Wasomi mmemsikia Edward Lowassa?

Wasomi mmemsikia Edward Lowassa?

Kile kilio cha siku nyingi cha maumivu ya mkopo wa elimu ya juu kinakaribia kupatiwa jibu. Mgombea wa Urais wa CHADEMA/UKAWA Edward Lowassa ameahidi kuwasamehe wale wote waliokopeshwa na kodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB). Lowassa anamaanisha kuwa wanaodaiwa hawatalipa tena na itakuwa ni kama wamesomeshwa bure tu na Serikali yao.

Wakati huohuo, Lowassa anaendelea kusisitiza kuwa elimu ya chuo kikuu itakuwa bure. Wasomi wa wakati wa nyuma na wale wa sasa, mnataka nini tena? Lowassa, kutokana na ahadi zake za kiuchaguzi, anatamani kuona elimu inakuwa bure na hata wale waliokopeshwa wakijisikia kuwa wamesoma bure. Lengo kuu ni kutoa elimu ya bure na bora kwa maendeleo ya Tanzania yetu.

Mtampa kura wasomi wa Tanzania? Wale waliolipa hadi kumaliza mkopo, Serikali itawarudishia fedha zao? Tutege masikio tena kumsikia Lowassa atalisemeaje hili.

TUMESIKIA!!! tatizo risiti zetu sisi tuliojisomesha wenyewe tumeshazipoteza!! Mimi nimeshapata BODA BODA ya Pili lakini IDADI YA WATU waliovyunjika Viuno na Miguuu kupitia Biashara yangu hii imefikia 10.... lakini sitoiacha!
 
Tanesco, nafahamu hili linasababishwa na serikali si wao nawaombea msamaha kwa Lowassa ila wakihakikishe nao wanazungumza wasibebeshwe zigo lisilo lao. Mfano madai wanayoidai serikali (Polisi, Magereza, Hospitali, Vyuo na taasisi zingine ni mengi sana) So, serikali iwalipe ili wafanye kazi kwa ufanisi zaidi.
 
Wasomi hatuna la kuzungumza zaidi ya kumpitisha LOWASSA kuwa Presidenttttttttttttttttttttttt
 
Sema ww msomi c wote! Nenda tumain uone lowassa anavyoonekana kichefuchefu.
 
Daaaaaaaah! Kesho mapema namsafirisha dogo kwenda mbeya akampe tako Mr edoo, Kama wachache wanaweza kuiba mapesa mengi kupitia, EPA, MEREMETA, TAN GOLD, ESCROW NA MA TEN % ZA KUTOSHA, Kwanini nisifurahie Nami kufaidi hata kidogo keki ya taifa langu?? Mungu ni mwema Sana

Duh! kweli watu mna mahaba na fisadi Lowasa!
 
Kama watu watasamehewa na wengine watasoma bure kabisa hata kule IMTU na St. Francis tutapiga bure kwa mujibu wa mh. sasa tatizo liko wapi? mpeni kura ili tujimwage vyuoni
 
Sasa inabidi wanafunzi wote wa vyuo vikuu tuchangie safari ya EL Ikulu kwa kujitoa kwenda kupiga kura tar 25/10
 
Mzee Mwanakijiji tunahitaji episode ya 3.
Pia huku nilipo watu wanaandamana walalamika kuwa dakika 10 hazitoshi...kila episode iwe na zaidi ya dakika 50

Waambie kazi ya kuongea sana ni ya wasanii ili kukidhi hsm ya waliotoa kiingilio.Acha mama apigizane kelele na watoto ila baba ukifika amri moja kila mmoja anatafuta mlango wa kutokea.
 
