Wasanii wa bongo Harmonize na Vanessa katika dilemma kubwa

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,140
2,012
WASANII WA BONGO HARMONIZE NA VANESSA KATIKA DILEMMA KUBWA.


Mambo vipi wanajamii,
Kuna choice nyingi sana mtu waweza kufanya pasipo pata wasiwasi wowote juu ya maamuzi yako, Lakini kuna mara unakuta unamachaguo mawili yote yenye kuwiana ulazima wake apo sasa ndipo dilemma anazaliwa. Nimekuwa nikufwatilia kwa karibu msani HARMONIZE na VANNESA baada ya kuhisi huenda kwa sasa wapo kwenye dilemma nitaeleza kwa nini nahisi hivyo.

Kama alivyo sema mwana stoic mmoja hapo zamani ya kwamba mambo yote huwa tunajitakia wenyewe, ndivyo ilivyokuwa kwa HARMONIZE maana mara baada ya kutoa remix ya KWANGARU akipraize serikali hakutegemea kwamba alijipa majukumu makubwa angali yeye bado ni kijana wa miaka 25. Sasa dilemma inayomkumba ni juu ya bleach ya kwenye nywele zake, hizi nywele zinamtesa sana harmo pale anapoalika kwenye shughuli RASMI maana akitazama KUSHOTO KULIA anaona watu ambao wapo formal wakimwangalia kwa jicho la kutokukubaliana na staili ya nywele zake, nisiwafiche ata mimi sikubaliani na nywele zake sijui nani anayemwambia kwamba zinampendeza ( inabidi akamatwe atoe maelezo kipi kinachopendeza ) ishu ni kwamba bleach inafaa sana kwa watu ambao wapo light skin sasa ndugu yetu HARMO anakuwa pundamilia. Ndo maana hapa majuzi kwenye sherehe za uhuru akavaa miwani nyeusi ili kuficha soni yake Lakini akasahau manywele yake, ila huyu dogo yaani kapiga show huku kaamkia kwenye sherehe nasubiri siku aje kudondoka kwa exhaustion ndo atajifunza.

Katika dilemma kubwa ambazo zimewahi kukumba bidadamu tangia enzi na enzi ni dilemma inayowaandama wanawake mashughuli juu ya kuwa wazazi au wendelee na shughuli zao. Kutokana na miundo ya kibiologia mwanamke ndio atabeba mimba miezi tisa na pia kuwa responsible kwa malezi ya mtoto ndani ya miaka tisa ya mwanzo. Tukija kwa VEE ninadadavua kuwa hii ndio dilemma iliyomkalia kooni kutokana na interview aliyofanya jux hivi karibini akisema vee alisema waachane ili akoncentrate na mambo yake, hapa naona JUX aliamua kuficha kwamba alikuwa akimpushi vee wapate mtoto kutokana na kimbunga cha wasanii kuzalisha refer DIAMOND. Sasa vee akipiga hesabu anakuta hazijumlishiki ikabidi ampige chini jux na acheki na mpenzi ambaye hana haja kuwa baba hapa ndipo anaingia ROTIMI ambako mpaka waweze kucyle movement zao itachukua miaka mitano ambako VEE atakuwa kashasogea na plani zake. Inaonekana vee kaamua career first lkn dilemma iko pale inamsubiri pale atakapofumba tuu macho inamvaa pengine inamjia hata ndotoni who know.

Ndo hivyo wapambane ila wasikimbie dilemma kwa kuvuta sigara nyingi aku kutumia pombe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom