Washushwa kwenye basi uchi uchi!

Washushwa kwenye basi uchi uchi!

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,085
Reaction score
34,871
Majambazi saba wakiwa na mashine za ukweli (bunduki), wameteka basi na kupora mali na fedha...huku wakiwashusha abiria hao mmoja mmoja na kuwaamuru kusaula viwalo na kubaki kama walivyozaliwa.

Katika songombingo hilo Suka (Dereva) wa basi hilo aliyejulikana kwa jina la Ahmed Hilali, alibandikwa risasi kichwani na kujeruhiwa ile kinoma.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Celina Kaluba amelitaja basi lililotekwa na majambazi hao kuwa ni mali ya kampuni ya Sunset ya mjini Singida na lilikuwa likitokea katika kijiji cha Iyumbu kwenda Singida Town.

Afande Kaluba amesema kabla ya kuliteka basi hilo, majambazi hayo yalifyatua risasi iliyovunja kioo kikubwa cha mbele kwa lengo la kulisimamisha...risasi ambayo ilimpata suka kichwani

Akifafanua Afande Kaluba alisema majambazi hayo yaliamuru abiria wote na wafanyakazi wa basi hilo kuteremka na kuvua nguo kabla ya kuanza kuwapora fedha na mali nyingine.

Hata hivyo mama mmoja alifanikiwa kuokoa fedha zake zaidi ya Sh. milioni 1.8, baada ya kufanikiwa kuzificha ndani ya basi, wakati wa purukushani ya kuteremka chini na kuvua nguo.
 
Are these Jokes or Nwes?
 
Duh, hivi huu ujambazi wa kuvuana nguo bado unaendelea mpaka zama hizi? Na hao wanaotembea na mahela mfukoni wanaishi karne ipi? Siku hizi kuna mabenki mpaka ya SACCOS wao bado tu wamo wanachimbia ela zao kwenye mkwiji..aaarrgghh
 
Guys be serious, is this a joke or real?
 
Are these Jokes or Nwes?

Mkuu sina hakika kama joke, ama real,
But i once heard, a true story, ambapo hao majanbazi baada ya kuwaamuru abilia washuke utupu, wali waamulu waanze kufanya mchezo mchafu live live, wakichagua tu randomly we njoo anza na huyu nawe wewe na yule hivo hvio, sasa eti akatokea jamaa mmoja yeye akawa hajapewa wa kudeal naye, akaona looo.. mbona nasahaulika,

akapaaza sauti kwa kunyoosha mkono kama darasani vile,eti mwizi ( ambaye ndo alikuwa bosi mpanga pair za libeneke ) na mimi bado.. akimaanisha nayeye apewe wa kudeal naye lol!
 
mh... harufu za pesa za mama zitasumbua vichwa vya mabaniani madukani, huh?
 
Mkuu sina hakika kama joke, ama real,
But i once heard, a true story, ambapo hao majanbazi baada ya kuwaamuru abilia washuke utupu, wali waamulu waanze kufanya mchezo mchafu live live, wakichagua tu randomly we njoo anza na huyu nawe wewe na yule hivo hvio, sasa eti akatokea jamaa mmoja yeye akawa hajapewa wa kudeal naye, akaona looo.. mbona nasahaulika,

akapaaza sauti kwa kunyoosha mkono kama darasani vile,eti mwizi ( ambaye ndo alikuwa bosi mpanga pair za libeneke ) na mimi bado.. akimaanisha nayeye apewe wa kudeal naye lol!

...Lol! ha ha haaaa 😀😀😀 acheni masikhara nyie ha haaaa..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom