Wasanii wa Kizazi Kipya-Jiungeni Vita Dhidi Ya Ufisadi.

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,499
21,527
Ndugu zangu kipindi hiki ambapo tunaelekea kwenye msuguano wa hali ya juu kutokana na hali halisi ya mambo ya kisiasa ambayo Taifa letu changa linayapitia nimeonelea nizungumzie jambo moja.

Hivi sasa Mwana REGGAE WA JAMAICA..COCOTEA..Ametoa Kibao Safi sana cha kumfagilia Obama.

Na hili limetokea wakati Obama mwenyewe anatarajiwa kuanza ziara ya Dunia.

Misuguano ni mingi hata huko Ujerumani anakoelekea Yule mama wa ujerumani Berkell alitoa kijembe na inasemekana alitonywa na Bush wakati wakiwa huko kwenye G8.

Lakini Utawala wa Bush wamesema si kweli bali mama huyo kauli hiyo ni ya kwake binafsi.

Mahali hapo ni pa kihistoria huko Germany kwani ndio pale ambapo Reagan alitowa ile hotuba yake maarufu a GORBACHEV..TEAR THIS WALL DOWN...

Hotuba ambayo ndiyo maarufu kwa kutajwa kuwa ilikuwa ni Msumari wa mwisho kwa USSR Kutoka kwa mmarekani ambapo Reaggan binafsi anapewa crediti ya kuiangusha URUSI.

Na ndio mahali ambapo hata JFK mwenyewe alitoa hotuba ya ke maarufu.

Sasa kuna kama trend na waliposia Obama anakwenda huko ndio mama ambaye alikuwa na Bush huko Japan akatowa kauli hiyo ya kutotaka Obama apatumie mahali hapo pa kihistoria.

Tukiachana na mifano hiyo ya USA..Huko Bongo nakumbuka hata Dk Remmy mwenyewe alitowa kibao cha MREMA.

Ama kweli kilikuwa ni kipindi chenye mageuzi ya kisiasa kwani hata yule tajiri wa Arusha aliyepata madini mengi sana ya Tanzanite anayekwenda kwa jina la ASKOFU..

Alimpiga sana tafu Mrema lakini ccm walichukia na wakampangia njama na matokeo tunayaona kuanzia SAMAX walipopewa...Makaburu sasa wameiteka Mererani na WANA APOLO hawana chao tena.

Visa vya Mkapa na Mrema ama kweli vilikuwa vikubwa.

Sasa tukio kwenye AWAMU MPYA YA KIZAZI KIPYA...

Kizazi ambacho hata hivyo ni makini sana tukipige msasa ili kisiingie kwenye UFISADI NA KULIANGAMIZA TAIFA!

NI MUHIMU KUWEKA MAANANI KUHUSU KIZAZI KIJACHO NA TUSIWE WABINAFSI KWANI UBINAFSI NA HUSUDA SASA VIMEWAJAA WABONGO NA HATA NILIPOKWENDA BONGO NILISHANGAZWA SANA NA MABADILIKO NILIYOYAKUTA.

Sasa kuna BONGO FLEVA..SIJUI NI FLEVA GANI HII AMBAYO HAINA MAUDHUI YA UHURU KAMA FLAVOR ZA KIMAPINDUZI YA KIFIKRA ZA KINA LUCKY DUBE, BOB MARLEY, PETER TOSH, RAS KIMONO NK.

Mr Politician ya Nakaaya Sumari ndio kibao Pekee chenye mwelekeo wa kutoa ujumbe wa kuwaelimisha wananchi.

Ni juzi tu ROSTAM AZIZ...Ametowa pesa za kuisaidia kwaya...

Na pia nadhani kuwa hata mambo ya ZE COMEDY TUNAYAJUWA...Pia baadhi ya vyombo vya habari kununuliwa...

VIPI KUHUSU WASANII WA BONGO FLAVA?

Binafsi nina masiliano na RAPA AY..Nimemgusia kuhusu suala hilo...

Lakini naona sijui kwanini wana Bongo Flava hawataki kuanza kuingia kwenye vita hii ya Kihistoria!

Kipindi kama hiki mlitakiwa mtoe vitu...Hata kama si RAP..Weka hata REGGAE!

Tuna wa miss sana wasanii wetu wengine wa Reggae ambao walishatutoka kama JUSTIN KALIKAWE!

