Ujinga wa waamini ndio ulizaa jina la "Atheists"

Ujinga wa waamini ndio ulizaa jina la "Atheists"

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
62,709
Reaction score
105,316
Japo wasioamini mungu hukubali tu kuitwa atheists (wasioamini mungu) ila kiuhalisia ni ujinga tu wa binadamu ndio ulipelekea kuwepo hili jina au hii lebo.

Jiulize kwa nini hakuna watu wenye lebo maalumu au wanaitwa wakataa/ wasioamini uchawi, wasioami spiderman, wasioamini uwepo wa sungura wanaoongea, wasioamini uwepo wa aliens, wasioamini uwepo wa paka wa bluu n.k ila wasioamini mungu wamepewa jina/ label maalumu kabisa wanaitwa "atheists".
 
Wanaoamini Mungu wanachukulia hali yao ya kuamini kuwa ni uhalisia wa mambo na ya umuhimu sana , hivyo asiye amini hayo mambo huwa ni jambo la kushangaza ndio maana kukazaliwa hilo jina
 
Mjinga hawezi kufahamu kuwa yeye ni mjinga pasipo kuambiwa ujinga anaoufanya.
 
Atheists bongo hawazidi hata 10 ,ila wanaleta msongo wa mawazo kwa theists mamilioni, angalia hata humu jf
Nafikiri wako wako kadhaa bwashee sema ndio hivyo inabidi waishi kwenye closet kama mashoga😁
Kuna siku nilipanda dalaladala dereva akaweka audio clip ya jamaa fulani wanaitwa wachokonozi wanahoji mambo ya mungu na dini kawaida tu, hali ilichafuka kwenye dalaladala utulivu ukakosekana kabisa.
 
Nafikiri wako wengi bwashee sema ndio hivyo inabidi waishi kwenye closet kama mashoga😁
Kuna siku nilipanda dalaladala dereva akawepa audio clip ya jamaa fulani wanaitwa wachokonozi wanahoji mambo ya mungu na dini kawaida tu, hali ilichafuka kwenye dalaladala utulivu ukakosekana kabisa.
Sifikiri kama wapo wengi, wengi waliopo , ni Agnostic, na wanafki wa imani tu
 
Agnostic kama sub ya Atheist tu iliyo bench, au kama bia na konyagi.
Wengi wapo hivyo na hawajijui , ukiwabana na maswali ya uwepo wa Mungu wana anza kuhoji kama Agnostic ,wachunguze vizuri, utagundua kitu
 
Back
Top Bottom