Wasabato ujumbe wenu huu hapa

Status
Not open for further replies.
Kwani yawezekana kwa kupitia mafundisho yake ndipo walipojifunza tabia zao za ajabu ajabu, badala ya kufuata mafundisho ya Yesu Kristo Aliyeleta Agano Jipya katika ulimwengu.

Ni watu ninaowadharau sana..
 

Waambie hao wataalam wa kuosha vikombe kwa nje,na kuacha ndani.
Tatizo lao ni moja tu,Wanafiki!
 
Mkuu Ntuzu nia kuu ilikuwa ni kuonyesha si makosa kupumzika siku ya kwanza ya juma,kuwa hata mitume waliabudu siku ya kwanza ya juma. Unaponiambia agano jipya linamuhusu Yesu sikuelewi,kwani alikuja kwa ajili ya nani? Hebu msikie Paulo 2 wakorinto 3:6- "naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya,si wa andiko, bali wa roho kwa maana andiko huua,bali roho huhuisha"endelea kusoma hadi mstari wa 15-17"ila hata leo torati ya Musa isomwapo utaji huikalia mioyo yao. Lakini wakati wowote watakapomgeukia bwana ule utaji huondolewa. Basi bwana ndiye roho, walakini alipo roho wa bwana hapo ndipo kwenye uhuru". Kwa hiyo andiko(torati) huua, bali roho agano jipya huhuisha. Ni uchaguzi tu, wasabato mmeamua kuwa wahudumu wa andiko,nasi wa agano jipya ambalo kwa imani limetuwena huru. Soma 1 wakorinto 10:25-31 halafu Luka 10-8 "na mji wowote mtakaoingia makiwakaribisha vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu. Kwa vifungu hivi tumeruhusiwa kula kila tukikutacho sokoni kinauzwa tutachokaribishwa,poleni sisi tuko
 
Wasabato ni waislam zaidi kuliko wakristu. Watu wa kufuata sheria sana hata kama haziingii akilini eg usile, usinywe, usi..."FAITH and REASON" avoid fundamentalism
 

we nani kakwambia ni kafara vitu vingne sio lazima tuandike uko ulikofika ndugu baki na unachoamini sio kukashifu wengne wanachaoamini
 

hyo unasema kweli mwamba ngozi huvutia kwake wao wanajiona bora na wanacho abudu ni sahihi hapo watabishana mpaka wachoke kwa Mungu wote ni sawa na vitu ving ni kwa neema tu sasa kupondea wengne wanachoamini si sahihi mtu yoyote anaweza kusoma bible kwa msada wa roho mtakatifu na hakaelewa sasa ku ng'ang'ania wao ndo bora kwa kigezo gani naona hamna ya kubishana na watu wasio amini roho mtakatifu na kunena kwa lugha na kama ingekuwa mbinguni wanaendaga kwa kusali jumamosi jumapili ijumaa basi wote wangeenda kubishana mambo ya dini na kujiona bora ni useles inahtaji Roho wa Mungu pekee yako
 
Haturuhusiwi hata kushangaa?



Dada yng FaizaFoxy naielewa Imani yako! Nafikiri ingekua vema km ungebaki Kua msomaji tu!

Maana tumefika mpk hapa ni kwasababu tunajadiliana Vzr!
 
Last edited by a moderator:
Wenyewe kwa wenyewe leo tunakashifiana kuhusu imani? Unataka kuufanya ukristu kama dini isiyo na msingi na muongozo....aibu!
 


Mkuu Ktk Yale mafungu uliyonionesha! Yanaelezea Kua tukio Hilo lilifanyika Siku ya kwanza ya Juma! Na si km ni fundisho la kupumzika Siku ya kwanza ya Juma!

Kumbuka Mungu si kigeugeu kwamba aitakase Siku ya 7 Na kupumzika then aje abadilike hapo baadae!


Na pia Ktk ile Jerimiah uliyonipa, pale kinachozungumziwa ni ukombozi Wa Yesu kwa Watu wote Ktk Hilo agano linalosemwa hapo! Na si km la kuwamboa Wana Wa Israel! Ndio Maana nikasema Hilo swala lilikua linamuhusu Yesu! Ebu isome tena Hiyo Jerimiah!
 

Mbona hoja zangu hamjibu? Hatujakimbia tupo tunawasikitikia na kuwaombea angalau mumjue Yesu.
"Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu,ni kwa ajili yao ili WAOKOLEWE. Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika MAARIFA." (Warumi 10:1-2).
Habari za neema ya KRISTO haziwezi kufahamika bila huyo Roho mtakatifu mnayemkataa.
NAKUPENDA ROHO MTAKATIFU.
 
Last edited by a moderator:

Nashukuru Ntuzu hiyo ya unajisi wa vyakula una thread yake na nilishaisoma na kuchangia.

Nasubiri tu majibu ya kuhusu mavazi ya mwanamke kufunika nywele, kupaka rangi kucha n.k

Pamoja na hii ya vinywaji kama cocacola na chai ya rangi. Ahsante
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahahaha, unachekesha sana unaposema hatuna roho mtakatifu eti kisa hatuneni kwa lugha. Au wewe ndie mtoa roho mtakatifu kwa wanadamu wengine? Na ndio maana unasema sisi wasabato hatuna roho myakatifu. Sikia sasa Paulo anaongea nini kuhusu muonekano wa mtu aliyejazwa roho mtakatifu.
Wagalatia 5:22,23 Lakini tunda la roho ni upendo, furaha, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo hayo hakuna sheria. Mtu aliyejazwa roho mtakatifu anajulikana kwa kutoa hayo matunda na si kwa kuropoka ropoka maneno yasiyo maana. Ndio maana Yesu alitutahadharisha kwa kusema hivi Mathayo 7:20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. Je roho wenu wa kusababisha mmuropokee Mungu wakati wa kuomba, anasababisha muwe na hayo matunda ya roho?.
 

Duuuh naona hapo red unajifariji, wa sda wamkatae roho mtakatifu????!????!!!!, pole sana. Kwa taarifa yako roho mtakatifu tunamfahamu sana, ndio maana katika mafundisho ya msingi ya imani, msingi unaoongelea roho mtakatifu ni msingi wa tano, na unasema hivi
God the eternal Spirit was active with the Father and the Son in Creation, incarnation, and redemption.

He inspired the writers of Scripture.

He filled Christ's life with power.

He draws and convicts human beings; and those who respond He renews and transforms into the image of God.

Sent by the Father and the Son to be always with His children, He extends spiritual gifts to the church, empowers it to bear witness to Christ, and in harmony with the Scriptures leads it into all truth
.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…