Hivyo ujumbe huu kwangu ni kwa wasanii wa KIZAZI KIPYA..

Muwe wabunifu na msijali kama mna wafadhili wenye kashfa za UFISADI...

Tafuteni wadhamini wapya...

Dr Slaa amewaaga wana jf kuwa anakwenda huko vijijini, na bongo hapo kuna Radio nyingi tu...

Sasa ni bora muingie kwenye HISTORIA KWA KUJIKITA KWENYE MAWAZO YA WANANCHI...

KWAMBA NI WAKATI WA KUWAHAMASISHA WANANCHI KWENYE HARAKATI ZA UHURU!

Video zenu nyingi zimekuwa zikionyesha wabongo wanavyosota....Lakini hamjawahi kuonyesha kuwa ni nini hasa kimepekea matatizo hayo!

Mfano wa kibao cha NIKUSAIDIEJE Cha Profesa JAY...

Tunawa hamasisha sasa mujiunge kwenye Vita Dhidi ya ufisadi.
 
Jmushi.. najua wewe mwenyewe ni kijana wa kizazi kipya... na hii fani unaiweza sasa onesha mfano. Nikutengenezee beat ya uhakika?
 
Jmushi.. najua wewe mwenyewe ni kijana wa kizazi kipya... na hii fani unaiweza sasa onesha mfano. Nikutengenezee beat ya uhakika?

Mzee Mwanakijiji ningeshukuru sana..Umeshawahi kusikia kibao cha Life cha D'Money feat AY?

Kibao hicho kilitoka mwaka 2005 kama sikosei na kinatabiri mambo mengi sana na hata yale ambayo tulikuwa hatuyajuwi kama vile kucheza faulo kwa wana ccm ambao kumbe ni kweli walifanya hivyo mwaka huo kwa kutumia EPA na wanamtandao.

Na pia kibao hicho kiligusia kuhusu UKABILA...Na sasa tunajuwa ni KWELI kwani yaliyotea na abayo yanaendelea kutokea kwa watu kutaka kuligawa taifa kwa misingi ya kikabila.

Kiligusia uwezekano wa kumwagika damu na ni kweli sasa tunazungumza mambo yaliyotabiriwa wakati hata JK haja apishwa!

Kiligusia ukabila wa kenya pale Tom Alipouwawa kwa chuki za ajabu ajabu na matokeo ya Kenya tunayajuwa damu ilimwagika!

Ni kibao ambacho kilipigwa mara kadhaa tu na Radio one...
Lakini ndani AY kachana safi tu.
 
MKJJ Wapi biti?
Ama it was a joke?
Hata hivyo nafikiri kuna vijana wengi tu wanaweza kufanya mambo...Mi ntawaandikia mashairi wakitaka.

NB:Bob Marley alipiga vibao safi sana vya ukombozi Wa Afrika kama vile Afrika Unite,Zimbabwe,Rat Race,War nk.

Hayati Lucky Dube ana kitu inaitwa HOUSE OF EXILE.

Ras Kimono ana MANDELA.

Dokta Remmy ana MREMA.

Nakaaya Sumari yeye ana MR POLITICIAN.

Cocotea YEYE ANA OBAMA NA ANAANZA ZIARA YA EUROPE(COCOTE SAMBAMBA NA OBAMA)

Sasa tunataka kusikia mapande ya KI UHURU UHURU.

FORGET ABOUT STAREHE KWASASA...FREEDOM FIGHTERS DONT EVEN CARE WHERE THEY ACTUALLY SLEEP OR EVEN WHEN AND AT WHAT TIME THEY WILL EAT!

Fufueni Muziki huo kwa kujikita kwenye FIKRA ZA MBONGO KWENYE KIPINDI HIKI CHA MPITO ILI MKUMBUKWE KAMA KINA SHAABAN ROBERT NK.
 
kwanini unafikiri ni Joke.. I'm very serious.. you didn't know niko kwenye fani ya muziki pia. Miye nitazibua kibao changu sometimes this year.. ningekuwa na muda ningeipua albamu nzima. muda tu.
 
