Wasanii wetu na 'Uzalendo wa maslahi'

Wasanii wetu na 'Uzalendo wa maslahi'

Napata shida sana kuwaelewa Pro CCM unatakiwa na wewe uwe umechanganyikiwa, mnafiki au mwizi Ndio utawaelewa
 
wasanii wa kweli hawapo tena siku hizi tunashabikia shabikia tu usishangae siku kusikia wameitwa lunch au msosi wa jioni no way out elimu yetu ya shule za kata imetufikisha hapo.
 
Sisiemu inatambua kwamba Taifa bila vijana haliwezi fika popo, so wanawatumia wasanii kwa kuwashawishi vijana kwa kuamini wasanii wanakubalika na wanauwezo wa kuwashawishi vijana. Witowangu kwa vijana tuwe makini na hawa wasanii.
 
Bilicanas hakuwa nacho?



Alikuwa nacho...turudi kwenye mada wasanii watarudishaje uzalendo wakati tuliowapa kutuongoza nchi yetu..ndio wezi wakubwa na ni mizigo?hata kinana na nape ni mashahidi
angalia ziara zote za viongozi wa magamba
 
Watu mnahasira sana kweli inauma tumekuwa mazoba wa tz
 
Uzalendo hauhitaji promo wala kufundishwa, uzalendo unatoka moyoni wala hamna haja ya kukumbushwam
Nimejiskia vibaya sana baada ya kumuona Niki wa pili akilamba viatu vya kikwete kwa kuwakilisha kile anachokiita uzalendo.
Uzalendo hauhitaji kikao wala uhamasishaji.
 
Wanafiki wakubwa hawa, muangalie Mrisho mpoto, huwa anaimba nini na kule Mbeya kwenye sherehe za ccm alienda kufanya nini, unafiki tu huo, maneno yake ni tofauti na atendacho, ile ni program ya maccm, hakuna kitu hapo.
 
Uzalendo utaletwa na shilole kutingisha ----?au ule wimbo ziku hizi sipigi pulley
 
Nash mc, sugu ,jd, mapacha, wazee wa gahawa (wagosi) mbona siwaoni
 
Nikki wa ii kaelezea vizuri sn kuhusu uzalendo kwaivyo sio wote hawajui uzalendo na kaongea kw niaba ya wasanii ikumbukwe huyu ana master yk toka UDSM

WASANII WAPO WENGI anawakilisha wasanii gani. vp ROMA amesemaje kuhusu uzalendo.
 
Asilimia kubwa ya wasnii wa Tanzania ni wajinga wa kutupwa angalia hata move zao jinsi wanavyoongea au sikiliza nyimbo zao ni takataka tupu labda wachache kama vile afande Sele na profesa J.Wao ni vinara wa kutafuta pesa kwa njia yoyote ile ili watimize tamaa zao.Walio wengi wauza unga na yamkini wengine wakiandamwa na kashifa za ushoga na mengine machafu.Kwa ujumla ni wachumia tumbo.Kuhusu Clouds urafiki wao na sisiemu hauna shaka sikiliza watangazaji wae wanavyotumia nguvu kuitetea sisiemu! Shame on you!
 
Naomba kujua kama Roma Mkatoliki ,J.D na Kala Jeremiah walikwenda ili niache kusikiliza mziki rasmi!
Maana nimebakiwa na wachache
 
.........pengine wale ambao hawajafika katika viwanja hivyo huko Dodoma ndio wazalendo waliobakia....

Uko sahihi mkuu!, kama kina Proj J na Jide ndo wazalendo halisi.
nilishangaa kumuona mpaka Afande Sele! Kweli NJAA mbaya sana.
 
Tafsiri ya pro-Chadema ili uwe mzalendo lazima uwasifie Mbowe na Dr.Slaa.

Si kweli mkuu,usiwe na akili za dongo,zikimwagiwa maji zinamomonyoka,
Binafsi si mfuasi wa chama chochote,lkn maana ya uzalendo naitambua.
Haiwezekani ukajiita mzalendo wakati huwajibiki kwa Taifa lako..(kashfa nyingi za ufisadi wa mali na fedha za umma, i.e Epa,Escrow,Mifuko ya pembejeo n.k)na bila viongozi kuwajibika.
Haiwezekani mashuleni wanafunzi wakae chini alafu wewe msanii na raisi wako mwache kupiga kampeni ya utengenezaji na ununuaji wa madawati na bado ujiite mzalendo.
Haiwezekani gharama za chakula na nishati kuwa juu kila mwaka,programmu nyingi za maendeleo kutotekelezeka (i.e kilimo kwanza,mkukuta n.k) na bila ya viongozi kuwajibika halafu ukawatangazie wananchi uzalendo.

Nashindwa kuelewa kama hawa viongozi wenye dhamana kwenye mambo haya wanahitaji kuwa na Phd ndio waweze kuyaona haya au vip?
 
Back
Top Bottom