Wasanii kumuunga mkono Magufuli

Wasanii kumuunga mkono Magufuli

Tuache uwanja wa kampeni uwe huru kwa watu wote wanaopenda kupigia kampeni upande fulani. Wasanii ni watu wanaohudumia jamii sawa na viongozi wa dini, wasanii wana utashi, wafuasi na wapenzi wao sawa na viongozi wa dini. Wasanii wanashawishi wapenzi wao na viongozi wa dini wanashawishi wafuasi wao, lakini mwisho wa siku watu nao huwa wana akili na matakwa yao, wataamua nani watampigia kura.

Haiwezi kuwa sawa wasanii waruhusiwe kufanyia mtu kampeni lakini viongozi wa dini wanyimwe. Kwani shida ni nini hasa Mh. Lubuva?, ruhusu wote au kataza wote (all or none) utaeleweka sana.

Naomba mifano mitano ya nchi ambazo zimeingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu tu ya wasanii kushabikia upande fulani wa kisiasa.
 
Ila wengi wa wasanii no pro-CCM! Donge la Kampeni lilishatengwa na wamekumbukwa!!
 
Naomba mifano mitano ya nchi ambazo zimeingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu tu ya wasanii kushabikia upande fulani wa kisiasa.
Taasisi yoyote hata iwe ya kishetani iko sawa kama itapigia kampeni upande fulani, lakini haiko sawa kama itapigia kampeni upande wa pili. Tumeona baadhi ya vyombo vya habari, taasisi, na makampuni yakilalamikiwa na mengine yakinyamiziwa kimya yanapoegemea upande.
 
Mkuu, nimeongea lugha nyepesi tu ya Kiswahili. Nimetumia maneno rahisi kuwa "Naomba mifano mitano ya nchi ambazo zimeingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu tu ya wasanii kushabikia upande fulani wa kisiasa." Naona unanipa hadithi badala ya kujibu swahi langu. Kama hakuna mifano sema hakuna, kama ipo basi itaje hapa. Sihitaji hayo maelezo uliyonipa, nahitaji mifano tu.
 
Msanii mahiri wa filamu nchini ,anayeongoza kwa skendo za Ngono nchini,Wema Sepetu ,kwa niaba ya wasanii wenzake zaidi ya 200 ambao ni wanachama wa CCM wamezindua tamasha la Mama Ongea na Mwanao 2015,lenye lengo la kumuunga mkono mgombea urais kupitia chama hich Dkt John Magufuli na makamu wake samia hassan suluhu....
 
Yeye mwenyewe anauzika? Jamii inamtambuaje. Yeye alikosa kura hazikutosha halafu aje amuombee mwingine kura, hii inawezekana kweli?
 
Kitu kilichoanzishwa mwaka 1977hakiwez kuwa kipya mwaka 2015 ongea kwa mntiki mkuu...kwa kikwete mlisema hivi hivi matokeo yake tupo hapa

Kwahiyo unasema Lowassa na ile taasisi aliyotokanayo ccm ndo inatuhakikishia mabadiliko? Jitambue bwa'mdogo
 
Kwahiyo unasema Lowassa na ile taasisi aliyotokanayo ccm ndo inatuhakikishia mabadiliko? Jitambue bwa'mdogo

Huwez ukaleta mabadiliko wakati chama kilekile kuwa na akili....hapo waswahili wanakwambia umebadili chupa wakati mvinyo uleule unategemea nini?....gongo ni gongo tuuuu hata iwekwe kwenye chupa ya chai bdo italewesha usidanganyike na khanga ulizopewa kama unahitaji ntakupatia hata mimi doti utakazo......brah....
 
Ni aibu kwa ccm, hapo usikute anafanya hivyo ili baadae apate uteuzi serikalini, na unaweza kushangaa kumsikia anapewa uongozi kweli.
 
Ni aibu kwa ccm, hapo usikute anafanya hivyo ili baadae apate uteuzi serikalini, na unaweza kushangaa kumsikia anapewa uongozi kweli.

Itakuwa anaufukuzia ukuu wa wilaya,kwa strugle zake izo magufuli hawezi kumuacha mtupu,umesahau alivmtunza madolari ,ana target zake hapo lazima
 
Kwahiyo unasema Lowassa na ile taasisi aliyotokanayo ccm ndo inatuhakikishia mabadiliko? Jitambue bwa'mdogo

Alaf kama ni mtu wa kufuatilia mambo ya maana kuna western proverb inasema "three type of people are very reluctant to develop
i)those who accepting everything
ii)those who tend not to accept others oppinions
iii)those who FEAR TO CHANGE
Sasa mwana usiwe muoga wa mabadiliko hata NYERERE alitaka mabadiliko juu ya serikali ya ukoloni ndio maana akapigania uhuru....ushawahi jiuliza je , kama angeogopa mabadiliko kama ilivyo kwako ingekuwaje???????
Fanya maamuzi ambayo hata kizazi chako cha baadae kikijua kitajivunia juu yako
DO NOT STAY AS AN OAK AND DOING NOTHING, ......hav a cute jancture
 
Mkuu, nimeongea lugha nyepesi tu ya Kiswahili. Nimetumia maneno rahisi kuwa "Naomba mifano mitano ya nchi ambazo zimeingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu tu ya wasanii kushabikia upande fulani wa kisiasa." Naona unanipa hadithi badala ya kujibu swahi langu. Kama hakuna mifano sema hakuna, kama ipo basi itaje hapa. Sihitaji hayo maelezo uliyonipa, nahitaji mifano tu.
Watakujibu wasomaji wengine wa jf hilo swali lako linalotaka kuhalalisha kutumika vibaya kwa wasanii kubeba mgongoni mafisadi kwenda Ikulu. Baada ya uchaguzi kwisha kazi za wasanii hao zitadoda kwa hasira za walioshindwa, na mifano hai tunayo ya wasanii walioanguka kwasababi za kushabikia vyama.
 
Ni kweli ila tatizo la wasanii wa bongo ni NJAA, CCM iliwaahidi mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwajengea studio ya kisasa na pia kulishuhulikia tatizo la haki miliki(copyright) ya kazi zao. ILA HAKUNA LILILOFANYWA NA CCM,zaidi ya kuwatumia kipindi cha kampeni ili kupata watu wengi kwenye mikutano yao.

Mkuu hao wanajisumbua sana maana upinzani kwa sasa(ukawa) hawahitaji kuwa na kina komba
 
Watakujibu wasomaji wengine wa jf hilo swali lako linalotaka kuhalalisha kutumika vibaya kwa wasanii kubeba mgongoni mafisadi kwenda Ikulu. Baada ya uchaguzi kwisha kazi za wasanii hao zitadoda kwa hasira za walioshindwa, na mifano hai tunayo ya wasanii walioanguka kwasababi za kushabikia vyama.

Huo ndio ukweli hawa wasanii wakimaliza kuwafanyia kampeni hao ni sisi wananchi kususia kununua kazi zao tuone kama ela za kampeni watakaa nazo kwa miaka mitano
 
Back
Top Bottom