Last edited by a moderator:
Shikamooo Lowassa, hakika wewe ndio rais tunayekuhitaji Tanzania
 
Kile kilio cha siku nyingi cha maumivu ya mkopo wa elimu ya juu kinakaribia kupatiwa jibu. Mgombea wa Urais wa CHADEMA/UKAWA Edward Lowassa ameahidi kuwasamehe wale wote waliokopeshwa na kodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB). Lowassa anamaanisha kuwa wanaodaiwa hawatalipa tena na itakuwa ni kama wamesomeshwa bure tu na Serikali yao.

Wakati huohuo, Lowassa anaendelea kusisitiza kuwa elimu ya chuo kikuu itakuwa bure. Wasomi wa wakati wa nyuma na wale wa sasa, mnataka nini tena? Lowassa, kutokana na ahadi zake za kiuchaguzi, anatamani kuona elimu inakuwa bure na hata wale waliokopeshwa wakijisikia kuwa wamesoma bure. Lengo kuu ni kutoa elimu ya bure na bora kwa maendeleo ya Tanzania yetu.

Mtampa kura wasomi wa Tanzania? Wale waliolipa hadi kumaliza mkopo, Serikali itawarudishia fedha zao? Tutege masikio tena kumsikia Lowassa atalisemeaje hili.

wewe na lowasa ficheni ujinga wenu msifikiri watanzania wote wapumbavu.hata kama unatafuta kura si kwa ulaghai kiasi hicho.funguka kama kweli wewe ni msomi usiwe mchumia tumbo.
 
Shit. Mi nimemalizia kulipa July mwaka huu. Naweza kuomba wakanirudishia milioni zangu 7?
 
Mungu mkubwa,asante Lowasa kwa kutukumbuka yale makato yanatesa sana.
 
Viva Edo Viva... Peperusha Benderaaaaa..!!
Tanzania Mpya inakuja very sooon!
 
Ulitaka tutongozwe kwa push ups? Lowasa mabadiliko.....

icon1.png
:lock1::lock1::lock1::lock1::lock1:
 
Hii habari italeta mgogoro kati ya vyuo binafsi na wanafunzi/wazazi.

Pamoja na kupewa mkopo pesa haziji kwa wakati sasa hizi ruzuku za chuo sijui zitafika vyuoni lini?

Kumbuka vyuo vinafunguliwa tarehe 2 november sidhani hata Lowasa atakuwa ameshaapishwa, na ratiba za semester zitabaki palepale.
 
Kile kilio cha siku nyingi cha maumivu ya mkopo wa elimu ya juu kinakaribia kupatiwa jibu. Mgombea wa Urais wa CHADEMA/UKAWA Edward Lowassa ameahidi kuwasamehe wale wote waliokopeshwa na kodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB). Lowassa anamaanisha kuwa wanaodaiwa hawatalipa tena na itakuwa ni kama wamesomeshwa bure tu na Serikali yao.

Wakati huohuo, Lowassa anaendelea kusisitiza kuwa elimu ya chuo kikuu itakuwa bure. Wasomi wa wakati wa nyuma na wale wa sasa, mnataka nini tena? Lowassa, kutokana na ahadi zake za kiuchaguzi, anatamani kuona elimu inakuwa bure na hata wale waliokopeshwa wakijisikia kuwa wamesoma bure. Lengo kuu ni kutoa elimu ya bure na bora kwa maendeleo ya Tanzania yetu.

Mtampa kura wasomi wa Tanzania? Wale waliolipa hadi kumaliza mkopo, Serikali itawarudishia fedha zao? Tutege masikio tena kumsikia Lowassa atalisemeaje hili.

petro, unachosema ni sahihi kabisa, kwanza pesa wanazokopeshwa wanafunzi zinatoka hazina na ni yale makusanyo ya kodi,

marejesho yote huenda hazina na hayaeleweki yanatumikaje? Inawezekana haya marejesho watu wanalipana posho za safari tu.

Hapa HESLB igeuzwe iwe provision fund tu, mtu akitaka kupeleka mwanae feza boys au shabarn robert akakope huko na sio kunyanyasa watoto wa masikini.
 
Back
Top Bottom