Wasikilize, lakini usipokee ushauri wa wanawake kuhusu wanawake

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Wanawake ni wazoefu wa kuwa wanawake lakini hawana uzoefu juu ya jinsi ya kumvutia na kumtunza mwanamke mwingine kimapenzi. Asilimia kubwa ya wanawake hawajui kitu haswa kinachomvutia kwa mwanaume aliyenaye, ni wachache wanaoweza kuweka hisia zao kwenye maneno yanayoeleweka.

Japo unaweza kuwasikiliza kupata maoni yao. Lakini ujue ushauri wanaotoa kwa wanaume ndio huo mara nyingi wanawapa wanawake wenzao, “kuwa na subira/ mvumilivu”, “mtu sahihi atakuja tu” au “muda sahihi ukifika utampata wako” au “muoneshe hisia zako”, mashauri haya mara nyingi yanafanya kazi kwa wanawake sio wanaume, na ukifanya hivyo utaishia kuwakera na kupotezewa na wanawake.

Wakati bado nahangaika kuwaelewa wanawake, kuna mdada mmoja tulikutana kwenye daladala tukabadilishana namba, nikamtongoza ikatiki. Sasa kilichokua kinanipa shida ni kwamba alikua ananipotezea sana, mpaka ajisikie ndo ananitafuta.

Siku moja nikaamua nimuulize rafiki yangu mmoja wa kike “Mbona huyu msichana ananipotezea sana? Wakati mimi najitahidi kumtunza?” Akaniambia “We wala usijali chuo kina mambo mengi labda masomo yamembana, au labda amepatwa na shida, akiwa na nafasi atakutafuta.”

Nikamjibu, “Lakini hata mimi nina masomo na mambo mengine lakini bado natenga muda kwa ajili yake.” Naye akanijibu “Mh, labda inawezekana anaogopa kupenda haraka baada mahusiano yake yaliyopita.” Hapo nikaelewa nikamjibu, “Labda, kweli acha na mimi nimpe muda apoe poe.” Nikikumbuka najiona nlikua hamna kitu.

Hapo utaona kwamba huyo rafiki yangu alikua anajaribu kunipooza na kunifanya nijisikie vizuri (amani) kutokana na kupotezewa. Alikua anajaribu kunipa moyo ili asiumize hisia zangu zaidi akinipa ukweli. Ukweli ulikua rahisi tu, huyo mwanamke hakukubali sana, au umekua dhaifu mpaka amekushusha heshima. Lakini mwanamke hawezi kukuambia hivyo wazi, ni wachache wanaoweza kukupa makavu live.

Kwanini hawawezi kutuambia hivo? Wanaogopa kutuumiza. Wanawake wana hisia mara kumi zaidi yetu wanaume, hivyo akikwambia anahisi utaumia sana. Pia wanaogopa kukabili maswali yetu kama “Kwani mi sifai? Kwani kuna shida gani akiwa na mimi? Sasa kwanini asinipende mtu kama mimi?”

Maswali haya huwa yana majibu machungu hivyo watajaribu kuyakwepa ili wasikupe majibu machungu. Wanataka uwe na furaha lakini hawajui jinsi gani ya kukuelezea vizuri bila kuficha ficha mambo lakini sisi wanaume tunapenda mambo yawe wazi, rahisi na moja kwa moja.

Kama na wewe uliwahi jisemea ‘hawa ni wanawake watakuwa wanajua kuhusu wanawake, wanaweza kunisaidia kuwaelewa,’ ujue ulikosea maana mwanamke wa kawaida hawezi elezea kiundani kwanini yupo na mwanaume huyu na sio yule, hivyo katika kundi la infinite kiumeni utapata kujifunza na wanaume wengine jinsi ya kumvutia na kumtunza mwanamke unayetaka kujenga naye maisha.
 
Back
Top Bottom