Yule mdada yupo sawa kabisa ,na anaeona kuwa ametukana huyo atakuwa hana akili vizuri na anashindwa kupambanua au ni mgonjwa wa akili bila ya yeye mwenyewe kujua ,tatizo wazimu upo wa aina nyingi ,ulizeni wanaosomea elimu ya uwenda wazimu ,ndio maana huwa sina tatizo na baadhi ya watu wanavyojibu,inabidi tuwachukulie tu.
Hivi kama yule dada ametoa matusi ni wapi ,nimesikiliza marambili tatu sijaona matusi ,au pale aliposema kuwa yeye anatokea mtaa wa Nyerere ? Na wasikilizaji kujibu Lanatullah . Na si nyerere tu anaesemwa hivyo linapotajwa jina lake ,hata Mkapa na hata Ali Hassan Mwinyi pindipo yatajwapo majina yao WaZanzibar hawasiti kusema lanatuLLAH ,wacha hiyo mikutano ya uamsho ,kwenye mikutano ya CUF misemo ni huohuo ,mnaogopa ?
Yule mwanamke ni shujaa sana na si aibu wa dhambi ,msije na elimu zenu za mashehe ubwabwa mkataka kutia watu makosani ,sijui mumewe,kaka yke baba yake ,ni bora mkakaa kimya.