Wasaliti hawafichiki, Henry Matata arejea CCM

Wasaliti hawafichiki, Henry Matata arejea CCM

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
142,106
Reaction score
285,844
Kamati kuu ya CHADEMA ilipomtimua ilionekana kama ni uonevu , lakini sasa imedhihirika wazi kabisa kwamba CHADEMA haikosei. limeripoti leo kuhusu jambo hili.

MY TAKE - usaliti ni laana mbaya sana .

============================

1.jpg

HATIMAYE Meya wa Halmashauri ya Ilemela jijini Mwanza, Henry Matata, amejiengua ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uamuzi aliufanya juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Minazi Mitatu Kata ya Kitangiri Manispaa ya Ilemela ambako alikabidhi kadi yake ya Chadema kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu na kupewa ya CCM.

Akizungumza baada ya kurudisha kadi ya Chadema, Matata alisema kabla ya kujiunga na upinzani alikuwa ndani ya chama hicho tangu utotoni lakini baada ya CCM kumfanyia mizengwe kwa kuweka jina lake nafasi ya nne katika kura za maoni kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, aliamua alikimbilia Chadema.

Alisema alipokimbilia Chadema alipokelewa kwa shangwe kwa sababu alikuwa anakubalika kwa wananchi na kumpa nafasi ya kuwania udiwani na kushinda Kata ya Kitangiri.

Alisema baada ya kuanza kutekeleza majukumu ya udiwani ndani ya upinzani alijikita kutekeleza ilani ya CCM ndipo alipoanza kuchukiwa.

"Mimi damu yangu ilikuwa CCM ingawa nilikuwa Chadema, baada ya kushinda udiwani nikaanza kupigania nafasi ya umeya kwa bahati nzuri nikapata.

"Sasa ukishakuwa meya lazima utekeleze ilani ya CCM kwa sababu ndiyo chama tawala… wenzangu wakaanza kunichukia na kuniundia zengwe kama ilivyokuwa awali CCM.

"Ikafika wakati nikavuliwa uanachama nikabaki diwani wa mahakama- lakini sikupoteza chochote kwa sababu stahili zangu zote nilipata," alisema.

Chanzo: Mpekuzihuru
 
Hivi usaliti mnauja au mnaropoka au amjui alietika ccm kwenda chadema ni msaliti
 
msaliti ni yule anayehama baada ya kununuliwa akiwa na lengo la kukwamisha mabadiliko , huwezi kwenda ccm leo ( chama kilichochoka ) ukasaliti ukombozi , halafu ukajifanya unataka kuleta maendeleo

Hapana ujatoa maana ya usaliti umeegemea upande moja
 
Kamati kuu ya CHADEMA ilipomtimua ilionekana kama ni uonevu , lakini sasa imedhihirika wazi kabisa kwamba CHADEMA haikosei. limeripoti leo kuhusu jambo hili.

MY TAKE - usaliti ni laana mbaya sana .

============================


Chanzo: Mpekuzihuru

Aende zake mpuuzi sana huyo .
 
Back
Top Bottom