Wasabato ujumbe wenu huu hapa

Status
Not open for further replies.

Kama Yesu hakuagiza kuandikwa Biblia wewe unaamini kwa kutumia kitabu kipi na unauhakika gani yote yaliyoandikwa humo ni ya kweli... Maana kama kila mtu alandika Biblia kwa aliyoyashuhudia hakika kila mwandishi hatafikisha yale yaliyotendwa na kuagizwa na Yesu kwa 100%. Ndio maana habari za Yesu katika Injili nne ukisoma kuna maneno yanakikanga kila mwandishi kaandika kivyake kwa tukio hilohilo moja.
Tofauti na amri za Mungu ambazo zilishushwa kutoka juu.
 
Ningekuomba uwe msomaji tu sio uanze kutuharibia mada yetu! Sisi twajadili uzuri kabisa hapa

Mwache huyo atatupotezea muda tuendeleeni na mada yetu tupate kufundishana na kujuzana mengi kuhusu Biblia.
 
www.exadventist.com/../default.asp

jisomee mwenyewe.

Sina hata muda wa kusoma mawazo ya mapandikizi(hasa majesuits) walioingizwa kanisani kwa sda ili waliharibu na waliposhindwa wakaondoka na kutoa hizo pumba.
 
Mkuu Naona unaongea vitu via ajabu tu tena bila maandiko!


Mungu ametuagiza kupumzika Siku ya Saba na ni sabato Yake! Wapi Ktk maandiko tumeagizwa kupumzika Siku ya kwanza ya Juma?

Maandiko gani zaidi nimekuambia soma (kutoka 12;16) Mungu amesema"siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa na kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yoyote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula,hiyo ifanyike kwenu" pia nimesema soma(matendo 20:7)"hata siku ya kwanza ya juma,tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akahutubu...." ina maana mitume wa kwanza walifanya ibada siku ya jumapili kama tunavyoelezwa hapa na Luka,maandiko haya umeshayasoma? Wasabato kwann hamtaki kuwekwa huru kwa agano jipya,soma(yeremia 31:31-33)"angalia siku zinakuja asema bwana nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli,na nyumba ya Yuda si kwa mfano wa agano lile nililofanya na baba zao..")soma yote halafu niambie agano lipi mwalifuata?
 
Ningekuomba uwe msomaji tu sio uanze kutuharibia mada yetu! Sisi twajadili uzuri kabisa hapa

.......haya bana Ntuzu ngoja nivumilie huku nikistagh'firuu !:wave:
 
Last edited by a moderator:


Kwani Yesu alipoingia Ktk sinagogi na kusoma kitabu cha Isaya juu ya unabii ulokua unamhusu yeye vilikua vimeandikwa wapi?
 


Mkuu thx kwa mafungu yako!


Lkn mafungu yako hayazungumzia kwamba yatupasa kupumzika Hiyo Siku km takatifu!

Hapo Mungu alikua akiwaelekeza wana Wa Israel juu ya pasaka ambayo walikua Wana takiwa kula kabla ya Safari! Ukisoma kuanzia kutoka 12:1-28 ndio kuna Hiyo habari!


Na pia Ktk utume Wa Paul alifanya kz siku zote za kuhubiri! Kwahiyo km Watu walikusanyika Siku ya kwanza ya Juma haimaanishi kwamba tuitunze km Siku takatifu ambayo Mungu alituagiza kupumzika! Kwa mfano Hiyo Matendo 20:7-12 Paul anaonekana kupeleka huduma Troas. Na Bado wakiwa Huko Siku ya Mikate ndio ikawadia! Kwahiyo Bado hakuna maagizo kwamba tuitunze Hiyo Siku km takatifu!

Unalifahamu Hilo agano Ktk Hiyo Jerimiah 31:31-33. Mbona maandiko yako wazi hapo sio agano la kubadili Siku km unavyosema Wewe? Sio agano km la kuwaokoa Wana Wa Israel Misri! Hili agano linamuhusu Yesu! Ebu soma ule Mstari Wa 33 utaona Hilo agano! Sasa Wewe unapata vipi kusema Kua ni agano la kubadili Siku?
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri sana,hata mimi kuna wakati uwa nashawishika kubadili dini na kuwa msabato kwani wengi wenu mna misimamo isiyoyumba ya kiimani na honestly wengi ni waadilifu,ila nilikuwa nasita kwa sababu watu walinieleza kuwa hiyo dini sio Wakristu,labda naomba unitoe shaka tena juu ya ili:Ni kwanini mnasoma zaidi agano la kale na kulipa msisitizo kuliko agano jipya?na kwanini sher4ia za Mussa ambazo nyingi zimetenguliwa na agano jipya nyinyi bado mnazikumbatia?ni kwanini ni haramu kula nguruwe.wakati biblia inasema kiingiacho sio haramu bali kitokacho,samaki wasio na magamba nk,nijuavyo mimi sheria za Mussa,almost zote zilikuwa ni za mpito kuwasaidia wanaIsrael kufika nchi ya ahadi ,walisafir kwa miaka mingi kuvuka jangwa,ukiangalia vyakula vingi vilivyozuiwa ni vyakula vya mafuta mafuta,nguruwe,samaki asiye na magamba,wanyama wasio na kwato etc hii ni applicable kila mtu akiwa anasafiri na familia kuwazuia wanafamilia bahadi ya vyakula especially vya mafuta ili wafike salama bila matatizo ya tumbo,na ukifika salama zile sheria kwa familia za usile mishikaki,kuku wa Salanda,vyakula vya mafuta etc zinakuwa sio applicable tena.Pia nisaidie vitu kama Coca cola,majani ya chai, sukari ect vimeandikwa biblia gani kwamba ni haraamu,wakati enzi hizo coca cola haikuwepo?
 



Mkuu Pamoja na kwamba nimeingilia hili swala lilikua linamuhusu ndugu Basluma Original

Mimi nilitaka kujibu kitu kimoja ambacho ata ndugu ZionGate aliniuliza cha kuhusu chakula na akajengea hoja km Wewe kwa si kimuingiacho mtu chaweza mtia unajisi Bali kimtokacho!


Wengi wamekua wanapotea kutokana na kueleweshwa vibaya juu ya hili andiko!

Ilikua ni kawaida ya Waisrael walapo chakula kunawa mikono mpk juu ya viwiko! Sasa mafarisayo wakamfata Yesu na kumuuliza, Kwanini wanafunzi wako wanakula chakula kwa mikono najisi? Matth 15:2. Na ufahamu kwamba Mafarisayo walikua wanaangalia usafi Wa nje ya mwili!

Kwahiyo hapo utaona kwanza swala lilikua ni kula chakula kwa mikono iliyo najisi yani sio misafi! Na si kwamba kujilia mivyakula hovyo tu na yaliyo najisi!


Ntaendelea kukufafanulia juu ya hili! Kwanza soma hapo uone!
 
Last edited by a moderator:
Wandugu,nitatoka nje ya mada kidogo.
Nimesoma na kuishi na wasabato sekondari na chuo pia ,kitu nilichogundua kuhusu hawa jamaa, kwanza kabisa ni Wabinafsi,wanajitenga sana na wakristo wa mathehebu mengine,pili wanajisikia kuwa wanajua biblia zaidi ya wakristo wengine. Tatu ukiwauliza Ellen G White ni nani,majibu wanayotoa ni ya mkato mkato.
Kifupi,hawa jamaa mi walikuwa wananikwaza kwa tabia zao hizo za ajabu.
 
Mkuu ngonani

Ukiendelea kusoma kuanzia Mstari Wa 3-9 Hiyo Mathayo utaona jinsi Yesu anavyo wajibu tena akanukuu unabii Wa Isaya Ktk ule Mstari Wa 7,8,9 kwamba walimkaribia na kujifanya kumcha yeye kwa midomo Yao lkn mioyo Yao iko mbali.

Kwahiyo mpk hapa dhumuni la Yesu ni kuangalia usafi Wa moyo na si Wa nje ya mwili na kumwabudu yeye bure Huku wakifundisha mafundisho na sheria za wanadamu!

Kwahiyo mpk hapa hakuna swala la vyakula! Hapa ni usafi Wa rohoni!



Ktk ule Mstari Wa 11 ndio wengi hujenga hoja ya kujilia vitu hovyo tu!

Na Ktk Mstari Wa 16-20 hapo tena kuna maelezo ya Yesu juu swala Hilo Hilo! Hasa ule Mstari Wa 18,19 na 20 Yesu ameweka wazi juu ya Matendo yamtiayo mtu unajisi! Si kwa kula chakula kwa mikono michafu au usafi Wa nje Bali ndani ya moyo Na wala hapo Yesu hakuzungumzia aina gani ya chakula kula au kuruhusu kula vilivyo haramu! Bali alifundisha juu ya usafi Wa ndani ya moyo na si Wa nje ya mwili!
 
Last edited by a moderator:
wasabato bana eti hawali kitimoto,hawatumii majani ya chai,hawanywi cocacola, wanawake kunyoa afro ndo fashion..wasabato banaaa
 
Sometimes tunalalamikia sana lakin ukweli nikua hatumjui Mungu vzuri kwa sababu hatuna bidii ya kumtafuta, lakin hata tumtafutapo tumelenga zaidi kwa mahitaji ya mwilin kuliko rohoni ndio maana mwisho wa siku tunaishia kusemana na kusengenyana kwasababu hatumjui Mungu vzuri

Ayubu 22:21 Mjue sana Mungu ili uwe na amani.....
 

sabato ina maana ya mapumziko
ss unapozungumzia sabato unatakiwa uelewe walipewa maagizo ya kumpumzika kulingana na matukio husika kulingana na walawi
lkn kuwepo kwa sabato nyingi haitoi umuhimu wa kupumzika siku ya saba kama sabato ya bwana(kukumbuka uumbaji)
 

Hizo ulizotaja ni tabia zao binafsi na si mafundisho ya wasabato. Tungekuwa wabinafsi tungekuwa tunafanya juhudi kuhakikisha kila mtu anafahamu neno la Mungu katika usahihi wake pasipo uchakachuzi?. Kumbuka pia Yesu alituasa kuwa tupendane na akatuombea kuwa na umoja. Lakini sasa Yesu akasema, nikikuona unaenda kinyume na mapenzi ya Mungu, nitakuelekeza kwa neno la Mungu, na ukikataa alisema na awe kwako kama mtu wa mataifa. Kwa hiyo chunguza mienendo yako, kama ulikuwa mtu wa dini na bado walikutenga, basi labda walikuelewesha na mkaishia katika ugomvi wa kiimani, tofauti na hapo ni sawa na lile fungu linasema kwa maana nuru na giza havichangamani.
 
Hapo penye nyekundu, unajisemea wewe na nani? kama umelenga kwa wanadamu wote basi you are wrong. Unapodhani kwamba unamuabudu Mungu ili akupe ya mwilini, unapaswa ujue kuwa kuna wengine walishaamua kukabidhi maisha yao jumla kwa Mungu(ingawa si katika ukamilifu). Vivyo hivyo katika kumtafuta maana anasema mkinitafuta kwa bidii mtanipata kwa hiyo mimi namtafuta Mungu kwa bidii(japo si katika ukamilifu).
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…