ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,529
- 21,530
Kumekuwa na ujinga mwingi sana wa watu ambao hawajui chochote kuhusu Uislamu na kuwa kimbelembele kutoa majibu ya Uislamu,ikiwa wao tu hawajui imani yao vizuri kumjua yupi ni Mungu na yupi ni nabii/mtume ndio wataweza kweli kuujua Uislamu?
Nimepitia post kadhaa kuhusiana na mwandamo wa mwezi,wengi ambao sio waislamu ndio wa kwanza kuiponda Bakwata kwamba ni chombo sijui cha Ccm au sijui cha Serikali,huu ujinga mmeutoa wapi?
Yani kwakuwa tu sikukuu haikuangukia Ijumaa basi ujinga wenu,upuuzi wenu wote mnaulekeza kwa Bakwata, je mnajua kuhusu elimu ya figh ya dini ya kiislamu?
Kama hamjui sasa mnapata wapi gut za kuzungumzia kitu ambacho hamkijui? Yani sawa sawa na Mimi leo kobazi nizungumzie kuhusu Naziri wanazo weka makatekitsi au mafaza au mabraza,though nilipata elimu kidogo kuhusu hili lakini sina gut ya kueleza kama wakatoliki wenyewe
Uislamu katika elimu ya figh/ Sheria ya dini kuhusiana na ibada mbali mbali,inasema kuelekeza njia mbili ambazo waislamu wanaweza kufunga au kufungua kutokana na muandamo wa mwezi
Kuna ile mkiona mwezi fungeni na ukionekana mwezi fungeni. Na hiyo ya kuona kutokana na zone ya nchi husika au ukanda husika ndio ambayo imekuwa ikitumika karne na karne,sasa Leo hii Bakwata wakitumia njia hiyo ndio mnawaona vibaraka wa CCM au Serikali?
Stay away from our business!!!
Ni hayo tu!