bughudha. “Kwa hiyo haki jinai ni suala la kidemokrasia lakini pia ni suala la kiuchumi.”