Sam,
Naona umesoma mchango wangu kwa hasira, kwani kwa kawaida huwa una michango iliyoandaliwa vizuri sana.
Umeandika: Kwanza naomba usipotoshe wanabodi, there is no such a thing "lapsed Christians", there is "lapsed Catholic".
Mtu yoyote aliyekuwa anamfuasa Kristu na sasa ameacha, ni lapsed Christian. Wako, tena wengi tu. All practicing Catholics are Christians, but there are many Christians who are not Catholic. You need not agree with this, but it is true nonetheless.
Umeandika: Catholic does not means christians. Give me a Break!
Bila shaka umekasirika ndio maana ukadhani kuna mtu amesema Catholic means Christian. We are slightly better informed than that.
Umeandika: Na mkristo siyo mtu anayemfuata Yesu tu, Mkristo ni mtu anayefuata mafundisho ya Yesu.
Sikusema Mkristu ni mtu anayemfuata Yesu. Nimesema Mkristu ni mtu anayemfuasa Yesu. Naamini unaelewa tofauti iliyopo. Amfuate Yesu wapi? Anamfuasa.
Umeandika: Nashangaa unawatetea viongozi wa kanisa, there are just human beings for GOD sake. I am sorry, I hate them like a morning "sheet metal".
Unamfuasa Yesu kweli? Kumbuka alisema kwamba tutawatambua wafuasi wake kutokana na upendo wao. Do not judge (Yesu alikataza). Huna haki kusema viongozi wa Kanisa wana dhambi na wewe huna.
Kanisa unalolishutumu linaongozwa na Yesu mwenyewe, kwa hivyo usihangake kulidhoofisha kwani hutaweza. Kama lina wadhambi, basi kwa vile wewe huna dhambi basi chukia dhambi yao, lakini usiwachukie wenyewe. Au utatenda dhambi kubwa kabisa.
Umeandika: Pamoja na discussion lote hili nashangaa hujui maana ya serikali. Unaposema Serikali haina dini ila watu ndiyo wana dini, hivi naomba nieleweshe vizuri wewe una define vipi serikali.
Serikali huundwa na watu. Serikali sio watu; ni umoja wa taasisi zinazoundwa na watu kwa ajili ya utawala. Kwa sasa, vingozi wa CCM ndio wameunda serikali yetu. Binadamu wameumbwa, na baadaye wakaunda serikali. Ni binadamu tu ndiye anaweza kuwa na dini. Viumbe wengine, na taasisi zote, haziwezi kuwa na dini. Zinaweza kuwa chini ya dini, lakini hazina uwezo wa kuwa na dini.
Imebidi nikujibu. Naelewa tuko nje ya mada, lakini mambo uliyoyaleta yalihitaji kujibiwa.
Nawaomba wachangiaji msiopendezwa na huu mchepuko mtuvumilie. Huenda tukaweza kurudi kwenye mada sasa.
Augustine Moshi