Persona za Wasanii wa Bongo

Ricky Blair

JF-Expert Member
Mar 13, 2023
391
872
Nimeona hii kitu Wasanii wa Bongo hata wa nje lakini ngoja nizungumzie wa Bongo;

wanapenda kuiga kila vazi au persona fulani hata kama si wao bali wavume;

Regardless of his personal life Diamond ni muimbaji mzuri kama wengi tu lakini me nashangaa hii persona yake mpya ya kuvaa micheni sijui grills kwa meno yaani persona ambayo naona kama more ya Jux na sio yeye;

Diamond wa Moyo Wangu, Mawazo hata hizi nyimbo za Zuwena na Yatapita; jinsi alivyo, nywele fupi, kuvaa simple na mwili wake naona anapendeza km hapo kwa picha uvoona tofauti;

Ushauri wangu kila mtu abaki na swaga zake asilia na unapendeza ivo kama Mzee Yusuf na Taarab zake hawez pandia Hip Hop, km Jay Melody na kuimba nyimbo zake za taratibu na mapenzi hawez kuwa Fid Q na kama Jay Dee hawezi kuwa Isha Mashauzi km Q Chief sio Juma Nature au Jay Moe na Mwana FA watu wa ku rap na kina Dulla Makabila na Sengeli sio kina Mdee na kina Ray C au D voice sio Mpotto;

Kila mtu abaki na persona yake na hata uvaaji sio kuiga iga lol.

IMG_9664.jpeg
IMG_9665.jpeg
 
haya ni matokeo ya pesa nyingi zisizo na kazi.

huyu bwana hizi cheni zote na masaa aliyovaa ni kama bilioni 2 hivi za kibongo(kama hajatupanga).
sasa kusema anatafuta persona kwa bilioni 2 haiingii akilini,ni kuwa tu mahela yasiyo na kazi.

kama damu kali anayo,hata akivaa kawaida tu huwa anaonekana vyema kabisa.
 
Mi naona hili tatizo sio kwa Diamond peke yake, hii shida inawakumba vijana wote dunia nzima, lack of cultural Identity yaani kukosa utamaduni wa asili, vijana wengi wa africa, south amerika, eastern europe, na russia hawajaweza kubuni identint ya kijana mwenye fedha aishiye hivyo vijana wengi kwenye hayo maabara ya njaa wanajikuta wanakopy utamaduni wa black american.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom