Wasioamini uwepo wa Mungu watazidi kuongezeka

Wasioamini uwepo wa Mungu watazidi kuongezeka

Hili ndio niliolokuwa nikiwaambia watu mtaani.

Kama kila mtu anaona hali ya nchi ilivyokuwa mbaya na kutamani kuona walau mtu yeyote anajitokeza wa kutuokoa hapo tulipo lakini kila tumaini linaloonekana kututia nguvu linazimika kama mshumaa na kuwapa ushindi watesi wanaozidi kutukandamiza kupitia nguvu ya madaraka.

Halafu hapo hapo unawaza eti kuna stori za Mungu muweza wa yote, mwenye upendo wote, yupo kila sehemu, Mungu huyo anayaona haya yote lakini hachukui hatua yeyote zaidi zaidi tunaona watu wema ndio wanazidi kuwa wahanga na kuwindwa kama kuku na kuuliwa halafu Mungu ni kama haya yanayofanyika anayachukulia kama sinema inayomfurahisha.

Kisha watu hao ambao ni wahanga ikifika ijumaa, jumamosi na jumapili wanaenda kumtolea sadaka Mungu huyu eti wanashukuru kwa yote. Huu ni ujinga tena ujinga wa kiwango cha juu sana.

Haiwezekani jambo ambalo katika maono tu ya kiutu tunaona halifai lakini eti tunaamua kujipa upofu wa fikra wa kutoona tatizo kwenye hii dhana ya Mungu mwenye upendo wote na nguvu zote ya kuepusha haya mabalaa, akayaacha tu yatendeke na kwamba hastahili lawama kwasababu ni perfect being.

Mungu huyu hastahili kabisa kupewa sifa hizo kwasababu ni miongoni mwa sadist.
 
Na hata wanamtandao wanajua tumefungwa kwenye fikra za Mungu kwahiyo hatutawafanya chochote
 
Mnataka kumuona Mungu? Muwe watu wa Rohoni ndio mtamuona. Mungu ni Roho, nao wamuabudiye inawapasa wamuabudu katika roho na kweli.
 
Wengi hawana Elimu sahihi kuhusu Mwenyezi Mungu, utukufu wake , sifa zake nk ndio maana wanaongea negatively kuhusu Mungu. Mimi hapa nafafanua kidogo kuhusu Mwenyezi Mungu kutoka na mafundisho ya dini ya Uislamu

Lawama inakuja kwa kutofanya uadilifu au kwenda kinyume na alivyoahidi . Mfano Mwenyezi Mungu aseme watu peponi hakuna shida Wala dhiki halafu mtu aende peponi akute dhiki na tabu hapo tunaweza kusema amekosa uadilifu kitu ambacho halipo kwa Mwenyezi Mungu kutokuwa muadilifu na mkweli katika ahadi.

Mwenyewezi Mungu ametangaza Zamani kwenye maandiko kuwa Dunia ni kama sehemu ya dhiki , watu kufanyiana uasi , kuuana nk . Na kwa waumini wanaomcha yeye ndio Wenye kupata mitihani zaidi. Pamoja na hilo akaahidi kuwanusuru wataofuta na kushikama na muongozo wake kisawasawa pamoja na kuwaandalia mwisho mwema yaani pepo.

Kanuni ya Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa Uislamu ametaka watu wasijiingize kwenye matatizo na katika kila jambo wajiandae ,kuchukua tahadhari na kufanya hatua muhimu (sababu ) ili kupata au kulifikia na sio kisa una Imani ukae tu kizembe Hilo swala halipo hayo sio maelekezo yake.

Na kuwa mjuzi wa yote sio hoja maana yeye anafanya atakalo na kuruhusu atayotaka kufanyika kutokana na hekima yake na ujuzi wake mabaya na mazuri yote yanatokea .
images (11).jpeg
 
Kwa hiyo Polepole yamemfika hayo yaliyomfika coz alikua anaamini kwa Mungu?

Kwahiyo asingeamini Mungu yasingemfika hayo yaliyomfika?

Kwahiyo wale wasioamini Mungu,wao hua hawapati matatizo?

Kama huamini uwepo wa Mungu,kwanini uamini kua Polepole kakamatwa coz alimuamini Mungu?
 
Back
Top Bottom