Mzumbe walikuwepo wengi sana ambao wanazo za Pacific Western University ambacho ni chuo cha online na wala vyeti vyake havitambuliki katika academic world.
Kwa hiyo, sio kwamba wahadhiri wote sio wachakachuaji, wako kibao tu na hasa kwenye hivi vyuo binafsi vilivyoanzishwa. TCU huwa wanafuatilia sana wakati wa kusajiri chuo, baada ya hapo sina hakika kama huwa wanafuatilia tena.
Madudu ya PhD fake za Mzumbe ambako wengine walishapeana mpaka u-Profesa, ziligundulika wakati wa kui-transform Mzumbe from IDM to Mzumbe University.
Kwa nyongeza tu, hata TCU wanapoamua kukagua baadhi ya vyuo, wakuu wa academics kwenye hivyo vyuo huwa wanaficha majina ya baadhi ya wahadhiri kwa kuwa lazima waambatanishe CV na transcript zao ili kuona kama wana-meet minimum requirement za kuwa wahadhiri na ku-verify kama degree zao ni genuine au fake. Kuna uhuni mwingi sana unafanyika na unaweza kushangaa kuna vyuo haviweki wazi orodha ya wahadhiri wake kukwepa hayo madongo. Huko kwenye vyuo vya binafsi mpaka watu wenye bachelor za GPA ya 3.3 wanaibua ajira kama kawa. Tofauti na vyuo kama UD, Muhimbili na SUA ambako lazima uwe na angalau GPA ya 3.8.