KIUNGOMCHEZESHAJI
Senior Member
- Oct 4, 2013
- 120
- 254
In short,
Nilikuwa naenda chuo fulani, nimetoka zangu home nikiendesha kikorola changu. Njiani nikamkuta dada mmoja anasubiri usafiri wa public. Aliponiona basi akanipungia kuomba lift, nikampakia. Tukawa tunaongea machache kupiga stori na kufahamiana. Nilipokaribia mjini, nikamwuliza anakoelekea ili nijue namwacha wapi au anaenda ninapoenda. Akasema anasoma chuo X ambacho ndo huko huko mimi naenda. Nikamwuliza unasoma pale? akasema ndiyo, nikamwuliza mwaka wa ngapi? akasema mwaka wa kwanza. Nikamwuliza unasoma kozi gani? akasema education. Nikamwuliza unasoma masomo yapi ya kufundishia (teaching subject)? Akanitajia.
Jambo asilolijua mimi nimefanya kazi, na ninaendelea kufanya kazi hapo chuoni kama part time sijawahi kusikia somo mojawapo kati ya hayo masomo aliyotaja. Akili ikanituma kuwa huyu anajipa promo, bila shaka hasomi chuo. Tukaendelea na safari yetu. Nikanyoosha moja kwa moja hadi geti la chuoni, akaniuliza, kwani wewe unaenda wapi? Nikamwambia naenda hapo chuoni pia. Akauliza unasoma au unafanya kazi, nikasema nafanya kazi. Tulipofika tu getini, akaniambia nimwache hapo getini anapitia assignment aliacha stationary jana yake. Nikasema poa, basi nikamwomba namba, lengo langu likiwa kujua hatima ya uongo wake.
Baadaye mchana na jioni tukawa tunapeana hi, akawa ananichangamkia sana usipime. Mimi nikawa napeleka mada za chuo na hayo masomo anayosoma. Mwishowe akaumbuka, na kukiri kuwa yeye hasomi chuo buana. Kumbe yuko anasugua tako kureseat huko kwenye tuition centres. Alivyosema ukweli wake nikamwambia mbona hilo somo umetaja halipo hapo chuoni? ikawa mwisho wa mawasiliano.
Enyi wadada, muwe wakweli jamani. kwani kuna haja gani ya kudanganya? wee kama muuza genge sema tu unauza genge.