Niliwahi kuanzisha thread hapa kuhusu Mageuzi yaliyotokea nchini Kenya. Nilielezea jinsi kikundi ya Redykyulas ambavyo kiliweza kuwaelimisha wananchi wa Kenya jinsi viongozi waliokuwa madarakani walivyokuwa wakiwasaliti. Na vilevile kuwaelimisha jinsi ya kuweza kuwaajibisha, naamini sisi wenyeywe tulishuhudia ni mawaziri wangapi na wabunge walivyoweza kupoteza nafasi zao. Naamini tukijifunza yale kwa makini na kuingizwa katika usanii, watu watavutiwa na kujifunza zaidi.
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=11172
 
Si wakati wa kuwaelezea namna ya kuwaelimisha bali ni wakati wa kuwaelimisha.
 
Si wakati wa kuwaelezea namna ya kuwaelimisha bali ni wakati wa kuwaelimisha.

Utawaeleweshaje husipowapa namna ya kuelewa?? Kuna namna ya ufundishaji Mushi, hata huko shule kindergaten ya Kibongo tulikuwa tuhahesabu vizibo ya soda au vijiti. Hiyo ilikuwa ni namna ya kuelewa hesabu za kujumlisha au kutoa. Namna ya uelewa iko tofauti tofauti inategemea na mwalimu mhusika ndio maana hata katika sanaa kuna nyimbo, ngonjera/ugani, maigizo n.k Njia zote hizo zinaweza kumuelewesha mtu madhui ya ujumbe hata kama ujumbe utakuwa uleule.
 
Namna ya kuelewa ndiyo hiyo tunayowaambia watumie vipaji vyao kulikomboa Taifa.
Na si tu kwa muziki bali hata kwa Movies nk.
Kwasababu hadi uone RA kaenda kuionga kwaya..Basi hapo ujuwe ana uhakikia hawa wa kizazi kipya hawana nguvu tena.
Sasa sijuwi kwanini a assume hivyo.
Tunajuwa si lazima wasanii wote wanaweza kufanya kufanya hivyo.
Kuliko wakae kimya...Ni heri wachaguwe moja na ndio maana muziki huo labda umeyumba kwasababu wananchi wanaishi maisha ya tofauti na message hai ingii akilini kwani wasanii wameshindwa kusoma ramani na kujuwa where to take the message and how to target the industry at the same time sending a positive message.
Hivyo narudia tena...Ni muhimu vijana wetu wakapewa uhuru wa kushiriki kwenye mkakati huu wa UHURU.
 
Jmushi,

Wagosi wa kaya wametoa wimbo mkali sana wa POLE, wamezungumzia yote yanayotokea na hata wamempa POLE JK kwa uchumi Unaokua POLEPOLE (MANENO NDANI YA WIMBO). Wimbo ni mzuri sana na mashairi yametulia sana, unapigwa ila sio sana si unajua redio zetu na madj? lazima wapewe Ma dj kitu kidogo ndio upigwe au uufanyie kampeni ya nguvu.

Huo wimbo unazungumzia ufisadi wote uliotokea majuzi hapa nchini yaani una hot issues zote.

Wasiliana na Fred Mkoloni kwenye +255 71 623 8590. Uweze kuwasaidia usikike zaidi na uweze kuwasaidia wa shoot VIDEO.

FairPlayer
 
Ndug JMushi nimekusoma na nimeona nia yako ni nzuri na kwa maendeleo ya taifa hili.Mimi binafsi nadhani hawa wasanii wetu ndio wanakipaji lakini wanavyoimba vingi vinazidi mapenzi?Wao mapenzi ndio chakula kwa hiyo haya ya siasa hawayataki.Lakini Prof.jay kidogo huyu anamwelekeo na wale waliokuwa wagosi wa kaya siku hizi sijui wamepotelea wapi?Wasanii watakapoanza kuattack politicians direcly kivumbi kitatimka nadhani umesahau kuna wakati Hakielimu walionywa kuhusu matangazo yao nadhani wasanii wanalijua hili kwamba hii ni nchi ya wenyewe jifanye kiherehere na domokaya wata kuarrange and fix you well.Kwa hiyo wasanii wetu hawa vilevile wanahitaji elimu.
 
Nadhani kama mtu ana nia ni vizuri tukaacha blah blah tukawasaidia hao wasanii

Tuwasaidie nini maana hata kusaidika hawa saidiki.Mpe mashairi then ataboronga tuu.Madj watamfanyia hujuma,wanasiasa wataweka mikono yao humo mwishowe itakuwa comedy show.
 
Tuwasaidie nini maana hata kusaidika hawa saidiki.Mpe mashairi then ataboronga tuu.Madj watamfanyia hujuma,wanasiasa wataweka mikono yao humo mwishowe itakuwa comedy show.

