Wasifu (CV) wa January Makamba

Mjinga wa kijijini si sawa na mjinga wa mjini, hali kadhalika mjinga ambaye hajavuka mpaka hata kwenda hapo malawi si sawa na mjinga aliyetoka hapa na kuishi ulaya au marekani, lakini wote wanakuwa na sifa moja tu UJINGA
 

Siasa tuache pembeni.

Hayo ya daraja sifuri kidato cha nne au cha sita hayana uhusiano wa moja kwa moja na maswala ya uongozi.

Profesa Abdoulaye Wade ambaye amepata kuwa rais wa Senegal ni moja ya marais wasomi wa Afrika waliowahi kushika nafasi hiyo pia Profesa Bingu wa Mutharika aliyetawala Malawi.Utawala wao haukuakisi uprofesa wao na kuleta matokeo chanya kwa maendeleo ya wananchi wa nchi zao.

Katika orodha hiyo, mfano mdogo hapa Tanzania kwa kutumia kipimo cha madaraja kwa kidato cha nne na sita, Dk. Cyril Chami, aliyepata kuwa Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko katika Awamu ya Nne,anatajwa kuwa moja ya wanafunzi bora kutokea nchini, Kidato cha Nne-Daraja la Kwanza Alama 7 (Div.I.7) na Kidato cha Sita-Daraja la Kwanza Alama 3(Div.I.3).Chuo Kikuu-First Class. Pamoja na matokeo yake hayo, wizara bado ilimshinda kuongoza.

Fundisho: Hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa maswala ya utawala na uwezo wa darasani.Isipokuwa elimu nzuri ya jumla inaweza kumsadia mtawala kuwa na upana wa uelewa wa ulimwengu unaomzunguka.

Busara.Hekima.Kuwajibika.Nidhamu.Kujitambua kwamba yeye ni mwajiriwa wa wapiga kura wake,hayo na mengine yanaweza kumfanya kuwa kiongozi bora.

Hitimisho:Januari Makamba au yeyote yule anaweza kufaa au asifae iwapo hatokuwa na maono katika nia yake ya kutaka kuwa rais wa nchi yetu tukufu.Wengine wanataka sifa tu, awe magogoni, kila kitu chake.Asafiri atakako,kwa kutaja machache. (Haya ni maoni yangu tu,sio msahafu huu!)
 

Boss. January Form six pale Forest Hill alipata Two ya 10.

Unaruhusiwa kumchukia mtu, huruhusiwi kumtungia maneno ya uongo.
 
Kama una ushahidi tuwekee, tuache kuendeleza mapambio ya mitaani yanayoibuliwa na kuenezwa na watu waliokosa hoja za ushindani.

Jamaa Kaandika hivi Kwenye Website yake (January Makamba)
"So, we did our exams – and the day to go and look for the result came. And, to the shock of friends and family and teachers, my name was not there in the results sheet. I felt like collapsing. I went to another result centre thinking that there was a mistake – again, nothing. Inquiries to the reasons were not responded to immediately. Later we learnt that I was mistakenly linked to a cheating scam that one of the teachers was involved in. I was a pawn in a terrible mistake. A really long and painful story. So, what was the alternative? To resit the exams. I quickly registered as private candidate and pursued High School studies at Forest Hill High School on a tentative basis while resitting – so that when I get my results I can proceed on to Form Six. It was such a task, but I succeeded"

Bado najiuliza, kama kweli alisingiziwa, kwa nini hakuruhisiwa kupewa majibu yake na badala yake akatafuta alternative?? Manake, kwa connections zile na kama kweli alikuwa ameonewa, sidhani kama majibu yake yasingetolewa, Tafakari!
 
Nilitaka kusoma reply Zote mpaka Mwisho lakini hii imenifanya niseme nijuavyo kuhusu January. Alimaliza kidato cha nne Forest hill sec school mwaka 1993 na alipata div 4, Forest ilikuwa inamitaala mingi ya comarce yeye alikuwa com 1 ambayo ndo waliwekwa walio vizuri class. Baada ya forest sijui alikwenda ila naamini a Rudia mitihani ya kidato cha nne kitu ambacho ni kawaida sana kwa mtu asiye kata Tamaa kutimiza malengo yake ya maisha. Naamini hata Hapa JF kunawengi wamerudia mitihani kwa kutoridhika na elimu ya kidato cha nne. Kwalolote alilofanya hakupenda kubaki na elimu ya kidato cha nne. Kwahiyo ukweli ni kwamba January hakupata div 0 kwenye sitting yake ya kwanza Bali ni div 4, maelezo hapo juu ni sahihi Kama alipohamia Forest hill form 3 hakuwa amefanya mtihani shule nyingine
 
Yaani kuwa secretary wa rais tu na yeye anataka kuwa rais.jimbo lenyewe limemshinda analiongoza kwa twiter nchi si ataiongoza kwa instagram!

Eti anaropoka "Upinzani hakuna mwenye sura ya urais". Simcard imemshinda ataweza kukabiliana na mikataba ya Nyuklia?Ushamba tu.

By the way,huwezi kusomea shahada ya conflict resolution kama una akili timamu.Je,Migogoro ikiisha utafanya nini?Utafitini na kuomba watu wagombane?Ndiyo future hii?Je,taaluma hii isingesaidia usuluhishi na mzee shelukindo huko Bumbuli?Conflict haihitaji digrii bali busara na kujitambua tu.Kwani wafalme wetu miaka ya zamani waliwezaje kutatua migogoro?Only,Weak Creatures watafanya promotion ya taaluma hii na kujisifia kwa vyeti na majoho.
 

cc Radhia
 
Hata mtoto wa jk Alipata zero, usidhani kuwa mtoto wa rais ndo kuwa na akili kichwani wakati mama yake alifeli kwenda sec na kuambulia kuwa mwl wa upe kawe shule ya msingi??
Hujui hata baba yake ana pass ya economics Udsm?
Ukishindwa shule na ukashindwa kuiba mtihani unadhani utaweza nini?
 

Bumbuli Development Corporation
 
Mkuu wewe mwenyewe umekiri kuwa unamfagilia lakini kusikia ati kapata division zero unaonekana kuhoji tena uwezo wake! Usingepata hiyo habari basi ungeendelea kumkubali? Kama ni ufaulu wa darasani basi nchi zingekuwa zinaongozwa na maprofessor.

Siasa za Tanzania hata uwe Prof unapoingia kwenye uongozi hasa bungeni wengi wanakuwa kama std 7 tu
 

Dr Cyril Chami hakushindwa mkuu ni siasa tu......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…