Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,996
Warioba anazungumza kana kwamba msimamo wake na mawazo yake ndiyo sahihi na kwenda kinyume nayo ni hatari kwa taifa. Wamependekeza serikali tatu na inaonekana wamependekeza kwa sababu tu wanataka 'kuuokoa Muungano' si kwa sababu nyingine yeyote ile. Sasa hajatuambia kwanini wanataka kuuokoa Muungano? Lakini zaidi hajasema kama wananchi wengi wanataka Muungano uokolewe!
Sasa hivi inaonekana kuna kampeni ya wapenzi wa 'Serikali tatu" kulazimisha nchi nzima kufuata njia hiyo. Hii si sahihi na si kweli. Zipo njia nyingi za kuuokoa Muungano mojawapo na labda sahihi zaidi ni kuuvunja kwanza! Baada ya kuuvunja nchi mbili zikae chini na kuamua kama wanataka Muungano tena na kwa masharti gani. Lakini njia sahihi ambayo ni chini ya kuuvunja na kupendekeza kwenda serikali na nchi moja mifumo mbalimbali; ni kama ilivyo Canada, UK, China na hata Marekani. Serikali tatu siyo SULUHISHO pekee la kuukoa Muungano - kama unahitaji kuokolewa.
Kwa vile amekuwa Mwenyekiti wa Tume hii ya kusikiliza maoni Warioba anataka watu waogope kupinga misimamo ya tume hiyo na mapendekezo yake ambayo mengine yanapakana na upuuzi. Sasa wananchi wanayo haki, uwezo na sababu wa kupinga ikibidi mapendekezo yote au mapendekezo yale ambayo yanaonekana kusukumwa na ajenda zilizoshindwa.
Wanaotaka serikali tatu wana haki sawa ya kutoa maoni kama vile wale wanaotaka serikali moja; na yeye kama Mwenyekiti wa Tume kusukumiza maoni yake kwa wananchi ni kutumia nafasi yake vibaya!