Mmhhh, kweli JF ni ya WOTE.

Umeambiwa wanataka mashairi? na hayo wanayoimba ni nini?

Kaazi kweli kweli.

Ndio watanzania sisi.
 
Ni kweli Ma DJ nao ndio tatizo...Na ndio maana nikatowa mfano wa ZE COMEDY pamoja na kwaya kupewa msaada na RA.
Ma DJ wapewe mishahara mizuri ili haya mambo yawe ni kwa manufaa ya Taifa kwani wasanii kwa utamaduni wetu sisi ni kioo cha jamii.
Sasa unafikiri hao mafisadi hawajapenya kwa namna moja ama nyingine kujaribu kuidhibiti hiyo situation?
Ni wakati kwa wasanii kufumbua macho na wafadhili wazalendo kuwasaidia wale wasanii waliojitokeza kama hao wagosi wa kaya nk.
 
Mmhhh, kweli JF ni ya WOTE.

Umeambiwa wanataka mashairi? na hayo wanayoimba ni nini?

Kaazi kweli kweli.

Ndio watanzania sisi.tehetehetehe!Mkuu hiyo ni mojawapo ya njia niliyo suggest ya kuwasaidia hawa wasanii wetu.Kuna watu wanaweza kutunga mashairi ila hawawezi kuimba na labda hawana muda wa kuimba Kama MwanaKjj anavyosema lakini kama akiwapa mashairi yake kwani ujumbe haufiki?Kaka/dada read and understand usikurupuke tuuuuuuu!
Ni sawa na wewe uliyempa JMushi no.ya simu ya mkoloni walikuambia wanataka msaada wa Video Shoot?
Kweli JF ni ya wote na siyo ya wachache wenye fikra duni kama wewe.
 
Jmushi,

Wagosi wa kaya wametoa wimbo mkali sana wa POLE, wamezungumzia yote yanayotokea na hata wamempa POLE JK kwa uchumi Unaokua POLEPOLE (MANENO NDANI YA WIMBO). Wimbo ni mzuri sana na mashairi yametulia sana, unapigwa ila sio sana si unajua redio zetu na madj? lazima wapewe Ma dj kitu kidogo ndio upigwe au uufanyie kampeni ya nguvu.

Huo wimbo unazungumzia ufisadi wote uliotokea majuzi hapa nchini yaani una hot issues zote.

Wasiliana na Fred Mkoloni kwenye +255 71 623 8590. Uweze kuwasaidia usikike zaidi na uweze kuwasaidia wa shoot VIDEO.

FairPlayer

Unaweza kumwaga lyirics hizo hapa?
Tungeshukuru kama una uwezo wa kutupa hizo lyrics za huo wimbo wa wagosi wa kaya.
 
tehetehetehe!Mkuu hiyo ni mojawapo ya njia niliyo suggest ya kuwasaidia hawa wasanii wetu.Kuna watu wanaweza kutunga mashairi ila hawawezi kuimba na labda hawana muda wa kuimba Kama MwanaKjj anavyosema lakini kama akiwapa mashairi yake kwani ujumbe haufiki?Kaka/dada read and understand usikurupuke tuuuuuuu!
Ni sawa na wewe uliyempa JMushi no.ya simu ya mkoloni walikuambia wanataka msaada wa Video Shoot?
Kweli JF ni ya wote na siyo ya wachache wenye fikra duni kama wewe
Soma tena post yangu nimesema, tatizo sio WIMBO, nyimbo zipo. Na sikusema asaidie Video tu, nimesema a promote wimbo kusikika hewani ikiwa video ni njia mojawapo. UJUMBE HAUFIKI KWASABABU WIMBO KUTUNGA NI RAHISI ILA KUSIKIKA REDIONI NA KWENYE TV (Ujumbe kuwafikia walengwa) NDO ISSUE.

Aisee ngoja nijiondokee. Tofauti ya Mwizi na aliyekuwa anaoga akaibiwa nguo zake haitaonekana.

Umeshinda. OVER and OUT for GOOD on this!
 
Hatukuwa tunashindana Mkuu ila tunajaribu kuelimishana maana naamini wewe ni mtu mzima na mimi ni mtu mzima kwa tunalofanya ni kueleweshana na kufundishana na siyo kushindana.
Anyways sorry kama nilikukwaza in any way.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom