Wasichana na promo za "nasoma chuo"

Wasichana na promo za "nasoma chuo"

Yaan unakuta wa hivyo anakutajia bei kuanzia unywele hadi miguuni ili tu umuone wa gharama. Bahatika sasa kuona anapolala utamuonea huruma.
Huo unakuaga ulimbukeni wapo wengi unakuta hata msichana kanunua hand bag sasa hakuna anae muuliza basi ye anaanza huu mkoba nimenunua laki mbili hiki kiatu nimenunua elfu tisini hujaulizwa. ULIMBUKENI HUO watu wamepanda wamenza kupanda ndege hawana hata meno mdomoni, wanatembelea magari wako kimya.
 
Atakua anasoma certificate of diploma in bachelor degree of o level studies.
[emoji23][emoji23] imetofautiana kidoooogo na course nayo chukua ya bachelor degree in diploma and certificate management... sema yeye yupo certificate! [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu nikazuri ajabu kweli Mungu hakupi vyote! Nilitamani nioe kabisa shida katanivurugia watoto.
Kwa hiyo ulikuwa na watoto tayari,au una mke lakini unataka kukaoa hako kabinti?Atakuharibia watoto atakao wakuta kwa mke wako wa sasa au atakao wazaa yeye atawaharibu?kivipi?Au kuna watoto uliozaa nje ya ndoa utakapowaleta yeye akiwa tayari mkeo atawaharibu?Ni mchawi/mchirikina?Ni kicheche unaogopa wanao pia watarithi tabia ya mama yao?Eleza upate ushauri kwani inaonekana kiumri u mkubwa lakini kiakili unatakiwa ukomazwe na magwiji wenye uzoefu wa maisha. KARIBU TENA BAADAE KWA MREJESHO.
 
Watu kama nyie ndio huwa mnaangukia pabaya kwa kufuru na dharau zenu eti "katanivurugia watoto"

Cha ajabu hizo degree zake mbili bado life linamgonga, jamaa limbukeni la elimu msamehe bure
 
[emoji23][emoji23] imetofautiana kidoooogo na course nayo chukua ya bachelor degree in diploma and certificate management... sema yeye yupo certificate! [emoji23][emoji23][emoji23]
ha ha ha ha hyo lazma mtofautiane mkuu kama yeye anasoma zile course za engineering in human resource of business management
 
Cha ajabu hizo degree zake mbili bado life linamgonga, jamaa limbukeni la elimu msamehe bure
Tena si ajabu kibinti kilimtolea nje pamoja na usomi wake [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Kwa hiyo ulikuwa na watoto tayari,au una mke lakini unataka kukaoa hako kabinti?Atakuharibia watoto atakao wakuta kwa mke wako wa sasa au atakao wazaa yeye atawaharibu?kivipi?Au kuna watoto uliozaa nje ya ndoa utakapowaleta yeye akiwa tayari mkeo atawaharibu?Ni mchawi/mchirikina?Ni kicheche unaogopa wanao pia watarithi tabia ya mama yao?Eleza upate ushauri kwani inaonekana kiumri u mkubwa lakini kiakili unatakiwa ukomazwe na magwiji wenye uzoefu wa maisha. KARIBU TENA BAADAE KWA MREJESHO.
Mkuu hizo degrii mbili nilizobeba sikupewa bure jamaaa yangu!

Psychologically intelligence ya mtoto iko likely inherited kwa mama kuliko baba. Ukiwa na mke kilaza watoto wako na hatihati ya kuwa km mama yao zaidi kuliko baba. Fuatilia tafiti kichwani hakako vizuri kiivyo.

Kuhusu kukaoa nilisha badiri gia angani kilichobaki nakahurumia kukalalua tu basi.
 
Kuna kidada kimoja kimoja nilikutana nacho, kikajifanya kinasoma UDSM na kinawahi kwenda kufanya eti "reseach"

Nikamwuliza yupo college gani alitoa macho kama kabanwa na mlango
 
Kusema ukweli nako kuna risk


Nina rafiki yangu wakati yuko chuo, alikuwa akiulizwa elimu anajidai yeye darasa la saba hata akiombwa namba anaziandika kwa mkono wa kushoto ili mwandiko uwe mbaya (ye anatumia mkono wa kulia) basi mkaka akiona hivyo anasepa tu... Wote walikuwa wanapeperuka na alikuwa hasumbuliwi
 
In short,
Nilikuwa naenda chuo fulani, nimetoka zangu home nikiendesha kikorola changu. Njiani nikamkuta dada mmoja anasubiri usafiri wa public. Aliponiona basi akanipungia kuomba lift, nikampakia. Tukawa tunaongea machache kupiga stori na kufahamiana. Nilipokaribia mjini, nikamwuliza anakoelekea ili nijue namwacha wapi au anaenda ninapoenda. Akasema anasoma chuo X ambacho ndo huko huko mimi naenda. Nikamwuliza unasoma pale? akasema ndiyo, nikamwuliza mwaka wa ngapi? akasema mwaka wa kwanza. Nikamwuliza unasoma kozi gani? akasema education. Nikamwuliza unasoma masomo yapi ya kufundishia (teaching subject)? Akanitajia.

Jambo asilolijua mimi nimefanya kazi, na ninaendelea kufanya kazi hapo chuoni kama part time sijawahi kusikia somo mojawapo kati ya hayo masomo aliyotaja. Akili ikanituma kuwa huyu anajipa promo, bila shaka hasomi chuo. Tukaendelea na safari yetu. Nikanyoosha moja kwa moja hadi geti la chuoni, akaniuliza, kwani wewe unaenda wapi? Nikamwambia naenda hapo chuoni pia. Akauliza unasoma au unafanya kazi, nikasema nafanya kazi. Tulipofika tu getini, akaniambia nimwache hapo getini anapitia assignment aliacha stationary jana yake. Nikasema poa, basi nikamwomba namba, lengo langu likiwa kujua hatima ya uongo wake.

Baadaye mchana na jioni tukawa tunapeana hi, akawa ananichangamkia sana usipime. Mimi nikawa napeleka mada za chuo na hayo masomo anayosoma. Mwishowe akaumbuka, na kukiri kuwa yeye hasomi chuo buana. Kumbe yuko anasugua tako kureseat huko kwenye tuition centres. Alivyosema ukweli wake nikamwambia mbona hilo somo umetaja halipo hapo chuoni? ikawa mwisho wa mawasiliano.

Enyi wadada, muwe wakweli jamani. kwani kuna haja gani ya kudanganya? wee kama muuza genge sema tu unauza genge.
Nawe nae? Si ungemnaniliu tu badala ya kumuumbua?
 
Uwiiiiii hii mambo ni across the world, na wewe mrembo ulonidanganya unasoma chuo unatoka asubuh unarud jion kumbe unafanya kazi ya usafi kampuni fulani huu uzi unakuhusu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] duh
 
Back
Top Bottom