Je, wajua kuwa kuna migahawa ambayo sharti la kuhudumiwa ni lazima uwe uchi kama walivyozaliwa?

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,527
14,399
Mgahawa wa Kwanza kabisa Duniani wa Vinywaji na Chakula Unaoruhusu wateja wake kupata huduma ya Chakula na Vinywaji wakiwa uchi Kama walivyozaliwa ni Mgahawa wa The Bunyadi. Wahenga wanasema Kua uyaona, na ukistaajabu ya Musa ya Firauni hayataiupita mbali.

Huu ni mgahawa wa aina yake uliokuwepo Miaka Minne Nyuma Mjini London Nchini Uingereza ambapo wateja wake wote wanaoingia kula na kunywa humo wanakuwa uchi wa mnyama kama walivyozaliwa. Inashangaza ndio.

Mmiliki wa mgahawa huu wa The Bunyadi Sebastian Lyall alisema kuwa siku chache tuu baada ya kuufungua June 2016, zaidi ya watu 45,000 walikuwa wamesha weka oda ya kusubiri kupata Huduma adhimu ya Chakula na Vinywaji hapo wakiwa uchi wa myama hata kabla mgahawa wenyewe haujakamilika na kuanza kutoa huduma.

Licha ya kwamba watu wengi sana waliuponda uamuzi wake wa kuanzisha mgahawa huo wa watu kuingia na kula wakiwa uchi, lakini wakati akiongea na wanahabari Sebastian alisema kuwa mtu kukaa bila nguo ni asili yetu, anapoingia kulala usiku huvua nguo, anapoenda ufukweni kuogelea huvua nguo, sasa iweje kuvua nguo unapoingia mgahawani hapo iwe ajabu?

Ilikuwa ukishafika tuu mgahawani hapo unaelekezwa na walinzi katika chumba maalumu ambako unaenda kuacha nguo zako zote huko na kubaki Kama ulivyozaliwa, kisha ndipo unarudi kuagiza chakula ukiwa hauna nguo yoyote hivyo hivyo. Unaweza kuchagua kukaa sehemu yenye taa za rangi, au ukaamua kukaa sehemu yenye taa za kawaida ukiwa na wateja wengine wengi walio uchi pia.

Ukiwa ndani ya mgahawa huu wa ajabu ni marufuku kuwa na simu, ni marufuku kuwa na Camera, ni marufuku kupiga picha kwa Vifaa kingine chochote, Vifaa vyote utakavyoingia navyo utaviacha katika sehemu maalumu ambako huko kutakua na walinzi madhubuti wa kulinda Mali zako. Bei ya chakula katika mgahawa huu ilikuwa inafika hadi Shilingi 200,000/= za Kitanzania Kwa Mlo mmoja Pekee.

Mwanzilishi Sebastian alisema kuwa Banyadi ni neno la kihindi lenye maana ya msingi au asili Huku akijinadi kwamba Asili ya binadamu ni kukaa Bila nguo, kwahivyo haoni Kama ni ajabu kufungua mgahawa wa Uchi ambapo watu wote Wanalazimika Kupata Huduma wakiwa Uchi wa Mnyama.

Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa mgahawa huo wa thebunyadi.com mgahawa huu ulifungwa, Hautoi Tena Huduma tangu Augost 12, 2016 Ikiwa ni Baada ya miezi miwili tuu tangu ufunguliwe huku kukiwa na zaidi ya oda za zaidi ya watu 46,000 zimebaki Wakisubiri Foleni ya Kupangiwa Tarehe ya kupata chakula hapo Kutokana na wateja kuwa wengi sana. taarifa zinasema kwamba Sebastian Aliamua Kuufunga Mgahawa huo ili kuutanua zaidi kwakua ulionekana kuzidiwa na idadi kubwa sana ya Wateja.

Sebastian alisema Kuwa Watu waliupenda sana Mgahawa huo, Walipenda sana Huduma za Mgahawa huo, Alisema London ni tofauti na maeneo mengine Mengi ya Dunia, watu wamekuwa wakisafiri kutoka sehemu mbalimbali kuja kupata huduma hapo, wameufurahia mgahawa, wanafurahia kukaa sehemu ambayo hakuna mtu anayeweza kukuhukumu kwa jinsi unavyoonekana.

Mgahawa huo uliokuwa na uwezo wa kuhudumia wateja 42 tuu kwa pamoja ulizinduliwa rasmi Juni 11, 2016 lakini Kuonyesha kwamba watu wengi waliufurahia, hata kabla ya kufunguliwa ulikuwa umeshapokea oda za zaidi ya watu 45,000 waliokuwa wakisubiri huduma hiyo ya Chakula Bila mavazi pindi tuu utakapofunguliwa.

Augost 12, 2016 Sebastian alisema kuwa ameamua kuufunga mgahawa huo huku akiwa na oda za zaidi ya watu 25,000 mkononi, alisema anafunga kwakua mgahawa wake ulikuwa ni Mdogo kuweza kukidhi mahitaji makubwa ya wateja wake, alikuahidi kurudi tena na huduma hiyo itakayokuwa kubwa zaidi na kuhudumia watu wengi.

Kama ulidhani kwamba huo ndio mgahawa pekee wa uchi Duniani na hakuna mwingine Basi utakua umekosea, November 2017 Mtandao maarufu Duniani wa Forbes uliripoti kuwa Mgahawa kama huu wa watu kula wakiwa uchi kama walivyozaliwa ulikuwepo pia Jijini Paris nchini Ufaransa baada ya kufunguliwa mwaka 2016, lakini kwa bahati mbaya ulifungwa na kutotoa Tena huduma miezi 15 tuu baadaye kwa madai ya kukosa wateja.

IMG_20231219_172745_399.jpg
 
View attachment 2847193
Sasa hapa kwenye hii picha uchi uko wapi?
 
Back
Top Bottom