Chambulo amwambia Gavana wa Benki kuu kuwa dollarization ipo kubwa zaidi serikalini

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753

View: https://youtu.be/0UZFmqxo2AY?si=2Q43Jp6nYxZ0pW5U

Hadi gavana hajui sababu ya matatizo ya $? Auibu

Mwenyekiti wa Chama cha watalii Tanzania, Wilbard Chambulo, amesema kuwa dollarization ipo zaidi serikalini na inasababisha watu wa wengine wadai dola. Amezungumza hayo baada ya Gavana wa Benki Kuu, Emmanuel Tutuba kuwataka wenye hoteli kutumia shilingi badala ya dola.

Chambulo amemwambia Gavana kuwa serikali inaokea tozo na kufanya usajiri kwa dola, hivyo inaleta ugumu kwa wao kutumia shilingi kwenye hoteli na sekta ya utalii kwa ujumla.
 
Huyo mfanyabiashara namjua vizuri, Yuko vyema kwenye biashahara ya utalii huko Arusha. Nimekuwa nikikutana naye sana kwenye biashahara zangu, anajua uchumi kwa uhalisia sio hao waliokariri uchumi wa nadharia.
Huwezi kuamini huyu jamaa alipotoka.
Kaburu ni Chotara aliyepitia maisha ya shida na taabu kibao.

Nilimwona na macho yangu akichoma mahindi Sanawari na baadae Metropol Sokoine Road.

Kaburu ni Std 7 ya kuungaunga.

Alipata bahati kwasababu ya rangi yake (Chotara) wazungu waliokuja kutembelea Tanzania miaka hiyo walimchukua sikumbuki vizuri nadhani ni Australia early 1980s kama kumbukumbu zipo aliishi huku 4 or 5 years akarejea Tanzania.

Kampuni zake Kibo Guides & Wilderness Camps ni miongoni mwa makampuni makubwa sana ya utalii.

Jamaa ni kichwa sana, na ana mpunga mrefu kweli kweli .Enzi za Bwana yule walichukua mpunga mrefu sana kupitia tozo na kodi mbali mbali za kubambika.

Machalii wa Sanawari na Kaloleni wengi wamelamba ajira katka kampuni zake.Mara nyingi sana si mtu wa kujishughulisha na vyeti au CV nzito nzito yeye anajali zaidi utendaji.
 
Huwezi kuamini huyu jamaa alipotoka.
Kaburu ni Chotara aliyepitia maisha ya shida na taabu kibao.

Nilimwona na macho yangu akichoma mahindi Sanawari na baadae Metropol Sokoine Road...
Yap wewe unamjua vizuri, alichukuliwa na mzungu wa DickDick. Jamaa huwa anajali watu wachapa kazi, sio maCV.
 
Ameibua hoja nzuri sana. BOT haiwezi kuzuia dollarization wakati taasisi za Serikali zinataka malipo kwa $ kama vile tupo Zimbabwe
 
Huyo mfanyabiashara namjua vizuri, Yuko vyema kwenye biashahara ya utalii huko Arusha. Nimekuwa nikikutana naye sana kwenye biashahara zangu, anajua uchumi kwa uhalisia sio hao waliokariri uchumi wa nadharia.
Kaburu yupo kitambo kwwnye game.
Ana kampuni ya utalii inaitwa kibo na campsites kibao
 
Sasa dereva wa watalii unamtozaje leseni kwa dola!!?. Inamana serikali ndiyo inayohamasisha dollarazation. Huu ni ujinga mkubwa.

Ukweli ni kuwa dollar yoyote inayoingia nchini inatakiwa kuingia serikalini, na serikali impe yule anayetaka kutumia pesa humu ndani Tsh. Hakutakiwi kuwa na Buro de change yoyote wala kuchange dola hotelini wala mtaani. Benki za serikali ndizo zinatakiwa kupokea na kuchange dollar zote nchini. Dollar amazo mwishowe huingia hazina. Mfanyabiashara akitaka kununua kitu nje serikali ipokee Tsh zake na kumpa dollar akanunue vitu. Bila ya hivyo dollar itazidi kuadimika huku ikidhidi kuongezeka thamani.

Hivyo ndivyo serikali ya China ilivyoweza kutengeneza akiba ya dola. Lakini hii system inahitaji ukauzu sana kwenye usimamizi. Vinginevyo wahuni watakuwa wanajikombea akiba ya dollar zilizoingizwa nchini na wakulima wa mazao ya biashara, wachimba dhahabu na makampuni ya kitalii na kisha kwenda kuzitumbua. Mtu kama JPM pekee ndiye alikuwa anaelekea kusimamisha system kama hii.
 
1711713232375.png
 
Back
Top Bottom